Thx sabry001Mbona mijanaume mingi hapa inaongelea ndoa kama kitu kibaya hv? Kama yako imekuwa jehanam usimtishe mwenzako bwana.! Hongera kwa kufikia hatua hyo. MUNGU AKUPE MAARIFA NA AKILI YA KUISHI NA MKEO!
aissss!kumbe ni kifungo!!!!vipi baada ya hizo siku kenda akichoose kuendelea na PART 1?!Bado siku kenda uache kwenda club...
Bado siku kenda uache kulala na pensi
Bado siku kenda ratiba yako ya kijiweni iharibiwe vibaya
Bado siku kenda kabla hujaingia jela
Bado siku kenda uanze kupandwa vipresha kama unamrizisha
Bado siku kenda uanze kutoa ela ya mboga home
Bado siku kenda ukome kulala nje na home bila 'ruhusa'
Bado siku kenda washkaji zako ambao hawajaoa kukutenga
Bado siku kenda uanze kunyemelea nyumba ndogo
Bado siku kenda uache uasherati na uanze uzinzi
Bado siku kenda uwe na siku za kwenda kazini ukiwa umekasirika
Bado siku kenda uanze kuwaza kama mkeo anaibwa
BADO SIKU KENDA KABLA MUVI YA MAISHA YAKO KUANZA PART 2...
karibu huku kijiweni na kila la heri...
thx mkuuhongera mkuu kwa kuamua kuoa.
Bado siku tisa uanze kutafuta small house
Si kuwa unataka ila inatokana na matarajio yasiyofikiwaHapana siko hivyo mimi
Nakupatia mistari hii, ni mizuri sana na ni changamoto kwa wengine, MANI, zumbemkuu, saudari karibieni hapa niwapige Neno. Neno hili linatoka Mhubiri 4:7-
Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua.4.8 Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
4.9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
4.10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
4.11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?
4.12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
mpwa imebidi ni copy na ku'pest, hahahahahah, hii kali aloo.