Bado siku tisa tu

Bado siku tisa tu

Salaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam

Ndugu zangu Tarehe 6 April nitakuwa nikifunga pingu za maisha ( naoa).
Bado siku tisa tu nitakuwa na familia yangu
Bado siku tisa tu ambazo huyo muolewaji ataitwa Mrs

Ni hatua nzuri nafahamu, lkn maswali lukuki najiuliza

Chonde chonde

Kwa wale mlio pitia hii hatua naomba usia wenu

hongera sana.....
mi nakutakia maisha mema ndoa yenu iwe yenye upendo, amani na furaha muda wote!!!!!!!!
mkeo ni binadamu sio malaika akikosa jitahidi kutanguliza busara kwenye kusolve mambo yenu wala usipende kuwashirikisha marafiki mambo ya ndani.
 
bado siku tisa utaanza kujua kuwa ugumu wa ndoa ndio kipimo cha busara.
 
Nakupatia mistari hii, ni mizuri sana na ni changamoto kwa wengine, MANI, zumbemkuu, saudari karibieni hapa niwapige Neno. Neno hili linatoka Mhubiri 4:7-

Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua.4.8 Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
4.9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
4.10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
4.11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?
4.12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
 
Last edited by a moderator:
..kamanda hongera sana,cha msingi jua ndoa hazifanani,hakujawahi kuwapo na ndoa kama yenu duniani kooote so kile mnachoamini kinawezekana kwenu wawili ndicho fanyeni kwa bidii na maneno ya watu yapimeni pamoja mkimshirikisha Mungu mtafanikiwa siku zoote. Changamoto zitakuja lakini mtatuzi mzuri wa tatizo lenu ni nyinyi wenyewe, mtu wa tatu ni kubahatisha tuu.... natamani niongee mengi ila ngoja wadau wachangie ila hongeraaa sanaaaaaa.....
 
Nakupatia mistari hii, ni mizuri sana na ni changamoto kwa wengine, MANI, zumbemkuu, saudari karibieni hapa niwapige Neno. Neno hili linatoka Mhubiri 4:7-

Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua.4.8 Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
4.9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
4.10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
4.11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?
4.12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

Mpwa unavituko sana wewe! Lakini si vibaya tumkaribishe kwa mistari kama hiyo.
 
Hongera kufikia huo uamuzi sahihi wa kuitika wito wa Mungu, jiandae kuishi maisha ya ndoa yenye kumpemdeza Mungu wako na mengine yote yatafuata kwa ziada.
 
[Asante kwa usiaziri

QUOTE=ng`wana ong`wa kulwa;6003568]-

usitake ndoa yenu ifanane na ya watu fulani bali mfanye yenu kama mtakavyo iwe.
-mnaapoanza maisha muishi kwa maisha halisi mliyo nayo si ya kuigiza maana ukianza kwa kuigiza baadaye ukaacha mwenzio atatafsri kuwa umeanza kumchoka kama hutaweza kumlisha mkeo siku zote vema usimlishe toka mnapoanza maisha.
-Jitahidi kumuonyesha mkeo kuwa unampenda na ujue tafsiri ya upendo kwake nini...wengine kupendwa ni kumpa zawadi,wengine kuongea naye mara kwa mara,wengine kufinywa wengine ukimsaidia kazi mbalimbali za ndani atajua kweli unampenda.
-umpe kile kilichomtoa kwao.....chakula cha uzima.
-Hakikisha anakula na kushiba na kumpatia mahitaji mengine ya msingi.
-Na kumuomba Mungu azidi kuwapa neema.
Nakupa guarantee ya ndoa yenye furaha siku zote ukiyafanya hayo.[/QUOTE]
 
Karibu kwenye chama. Kila moja wenu amsome mwenzake na kumwelewa kikamilifu, ayakubali mema na mapungufu ya mwenzake. Mpendane na kuteteana kwa mvua na jua. Mkifanya hivyo mtafikia uzee mkiwa pamoja. Ninajua kwa vile ndoa yangu inaingia miaka 30 sasa.
 
Bado siku kenda uache kwenda club...
Bado siku kenda uache kulala na pensi
Bado siku kenda ratiba yako ya kijiweni iharibiwe vibaya
Bado siku kenda kabla hujaingia jela
Bado siku kenda uanze kupandwa vipresha kama unamrizisha
Bado siku kenda uanze kutoa ela ya mboga home
Bado siku kenda ukome kulala nje na home bila 'ruhusa'
Bado siku kenda washkaji zako ambao hawajaoa kukutenga
Bado siku kenda uanze kunyemelea nyumba ndogo
Bado siku kenda uache uasherati na uanze uzinzi
Bado siku kenda uwe na siku za kwenda kazini ukiwa umekasirika
Bado siku kenda uanze kuwaza kama mkeo anaibwa

BADO SIKU KENDA KABLA MUVI YA MAISHA YAKO KUANZA PART 2...

karibu huku kijiweni na kila la heri...

Hahahah daaah hii kali aisee kuna jamaa aliwahi niambia kwamba to a woman marriage is a beginning of a new chapter in her life lakini to a man its the end..maana vyote ulivyovitaja vinasignify the end..of somethings na pia ndo mana wanaume wengi wanasemaga nimefanya. Hivi na hivi parties alot ngoja nioe sasa
 
Salaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam

Ndugu zangu Tarehe 6 April nitakuwa nikifunga pingu za maisha ( naoa).
Bado siku tisa tu nitakuwa na familia yangu
Bado siku tisa tu ambazo huyo muolewaji ataitwa Mrs

Ni hatua nzuri nafahamu, lkn maswali lukuki najiuliza

Chonde chonde

Kwa wale mlio pitia hii hatua naomba usia wenu

Kiongozi hongera sana kwa hatua kubwa kama hii ambayo umefikia

Nakuombea na kukutakia heri

Waweza pitia hapa usikilize huu wimbo https://www.jamiiforums.com/mahusia...873-kwa-wanandoa-wote-with-love-and-care.html

Karibu chama TAMU
 
[thx sana

QUOTE=Gefu;6006211]..kamanda hongera sana,cha msingi jua ndoa hazifanani,hakujawahi kuwapo na ndoa kama yenu duniani kooote so kile mnachoamini kinawezekana kwenu wawili ndicho fanyeni kwa bidii na maneno ya watu yapimeni pamoja mkimshirikisha Mungu mtafanikiwa siku zoote. Changamoto zitakuja lakini mtatuzi mzuri wa tatizo lenu ni nyinyi wenyewe, mtu wa tatu ni kubahatisha tuu.... natamani niongee mengi ila ngoja wadau wachangie ila hongeraaa sanaaaaaa.....[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom