Bado siku tisa tu

Bado siku tisa tu

Fundi mahiri wa Ujenzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2012
Posts
4,708
Reaction score
3,632
Salaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam

Ndugu zangu Tarehe 6 April nitakuwa nikifunga pingu za maisha ( naoa).
Bado siku tisa tu nitakuwa na familia yangu
Bado siku tisa tu ambazo huyo muolewaji ataitwa Mrs

Ni hatua nzuri nafahamu, lkn maswali lukuki najiuliza

Chonde chonde

Kwa wale mlio pitia hii hatua naomba usia wenu
 
Bado siku 9 tu uingie kifungoni.
Bado siku 9 tu uwe vulnerable to..........
 
Ngoja na mimi niongezee kidogo,
---------------------------------------
Bado siku tisa tu, tutakula mpaka tinye,
Bado siku tisa tu, tukuone ukiwa umevaa suit,
Bado siku tisa tu, tukione ukiwa umenyoa nywele,
Bado siku tisa tu, NITAKUPA USIA WANGU.
-----------------------------------------
 
Ngoja na mimi niongezee kidogo,
---------------------------------------
Bado siku tisa tu, tutakula mpaka tinye,
Bado siku tisa tu, tukuone ukiwa umevaa suit,
Bado siku tisa tu, tukione ukiwa umenyoa nywele,
Bado siku tisa tu, NITAKUPA USIA WANGU.
-----------------------------------------

Hayo yote bado siku tisa tu ila naomba huo usia wako leo
 
Sali sana. Mwenyezi Mungu mwenye rehema nyingi akuongoze kwa kila jambo.
 
-usitake ndoa yenu ifanane na ya watu fulani bali mfanye yenu kama mtakavyo iwe.
-mnaapoanza maisha muishi kwa maisha halisi mliyo nayo si ya kuigiza maana ukianza kwa kuigiza baadaye ukaacha mwenzio atatafsri kuwa umeanza kumchoka kama hutaweza kumlisha mkeo siku zote vema usimlishe toka mnapoanza maisha.
-Jitahidi kumuonyesha mkeo kuwa unampenda na ujue tafsiri ya upendo kwake nini...wengine kupendwa ni kumpa zawadi,wengine kuongea naye mara kwa mara,wengine kufinywa wengine ukimsaidia kazi mbalimbali za ndani atajua kweli unampenda.
-umpe kile kilichomtoa kwao.....chakula cha uzima.
-Hakikisha anakula na kushiba na kumpatia mahitaji mengine ya msingi.
-Na kumuomba Mungu azidi kuwapa neema.
Nakupa guarantee ya ndoa yenye furaha siku zote ukiyafanya hayo.
 
Kama ulimshirikisha Mungu katika kumpata mwenzako mshirikishe na baada ya ndoa pia mambo yakakua poa.
 
Una uchaguzi wa kuifanya kuwa ndoa ya mfano mzuri au mbaya, Kwa vyovyote itakavyokuwa keep up the spirit na uelewe mkeo ni mtu na ana madhaifu mengi kama ya kwako maana naye ni binadamu, Jitahidi kujifunza kusamehe na kuvumiliana. Never regret this decision you are making.

Pili punguza kwaito kaka siku ya ndoa, Make sure kabla ya siku ya pili kuingia (Kabla ya saa sita usiku) uwe umetimiza ahadi(patano) yako ya ndoa ''NAKUOA LEO HII'' agreement hii hukamilika mnapokutana kimwili maana ndio muunganiko wa mtu na mtu kuwa mwili mmoja. and this has to happen the same day. (wengi wanaweza kupuuza hili lakini ni ndio NDOA yenyewe)

Tatu, Kama umewahi kuumiza watu wengine au kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wengine, kumbuka ku-denounce uhusiano huo maana bado unakuwaga binding kiroho hata kama mmeachana lakini mmewahi kufanya ngono. Unaweza kuta mambo yako yanapinda pinda kumbe ni maroho au mabalaa ya mmoja wa ex wako maana ukilala na mtu kimwili mnakuwa mmoja according to holy scripture unachukua baraka na laana zake same na yeye anachukua zako (Mnaunganika katika spiritual realm)

Wenye ufahamu zaidi watanisaidia kufafanua zaidi.
Nakutakia kila la heri na Maisha mema ndugu.
 
Upendo,uvumilivu,utii uaminifu na kuaminiana ni silaha yenu ya nyuklia zidi maadui wenu wote,Mwenyezi MUNGU awe kiongozi wenu,dictionary yenu muijaze maneno yafuatayo:nakupenda,pole,nisamehe,asante.........,
 
jitahidi uishi na mwenzio maisha yenu sio kama wale au mimi...
ukubali mapungufu yake...
mapenzi hayana mazoea...
 
Kama unapenda mpira mapema sana DSTV kama hukuwa nayo please mapema sana ifunge kwako kwa sababu tutakumith kule kwenye vibanda vyetu
 
Huu sasa uchokozi, utaacha Mpwa wangu aaahirishe jamani ujue...kwa muda huu wa siku tisa tunatakiwa kumu-encourage tu, kuwa ndoa ni tamu, hata kama kuna shubiri, hebu ngoja kwanza nipige simu nyumbani nione kama kaacha kununa au bado kanunua....hahahhaaaa May the Good LoRD; Jesus Christ Bless you forever,
Uliwezaji kusahau machungu ya kutomkuta sealed?!
 
Bado siku kenda uache kwenda club...
Bado siku kenda uache kulala na pensi
Bado siku kenda ratiba yako ya kijiweni iharibiwe vibaya
Bado siku kenda kabla hujaingia jela
Bado siku kenda uanze kupandwa vipresha kama unamrizisha
Bado siku kenda uanze kutoa ela ya mboga home
Bado siku kenda ukome kulala nje na home bila 'ruhusa'
Bado siku kenda washkaji zako ambao hawajaoa kukutenga
Bado siku kenda uanze kunyemelea nyumba ndogo
Bado siku kenda uache uasherati na uanze uzinzi
Bado siku kenda uwe na siku za kwenda kazini ukiwa umekasirika
Bado siku kenda uanze kuwaza kama mkeo anaibwa

BADO SIKU KENDA KABLA MUVI YA MAISHA YAKO KUANZA PART 2...

karibu huku kijiweni na kila la heri...
 
Back
Top Bottom