Bado siamini kama wote walikufa

Bado siamini kama wote walikufa

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
42,471
Reaction score
105,023
Mwanzoni, sikuamini kwamba walikuwa wamekufa. Kwa hakika nikiwaza sana namna gani wote waliweza kufa kwa pamoja... Wakati pale nilitambua kwamba ilikuwa kweli wamekufa, bado ilinichukua muda kitambo kuamini kama kweli walikua wamekufa.
Ama kwahakika, hili ni tukio lililo niliumiza sana na kunifanyia majeraha makubwa moyoni, na katika maisha yangu sikuwahi kuumizwa na kujeruhiwa moyoni kwa namna ile...
Siku zilivyo zidi kusogea nilijisikia kama kuishi bila wao haina maana. Kwa muda wa miezi mingi, nilikuwa ninalia kila siku.. Nilijilaumu kwa sababu niliacha mtu mwingine aendeshe gari lile kwasababu tu nilichelewa kurudi kutoka kwenye starehe.... Pengine hawangekufa ikiwa ni mimi ndie ningekua naendesha gari lile.
“Miaka kumi na sita imepita, na nimerudilia maisha yangu ya kawaida. Lakini, kifo chao kimeacha jeraha na sonona katika moyo wangu. Hiki ni kidonda ambacho hakijapona mupaka sasa, kwa babu nahisi kama pengine nisinge enda kwenye starehe, watu hawa wasinge kufa"

car-crash-unbelievable-552965_422_315.jpg
 
Kwenye picha ni gari au maboksi sio kwa kubonyea kiwango hiki.
 
polee sana.

usilaumu kwaiyoo ulitaka ufe wewe?? kifo chako kilikuwa bado ndo maana kikatokea kikwazo chakutoendesha wewe.

hiyoo gari inaelekea ilikuwa kwenye mwendo wa kasi sana.
 
Duu! naona pikipiki imeingia katikati ya gari,sidhani kama kuna aliyepona pale,labda dereva pikipiki.
R.I.P
 
sasa unaelewa ulichokiandika ?

hueleweki ,....hapo kuna muhtasari kwamba mlipata ajali wafariki ndg zako (not sure kama ni ndg au jamaa/washkaji)

any ways pole, kuna maisha baada ya kuondokewa na mtu wako wa karibu au ndugu....maana njia yetu ni moja!

jifunze kusimulia jambo, vinginevyo haina maana kuileta hapa
 
Duu! naona pikipiki imeingia katikati ya gari,sidhani kama kuna aliyepona pale,labda dereva pikipiki.
R.I.P
Motor rider aliruka kwa juu na kuenda mbali upande wa pili, hapo ni baada ya impact kubwa alio kutana nayo kwenye ubavu wa motokari
 
Usingeenda kwenye starehe na kuwemo ndani ya gari pengine tusingekujua humu ndani, Mungu huwa ana makusudi yake mkuu.

Kidonda cha kufiwa huwa hakiponi, kufiwa kusikie tu kwa jirani.

Pole Sana mkuu, tuzidi kuwaombea ndugu zetu.
 
sasa unaelewa ulichokiandika ?

hueleweki ,....hapo kuna muhtasari kwamba mlipata ajali wafariki ndg zako (not sure kama ni ndg au jamaa/washkaji)

any ways pole, kuna maisha baada ya kuondokewa na mtu wako wa karibu au ndugu....maana njia yetu ni moja!

jifunze kusimulia jambo, vinginevyo haina maana kuileta hapa
Sielewi nilicho kiandika mkuu.....
Samahani kama nimekukwaza asubuhi ya leo
 
Usingeenda kwenye starehe na kuwemo ndani ya gari pengine tusingekujua humu ndani, Mungu huwa ana makusudi yake mkuu.

Kidonda cha kufiwa huwa hakiponi, kufiwa kusikie tu kwa jirani.

Pole Sana mkuu, tuzidi kuwaombea ndugu zetu.
Pengine nami starehe ndio iliniokoa, asante kwa kuwaza nje ya box mkuu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom