Bado ninakukumbuka Rose

Bado ninakukumbuka Rose

Ni takribani miaka tisa (9) tangu nilipokutana na huyu binti ambaye mwanzoni sikujua kama nitakuja kuwa nae na ukaribu uliopelekea kuingia kwenye mahusiano.

Nakumbuka nilikutana na Rose nikiwa katika safari yangu ya kuelekea moja kati ya mikoa ya kanda ya ziwa ndipo kwa bahati nikatokea kukaa siti moja na huyu mrembo, kweli niliona ni kama bahati hasa kukaa siti moja na yule mrembo, baada ya salamu haikuchukua muda kuzoeana na story za hapa na pale ili kunogesha safari yetu ambayo tulitegemea ingetuchukua siku nzima kufika.

MAISHA YA MAHUSIANO

Baada ya mazoea ya muda mrefu tulijikuta tukiwa katika mahusiano ambayo kwa kweli yalikuwa yamejaa malengo kedekede huku kila mmoja akiwa na hamu ya kumjua mwenzie kiundani ata hivyo haikupita muda mrefu nadhani ni zaidi ya kama ya mwaka mmoja na nusu hivi ndipo penzi letu lilipoanza kuingiwa na mdudu mbaya.

Mwenzangu akawa ni mgumu katika kuwasiliana kejeli nyingi sana pamoja na hayo mtoto wa kiume nikapiga moyo konde huwenda akabadilika hivyo niliamua kuwa mvumilivu kidogo.

Lakini baada ya kutoona mabadiliko niliamua kukubali yaishe kwa kweli niliumia japo nilifanikiwa kuzoea na kuendelea na maisha mengine

KIFO SIKU YA KUMBUKUMBU YAKE YA KUZALIWA

Nakumbuka usiku wa kuamkia siku yake ya kuzaliwa miale kama ya sita na nusu usiku nilipokea ujumbe (sms) kutoka kwa Rose kuwa “ hata kama tumetengana bby huwezi ata kuni wish happy birthday” maneno haya yalinifanya niingiwe na utu nikamuomba radhi na nikamwambia sorry nilikuwa nangoja ifike kesho...ila alijibu jibu ambalo still mpaka leo linaniumiza sana “ vipo kama kesho nikifa mpenzi” nilicheka nikajua basi ni maneno tu

Nakumbuka siku hiyo ndipo penzi letu lilipochipua kwa mara nyingine kwani baada ya hapo kesho yake ikiwa ndio siku ya birthday yake kutokana na kuwa na shughuli nyingi na tulikuwa tunaishi mikoa tofauti nikaone ni vyema nisibiri jioni nimtafute tena

USIKU WA AJALI MBAYA ILIYOMPOTEZA KIPENZI CHANGU

Kwenye muda wa saa moja usiku niliona text ya Rose kuwa katika kusherekea birthady yangu ninakwenda kula nyama na baadhi ya marafiki zangu na moja kati ya marafiki zake niliwajua na ndiye aliyenipa taarifa hii mbaya ambayo ni ngumu kuisahau kwani wakiwa katika usafiri wa boda boda waligongana na roli na yeye pamoja na dereva wa bodaboda walifariki pale pale

Kwangu ilikuwa ngumu kuamini ili baada ya kupewa uhakika kweli iliniuma sana...!!! Usiombe kumpoteza mtu wa karibu

Basi zawadi pekee ambayo niliona kwako itakufaa ni kukuombea tu naamini Mungu alishakupokea kwani nina utaratibu wa kila jumapili ya mwanzo wa mwezi kukuombea kipenzi changu najua upo katika mikono salama ya Baba yako wa milele na utafurahi siku tukikutana tena

R.I. P Rose

View attachment 1184811
pole sana mkuu
 
Rose! Rose! Rose! umenikumbusha mbali sana mkuu kweli maisha usiku wa kiza nisiseme chochote namtakia kheri huko aliko.
 
R.I.P Rose..Pole sana mkuu..Haya majina ya rose sio mchezo tukianza na titanic rose alimtenda mume wake akaenda kwa jack
 
Mwenyezi mungu anasema.
WAOMBEENI MEMA MAREHEMU WENU.
ukiwatolea sadaka zinawafikia.
Ukiwaombea dua pia zinawafikia.
Maombi hayabadili na wala wanadamu hakuna wanachoweza fanya kwa niaba ya aliyekufa.
Ukifa umekufa husikii chochote na wala hakuna kinchobadilika
 
Ule uzi wa Heaven on Earth ulileta simanzi sana, lakini haukua na madhara sana hata alipoweka ile picha kwa kuwa wote ni wanawake na walikua marafiki walioshibana. Urafiki wao ulitambulika na kujulikana na wengine pia. Sikuona madhara makubwa kuwepo ile picha ya Carol.

Lakini kwa upande wako, maelezo yanaonyesha ukakasi wa mahusiano na si ajabu huyu binti tayari alishaamua kuendelea na maisha yake, sikuona haja ya kuweka wazi hadi picha yake kwenye maelezo yako, kumbuka huyu hakua mchumba wala mke. Mtunzie heshima yake.
 
Hata km una usafiri wako .hazikwepeki bado yaani

Hicho ndio kitu wengi hawakielewi, hasa ukiwa Dar kwenye foleni na mishemishe za kufukuzana na wakati. Hapo ndio usafiri binafsi au wa kukodi unapoonekana kukosa thamani unajikuta kudondokea kuweka rehani ya maisha kwa bodaboda.
 
Mara tiii taarifa ni ya uongo uliyopewa hilo sekeseke na sokomoko litakalo ukumba huo moyo wako

Mkuu pole sana maisha ndo haya haya na safar ni moja yatupasa tukubal hata kama hatutak
 
Back
Top Bottom