Bado nawaandama wageni..!

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,974
15,310
Mtu ndio mara ya kwanza anakuja kukutembelea. Kufika na kufika tu mlangoni hata kabla hajaingia ndani anaanza
..."He, ina maana viatu ndio mnawekaga hapa? Sasa kwanini msinunue ile nanii ya kuwekea? Nunueni ile bwana..."
Akifika sebuleni utamsikia "Ah, hii tivii hapa ilipokaa sio pazuri, mngeihamishia kwa pale kwenye kona"
Hujakaa sawa "Nanyie sasa ndio mapazia gani haya? Mbona hayamachi na rangi? Hapa nunueni ya brauni..!"
Kidogo "Heheee... kumbe na nyie wachina waliwapata. Haya makapeti ni bomu haya sijawahi kuona. Mi nilishatupa lile langu!"
Huku na kule mara "Ah, manyimbo gani hayo mmeweka? ina maana humu ndani hamna nyimbo za dini? Mnaishije? Hebu toeni
hayo manyimbo bana.. niwekeeni nanii..!"
Jamani, wewe ni mgeni au ndio mwenye nyumba? HAYO MASHARTI KAFANYE NYUMBANI KWAKO! PUMBAVU! NA USIJE TENA KWANGU!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom