Bado naiamini CCM!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado naiamini CCM!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ms Judith, May 30, 2012.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  nimehuzunishwa na habari za kuchomwa moto makanisa huko Zanzibar!

  napenda kusema kuwa, kanisa laweza kuchomwa moto na hata biblia pia!

  kisichoweza kuchomwa moto ni Mungu tu. wale maaskari wa kiyahudi walipijitahidi kumuua Mwana wa Mungu kwa ruhusa ya pilato aliyeshinikizwa na wakuu wa mafarisayo, lakini waliishia kukiri kuwa "alikuwa Mwana wa Mungu"

  sasa niwatoe hofu kabisa wapendwa, acheni makanisa yachomwe moto. nyie kesheni katika sala mkijua kuwa shetani katoka kifungoni na anajiua kuwa ana muda mchache tu!!

  zaidi sana nawakazia mzitazame siasa! wanasiasa wetu wamekosa weledi wa kufanya siasa na sasa nawafanya "mambo ya siasa"!! muungano wetu umeachwa bila maelezo ya kuwa una faida gani? vijana wasio na kazi, pesa wala akili, wanadanganywa kuwa wakivunja muungano watapata pesa toka OIC na jumuiya nyingine za kiislamu; na zitawawezesha kuwa matajiri!

  viongozi wetu wanachekelea anasa za mashangingi waliyolazimisha kujinunulia kwa jasho la wananchi masikini. wanajiita waheshimiwa, wanajitutumua kuchoma nyavu za kuvulia samaki ili waonekane "wachapa kazi", lakini mwisho wa siku hawana cha kujishaua mbele ya watanzania kuwa wamelitumikia taifa lao.

  siasa yetu imekufa, imebaki "biashara ya siasa"!

  hebu tuamke, tuamke kuipigania nchi yetu!

  Mungu ibariki Tanzania, ibariki Afrika,

  Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

  bado nakiamini Chama Cha Mapinduzi, kinaweza kutukomboa!

  Glory to God!
   
 2. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Useful thread!
   
 3. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Kwenye post yako nimeipenda hii......."viongozi wetu wanachelea anasa za mashangingi waliyolazimisha kujinunulia kwa jasho la wananchi masikini. wanajiita waheshimiwa, wanajitutumua kuchoma nyavu za kuvulia samaki ili waonekane "wachapa kazi", lakini mwisho wa siku hawana cha kujishaua mbele ya watanzania kuwa wamelitumikia taifa lao......" Je hawa wanatoka chama gani wanaoogoza kwa hayo? kiongozi wao ndio waliosababisha tukichukie chama kwa kushindwa kuchukua hatua kwa watu kama hawa na akiwemo yeye mwenyewe.
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuchoma makanisa na kidumu Chama cha Mapinduzi kuna uhusiano gani? We unafikiri ni CUF ndiyo wanaochochea hayo?
   
 5. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  asante sana mpendwa kwa kunitia moyo.

  ubarikiwe sana

  asante sana mpendwa kwa kuona hayo niliyoandika.

  viongozi wa CCM wamepoteza uwezo wa kuwa wnasiasa, si wanasiasa tena, tunu muhumu kama muuungano wanaichezea, wanasema ni uamsho! sio kweli, si uamsho, uamsho, kwani nani aliyekuwa aliyekuwa kalala?

  huu ni ulegevu wa uongozi, muungano wetu mzuri unaonekana sasa kama chanzo cha mifarakanoi ya kidini, kwa kweli tunataka viongozi wetu watuambie. nani aliyewalazimisha kuapa kuilinda katiba ya jamhuri ya "muungano" wa tanzania ikiwa hawana weledi wala ujasiri wa kuulinda muungano??

  mbarikiwe sna wapendwa

  Glory to God!

  nimesema "kidumu Chama cha Mapinduzi" kwa kuwa ndicho chama chennye dhamana ya kuulinda na kuuenzi Muuungano wetu mzuri "kwa sasa"

  ubarikiwe sana mpendwa,

  Glory to God!
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umeongea mambo mengi mazuri,lakini sijaona sababu yeyote ya msingi kwanini unakipenda chama cha magamba,chama kinachokaribia kuzikwa.Amka bwana,CCM hakina jipya kwa watanzania.
   
 7. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,854
  Likes Received: 1,297
  Trophy Points: 280
  HATA MIMI NINAIMANI NAO ENDAPO TU WATAACHA UMIMI NA KUANGALIA KWANZA WANAINCHI.
  oVEr!
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Nadhani kipindi kilichosemwa katika Isaya 60:2 unaanza kuwadia. Shetani ameanza kutumia dini yake kuteketeza Kitabu kitakatifu cha Mungu.
  .
  "LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  CCM kama chama ni kweli hakina jipya, ila sisi wanachama wake bado tunaamini kuwa CCM inaangushwa na viongozi wake. na hili linatupa changamoto si ya kuuliza "CCM imenifanyia nini" bali "mimi nitaifanyia nini CCM"

  tarajia kuniona katika harakati za kuijenga CCM karibuni

  ubarikiwe sana mpendwa

  Glory to God!
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Una Imani na Chama Mfu?
   
 11. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ishimaei mtoto haramu wa Ibrahimu anapambana na Isaka aliepewa mamlaka na Mungu kuwa mtawala wake!
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  kwa kujibu swali lako, nasema "yes",

  nina imani na Chama cha Mpapinduzi!!

  CCM si chama mfu, CCM kitashiunda tena uchaguzi wa 2015, kitashika dola tena!! na kwa mshangao wako, hao "wafu" unaowaona CCM hawatakuwepo tena, watakuwa wameishaondoka na makundi ya "wafu" wenzao. sisi tulio hai tutakaokuwa tumesalia tutakuwa pamoja na watanzania wenzetu nchi nzima tukiujenga uchumi wa kijamaa kwa manufaa ya jamhuri ya muungano wa tanzania na watu wake wote!

  kidumu Chama Cha Mapinduzi!!

  mbarikiwe sana wapendwa,

  Glory to God!
   
 13. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Duuu....

  Labda natakiwa kuelewa tofauti hapa!!

  Ila nikupe hongera kwa msimamo wako.......
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ms. Judith,
  umekiri mwenyewe kuwa viongozi wetu wanatumia mashangingi kwa anasa, na hapo hapo umesema bado unaiamini ccm.
  Unatuchanganya mummy! Funguka bana
   
 15. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  tofauti gani tena mpendwa?

  hebu funguka zaidi tupate tujadili vizuri.

  ubarikiwe sana

  Glory to God!
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  asante mpendwa kwa kunisoma,

  kuna tofauti kubwa sana kati ya CCM na viongozi wa CCM.

  ile kusema naiamini CCM ni kusema bado ninaamini imani, lengo na madhumuni ya CCM!

  ukisoma katiba ya CCM utaviona vyote hivyo tena vizuri sana. hayo hayajawahi kubadilika na yakitokea kubadilika huwa ni baada ya kitambo kirefu. ila viongozi wa CCM wamebadilika sana, tokea enzi za mwalimu hadi leo, tumeshuhudia vioja vya viongozi hadi wengine wanatia hata aibu kuwasimulia. hawa ndio "magamba" halisi! hao ndio akina lusinde wa mtera wenye mashati yanayometameta ya kijani ya ki-CCM huku mioyoni mwao imo imani mbaya kuliko hata aliyokuwanayo marehemu saddam husein!!

  sasa kama hiyo ndiyo CCM ya sasa, sote tunapaswa kujiuliza, sie tunaoendelea kuiamini CCM, tutaifganyia nini hii CCM ya sasa??

  karibu sana mpendwa,

  Glory to God!
   
 17. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  we ni ndugu na nape?manake hueleweki unajua kbsa hilo lichama lenu liliaminika sna na kupewa nafasi ya kukamata dola miaka 35.unadhani hyo itajirtdia tena?mwisho wenu wakuiba umefika mwisho.nakumbuka member mmoja humu jf alisema ukiona mtu anaitetea ccm ujue nae ana maslahi binafsi.umepotea wewe baki na imani zako hizo za kufikirika ila hali halisi unaijua ccm kwisha kazi
   
 18. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Content katika thread yako ni nzuri, ningefurahi zaidi kama ungebadilisha heading! Hapo naona umeharibu.... ahh labda nawe kwakuwa una haki pia. Na ulivyomalizia pia uliharibu zaidi, Hayo maneno "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI" yananikumbusha wakati niko darasa la pili, hata akifika katibu wa kata shuleni mnaimba hizo nyimbo, lakini siku za leo nikisikia huwa napata machungu sana. Maana ninapopita mtaani na kuona watu wanalalamika na maisha nathubutu kusema ni CCM. Nikiona mtu anakosa mlo mmoja kila siku pia nazidi kupata uchungu zaidi.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Duh, hii sasa ni hatari! Kwanza ninavyojua, kuiamini CCM ni pamoja na kukubaliana na maamuzi yanayochukuliwa na uongozi wa CCM. Ms Judith, je unakubaliana na wahenga waliosema kuwa"you cant eat your cake and have it!" Sasa hii ya kwako inakuwa zaidi ya unafiki, itakuwaje udai unaiamini CCM na wakati huo huo unaulaumu uongozi wa CCM ambao wewe huyo huyo ulishiriki kuuchagua? Halafu pamoja na kasoro zinazojitokeza kila leo, bado unapata wapi ujasiri wa kudai CCM kitashinda tena uchaguzi wa 2015 na kushika dola, hii jeuri unaitoa wapi tena! Je hao watakaoichagua tena CCM ni hawa hawa Watanzania wanaopigika kwa sera za kifisadi za CCM au wananchi wa taifa lipi hilo?

  Ms Judith, nakuomba uwe mkweli kwa Watanzania hata kama umeamua kujidanganya kwa nafsi yako, kitu gani kitaibadilisha CCM baada ya miaka karibu 40 ya huu utawala wa kifisadi. Unadai wakeretetwa wasiulize CCM imewafanyia nini na badala yake wajiulize wao wameifanyia nini CCM, je wewe binafsi umefanya nini kukinusuru CCM? Je aliyekuwa muumini wa NAZIISM hivi hata leo akipatikana anaweza akakwepa kufikishwa mbele ya sheria kwa utetezi wa ati yeye alikuwa muumini tu? Ms Judith, ni watu kama wewe mnaowapa vichwa hawa mafisadi walioko madarakani kuwa wasiwe na wasiwasi wowote hata wakiiba namna gani, hakuna wa kuiondoa CCM madarakani, how sad...!

  Kwa kumalizia ni kwamba watu wenye mawazo kama yako ni hatari kwa taifa kuliko hata hao viongozi unaojaribu kuwatupia lawama. Baba wa Taifa, aliwahi kusema kuwa, pamoja na kuwa mwasisi wa CCM, alikuwa radhi kukihama kama hakukubaliana na mwelekeo wake kwa sababu CCM si mama wala baba. Sasa leo anatokea Ms Judith ambaye hajui hata anakotoka au anakokwenda na kudai hatahama CCM hata ikiboronga namna gani, kuna ulimbukeni unaozidi huu? Hapana, lazima ifike wakati tuachane na ujinga huu wa kung'ang'ania hata kile kisichokuwwa na uwezo wa kutufikisha popote, huu ni mwaka wa kujikomboa kutoka makucha ya CCM na ambaye hayuko nasi, bye bye...!
   
 20. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Hebu nitajie Rais unayemuona wewe atafit kwa CCM mwaka 2015, Kisha nitajie na makamu wake, na pia nitajie na waziri mkuu wake.
  Kisha baada ya hapo nitajie Baraza la Mawaziri 20 tu, plz manaibu usiwaweke...
   
Loading...