Bado naiamini CCM!!!

Bado naiamini CCM!!!

Duh, hii sasa ni hatari! Kwanza ninavyojua, kuiamini CCM ni pamoja na kukubaliana na maamuzi yanayochukuliwa na uongozi wa CCM. Ms Judith, je unakubaliana na wahenga waliosema kuwa"you cant eat your cake and have it!" Sasa hii ya kwako inakuwa zaidi ya unafiki, itakuwaje udai unaiamini CCM na wakati huo huo unaulaumu uongozi wa CCM ambao wewe huyo huyo ulishiriki kuuchagua? Halafu pamoja na kasoro zinazojitokeza kila leo, bado unapata wapi ujasiri wa kudai CCM kitashinda tena uchaguzi wa 2015 na kushika dola, hii jeuri unaitoa wapi tena! Je hao watakaoichagua tena CCM ni hawa hawa Watanzania wanaopigika kwa sera za kifisadi za CCM au wananchi wa taifa lipi hilo?

Ms Judith, nakuomba uwe mkweli kwa Watanzania hata kama umeamua kujidanganya kwa nafsi yako, kitu gani kitaibadilisha CCM baada ya miaka karibu 40 ya huu utawala wa kifisadi. Unadai wakeretetwa wasiulize CCM imewafanyia nini na badala yake wajiulize wao wameifanyia nini CCM, je wewe binafsi umefanya nini kukinusuru CCM? Je aliyekuwa muumini wa NAZIISM hivi hata leo akipatikana anaweza akakwepa kufikishwa mbele ya sheria kwa utetezi wa ati yeye alikuwa muumini tu? Ms Judith, ni watu kama wewe mnaowapa vichwa hawa mafisadi walioko madarakani kuwa wasiwe na wasiwasi wowote hata wakiiba namna gani, hakuna wa kuiondoa CCM madarakani, how sad...!

Kwa kumalizia ni kwamba watu wenye mawazo kama yako ni hatari kwa taifa kuliko hata hao viongozi unaojaribu kuwatupia lawama. Baba wa Taifa, aliwahi kusema kuwa, pamoja na kuwa mwasisi wa CCM, alikuwa radhi kukihama kama hakukubaliana na mwelekeo wake kwa sababu CCM si mama wala baba. Sasa leo anatokea Ms Judith ambaye hajui hata anakotoka au anakokwenda na kudai hatahama CCM hata ikiboronga namna gani, kuna ulimbukeni unaozidi huu? Hapana, lazima ifike wakati tuachane na ujinga huu wa kung'ang'ania hata kile kisichokuwwa na uwezo wa kutufikisha popote, huu ni mwaka wa kujikomboa kutoka makucha ya CCM na ambaye hayuko nasi, bye bye...!


Mkuu thanx for usefull post...
 
[h=2]Walipata Kunena[/h]
  • Sikuwa na njia ya kumpinga mgombea wa CCM aliyepitishwa na ngazi zote zinazotakiwa na chama, hata kama hafai. Ukimpinga watauliza; huyu Mrema vipi, labda zi mwenzetu. Mtu kama Kitwana Kondo kwangu mimi kama Mrema, Kitwana Kondo hafai kuwa diwani wa Kariakoo. Lakini mimi Mrema, kama CCM, Kitwana Kondo anafaa kuwa diwani wa Kariakoo


    Mrema na u-CCM​



 
Ms Judith mwanzo umeandika maneno ya busara lakini mwisho pumba tupu au wewe ni Risasi Mwaulanga nini
 
Duh, hii sasa ni hatari! Kwanza ninavyojua, kuiamini CCM ni pamoja na kukubaliana na maamuzi yanayochukuliwa na uongozi wa CCM. Ms Judith, je unakubaliana na wahenga waliosema kuwa"you cant eat your cake and have it!" Sasa hii ya kwako inakuwa zaidi ya unafiki, itakuwaje udai unaiamini CCM na wakati huo huo unaulaumu uongozi wa CCM ambao wewe huyo huyo ulishiriki kuuchagua? Halafu pamoja na kasoro zinazojitokeza kila leo, bado unapata wapi ujasiri wa kudai CCM kitashinda tena uchaguzi wa 2015 na kushika dola, hii jeuri unaitoa wapi tena! Je hao watakaoichagua tena CCM ni hawa hawa Watanzania wanaopigika kwa sera za kifisadi za CCM au wananchi wa taifa lipi hilo?

Ms Judith, nakuomba uwe mkweli kwa Watanzania hata kama umeamua kujidanganya kwa nafsi yako, kitu gani kitaibadilisha CCM baada ya miaka karibu 40 ya huu utawala wa kifisadi. Unadai wakeretetwa wasiulize CCM imewafanyia nini na badala yake wajiulize wao wameifanyia nini CCM, je wewe binafsi umefanya nini kukinusuru CCM? Je aliyekuwa muumini wa NAZIISM hivi hata leo akipatikana anaweza akakwepa kufikishwa mbele ya sheria kwa utetezi wa ati yeye alikuwa muumini tu? Ms Judith, ni watu kama wewe mnaowapa vichwa hawa mafisadi walioko madarakani kuwa wasiwe na wasiwasi wowote hata wakiiba namna gani, hakuna wa kuiondoa CCM madarakani, how sad...!

Kwa kumalizia ni kwamba watu wenye mawazo kama yako ni hatari kwa taifa kuliko hata hao viongozi unaojaribu kuwatupia lawama. Baba wa Taifa, aliwahi kusema kuwa, pamoja na kuwa mwasisi wa CCM, alikuwa radhi kukihama kama hakukubaliana na mwelekeo wake kwa sababu CCM si mama wala baba. Sasa leo anatokea Ms Judith ambaye hajui hata anakotoka au anakokwenda na kudai hatahama CCM hata ikiboronga namna gani, kuna ulimbukeni unaozidi huu? Hapana, lazima ifike wakati tuachane na ujinga huu wa kung'ang'ania hata kile kisichokuwwa na uwezo wa kutufikisha popote, huu ni mwaka wa kujikomboa kutoka makucha ya CCM na ambaye hayuko nasi, bye bye...!


Nashukuru kwa POST yako umemwelewesha sana huyo Ms Judith ambaye anajifanya sikio la kufa.
Na nimeipenda sana AVATA yako yenye kaburi la CCM
 
kuna tofauti kubwa sana kati ya CCM na viongozi wa CCM.

Ni lazima tukubali viongozi ndio taswira ya CCM na CCM haiwezi kuwa bila ya hao viongozi, kuvitenganisha vitu hivi viwili ili vikidhi dhamira yako ni upotoshaji usio na mantiki..! Hukatazwi kuendeleea kuiamini hata kama kuna walafi wanaokosesha watu madawa hospitalini lakini nyinyi bado mna imani nao na mnashindwa kuwachukulia hatua stahiki hata kama kuna ushahidi kiasi gani...kama bado wanashindwa kusimamia maslahi ya wengi na nyie mnashiriki kwa namna moja au nyingine kubariki hayo maamuzi nashindwa kukutofautisha na hao 'viongozi'..!

Nilitegemea 'mpendwa' kusimamia haki na ukweli na kujitenga na unafiki,lakini kukaa ndani ya nyumba ilijaa uvundo na kujitanabaisha kwamba u-msafi mashaka ni mengi...Imani njema hata hivyo..!
 
mpendwa,

CCM kama chama ni kweli hakina jipya, ila sisi wanachama wake bado tunaamini kuwa CCM inaangushwa na viongozi wake. na hili linatupa changamoto si ya kuuliza "CCM imenifanyia nini" bali "mimi nitaifanyia nini CCM"

tarajia kuniona katika harakati za kuijenga CCM karibuni

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!

Kwa jinsi hii, ipo siku utataka kumhubiria Shetani ukifikiri kuwa atabadilika
 
Back
Top Bottom