Bado Mama Samia hajaingia kwenye 18 zangu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
BADO MAMA SAMIA SULUHU, HAJAINGIA KWENYE 18 ZANGU.

Na, Robert Heriel

Tangu Rais Samia alipoingia kwenye utawala, watu wengi wamekuwa wakihitaji maoni yangu juu ya utendaji kazi wake. Wengi wamekuwa wakinambia kuwa mbona sijaandika makala zozote zinazomlenga SSH. Ni kweli kabisa, mpaka muda huu sijazungumzia jambo lolote kumhusu Mama Samia, na hata andiko hili bado haliwi sehemu ya kumzungumzia yeye bali ni sehemu ya kuwajibu kwa pamoja wale wote wananiuliza kwa njia mbalimbali.

Sijamzungumzia Mama Samia mpaka sasa kwa sababu; Bado hajaingia kwenye 18 zangu, bado yupo nje ya 18, bado yupo nje ya boksi hivyo siwezi kumzungumzia mtu ambaye hayupo Eneo la hatari

Ndani ya 18 ni eneo hatarishi sana ambalo lolote linaweza kutokea, Mama samia awapo ndani ya 18 hucheza kwa kufuata kanuni za mchezo, hachezi valuvalu hivyo ni ngumu kusababisha Penalt. Eneo la 18 kisiasa linahitaji kiongozi mtulivu sana anayejua namna ya kuondoa hatari pasipo kusababisha hatari kubwa. Katika hili Mama Samia naona kama anacheza nalo kwa umakini wa hali ya juu.

Ndani ya 18 kisiasa hutokea pale maadui wanaposhambulia, hasa maadui wanaojua kuchenga na kuchezea mpira wa siasa. Hivyo Rais kama Full back anapaswa awe makini kuhakikisha hatari yoyote haiwezi kutokea ikiwemo Kadi ya njano, nyekundu, Penalt au Goli kabisa, Siku zote Wananchi ndio Magolikipa.

Washambuliaji wa Kisiasa katika uwanja wa siasa huwa wa namna mbalimbali, kama vile;
1. Wanasiasa waupinzani
2. Wafanyabiashara wakubwa wasiopenda kulipa kodi
3. Wawekezaji wa kimataifa wanaohitaji kunyonya Rasilimali za nchi
4. Wanaharakati

Makundi hayo ni timu moja ambayo huungana mara kadhaa kuishambulia serikali inapobana maslahi yao, ingawaje hutumia kigezo cha kutetea wananchi kama mwamvuli lakini nyuma yake huwa na agenda zao za siri.

Winga wa kushoto na Kulia huwa ni wanaharakati wa haki za binadamu, na wale wanaharakati viongozi wa dini;
Wafungaji huwa ni Wanasiasa hawa hucheza namba tisa au kumi kabisa.
Viungo washambuliaji huwa ni Wawekezaji wa kimataifa, hawa hujitokeza indirect way kwenye mchezo
Viungo wakabaji na mabeki huwa Wafanyabiashara wakubwa ambao hujificha nyuma ili wasifahamike lakini hutoa sapoti kimya kimya.
Golikipa siku zote ni wananchi.

Hii ni kusema Mwananchi anadaka pande zote, upande wa Serikali na pia upande wa timu pinzani. Kumaanisha matokeo yoyote katika mechi hiyo lazima yamuathiri Mwananchi.

Mama Samia kitu anachokimudu mpaka sasa kwenye mtanange huu ni kuwa anajua kucheza na washambuliaji wa timu pinzani pasipo kusababisha madhara.

Wakati washambuliaji wakishambulia yeye hujua namna ya kupoteza na kuharibu mipira yao kwa namna ya akili pasipo kusababisha Faulu au penati.

Washambuliaji wa kisiasa kama Kina Tundu Lisu, Kina Freeman Mbowe, Zitto Kabwe na wengine wanaposhambulia na kuingia kwenye boksi Mama Samia hatoki mzima mzima kuwachezea Rafu isipokuwa anawaharibia direction ya mpira kwa kuugusa mpira kidogo tuu.
Winga za kushoto na kulia ambazo ni wanaharakati wanapopandisha mipira na kuingiza Cross ndani ya box, Mama Samia anajua namna ya kuokoa mipira iwe kwa kichwa au kubutua mbele. Winga ya kushoto kama Kigogo2014 akichukua sub ya Mange kimambi, alafu upande wa kulia huwa Maria Sarungi na Fatume Karume hawa wakiachia Cross ndani ya boksi inahitaji utulivu kucheza na mipira hiyo.


Hii ni tofauti na utawala wa awamu iliyopita ambapo JPM hakuwa mzuri wa kuzuia mipira ya wachezaji machachari waingiapo ndani ya Boksi. Ilikuwa rahisi sana kwa JPM kucheza Rafu hata kwenye eneo la hatari na kusababisha kadi nyekundu na Penalt papo hapo.
Ilikuwa ni kawaida JPM kushindwa kuzuia winga za kushoto na kulia na kujikuta akicheza Faulu zisizo na ulazima hali iliyokuwa inahatarisha timu.

JPM alijitahidi sana kwenye kubutua butua, hata hivyo alikuwa mtu wa Counterattack.

Mama Samia hajaingia kwenye 18 zangu kwa sababu bado anajua kucheza kwa ujanja pasipo kukwatua wachezaji na kusababisha Kadi nyekundu au Penalt.

Mama Samia pia anacheza mpira as a team, hang'ang'anii kila penalt au Faulu au kona apige yeye. Hii ni Tofauti na JPM ambaye kila Penalt, Faulu au kona anapiga yeye.

Kila pasi anataka apewe yeye hali iliyomfanya apewe lawama kila muda kwani kila mara yeye ndio yupo na mpira, JPM pia kila mtu alikuwa anataka kumkaba yeye, sio ajabu faulu na penalt zote yeye ndio sababu.

Mama Samia bado hayupo kwenye 18 zangu kwa sababu bado hajaweza kusababisha kadi nyekundu iliyomuondoa mchezaji uwanjani. Bado hajamkwatua wala kusababisha Faulu yoyote.

Mama Samia bado hayupo kwenye eneo la hatari kwa sababu hajadhulumu mtu roho yake, na hapa ndipo kiongozi yeyote akiingia madarakani anapaswa awe napo makini sana kuliko eneo lolote lile.

Ingawaje ni mapema lakini mpaka sasa mambo ni shwari, mechi bado inaendelea mpira umetulia kila mmoja anapanga ku-score.
Haki na sheria za mchezo zinazingatiwa hivyo mchezo ni wafuraha.

WITO; Mama endelea kuzingatia haki na sheria za mchezo, ingawaje uwe makini kwa wanakusifia sana kama nilivyosema hapo juu timu pinzani hujua kuchezesha wachezaji wake vyema, hata hivyo jambo la hakika ambalo sitakuonea haya ni kuwa HAKI HUINUA TAIFA, HAKI HUINUA JINA LAKO, HAKI HUINUA NA KUBARIKI KIZAZI CHAKO. Ukitenda kwa haki taifa hili litafurahi kama linavyoendelea kufurahi. Ukitenda haki huna haja ya kuomba kuombewa kwani kutenda haki ni maombi tosha yatakayo kulinda.

Lakini usipotenda haki, mimi Taikon nakuhakikishia hautafika popote, nitakuandama kwa kukukemea, na kama utakuwa na kiburi basi ni wazi mechi UTAPOTEZA kama Mungu aishivyo, tena jina lako litakuwa jina la aibu, tena litakuwa kama tusi mbele za watu.

Kama ilivyoandikwa kuwa Usiwe muovu Kupita kiasi usije ukaangamia kwa upesi,
Nakuombea uwe na uwezo wa kutenda mema, na ujue namna ya kukaba mipira ya hatari ndani ya boksi.

Ulikuwa nami mwana wa Tibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Mvomero, Morogoro
 
Chawa wa Bashite katika ubora wake

Kama hukuwin enzi za mwendazake na genge lenu,awamu hii unakula kwa urefu wa kamba na Mama hataki mamluki wa kisiasa
 
Mtawala lazima kuna wakati unapaswa kucheza rafu, tena ya kuvunja mguu kabisa kiasi cha kutorudi mchezoni tena. Hii ilikuwepo tangu enzi na enzi, vitabu takatifu vimetueleza, watawala kuna wakati wanalazimika kufuta mtu duniani kwa maslahi ya watawaliwa.

Mpinzani anajua kupinga tu, hata jema anapinga tu, anachochea vita, unategemea mchochezi anayeta kuvuluga amani ya nchi afanyweje?

Ni kumsimika kuzimu. Full stop.
 
Mtawala lazima kuna wakati unapaswa kucheza rafu, tena ya kuvunja mguu kabisa kiasi cha kutorudi mchezoni tena. Hii ilikuwepo tangu enzi na enzi, vitabu takatifu vimetueleza, watawala kuna wakati wanalazimika kufuta mtu duniani kwa maslahi ya watawaliwa.

Mpinzani anajua kupinga tu, hata jema anapinga tu, anachochea vita, unategemea mchochezi anayetaka kuvuluga amani ya nchi afanyweje?

Ni kumsimika kuzimu. Full stop.
 
Mtawala lazima kuna wakati unapaswa kucheza rafu, tena ya kuvunja mguu kabisa kiasi cha kutorudi mchezoni tena. Hii ilikuwepo tangu enzi na enzi, vitabu takatifu vimetueleza, watawala kuna wakati wanalazimika kufuta mtu duniani kwa maslahi ya watawaliwa...
Duh kwa kweli mmewasimika wengi awamu ile. Lkn na nyie Mungu kamsimika dikteta wenu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom