Bado Kilimo cha Parachichi kinalipa 2023

JOSEPHAT_07

JF-Expert Member
Aug 8, 2011
290
162
Wadau wa kilimo naomba kuuliza nimesoma komnti na maelezo watu waliondika kuhusu kilimo cha maparachichi za 2021.

Naomba kuuliza vip kwa miaka hii 2023 bado kilimo cha maparachichi kinalipa?

Je, vipi kuhusu soko? Ukishalima uangaiki kutafuta wateja?

Naomba mnisaidie majibu mda si mrefu nataka kuwekeza huko.
 
Kilimo bado kinalipa kama kawaida, changamoto ni miundombinu katika mfumo mzima kuanzia shambani mpaka sokoni. Soko lipo sana, ila hatujaamua kulifanya liwe active. Sera na taratibu za biashara kwetu bado zinazingua mno.

Kama unataka kuwekeza, angalia factors nyingi, usiangalie moja tu, mfano; maji, usafiri, mvua, usalama, uaminifu wa wenyeji, na huduma za kijamii kama zipo karibu.

Habari nzuri ni hii, tayari park houses nyingi zinajengwa na locals, parachichi processing plants zinajengwa pia, kwa hiyo hata rejects zitapata masoko.
 
Wadau wa kilimo naomba kuuliza nimesoma komnti na maelezo watu waliondika kuhusu kilimo cha maparachichi za 2021.

Naomba kuuliza vip kwa miaka hii 2023 bado kilimo cha maparachichi kinalipa?

Je, vipi kuhusu soko? Ukishalima uangaiki kutafuta wateja?

Naomba mnisaidie majibu mda si mrefu nataka kuwekeza huko.
Wakulima wa maparachichi mbona kimya ?
 
Wadau wa kilimo naomba kuuliza nimesoma komnti na maelezo watu waliondika kuhusu kilimo cha maparachichi za 2021.

Naomba kuuliza vip kwa miaka hii 2023 bado kilimo cha maparachichi kinalipa?

Je, vipi kuhusu soko? Ukishalima uangaiki kutafuta wateja?

Naomba mnisaidie majibu mda si mrefu nataka kuwekeza huko.
Mkuu, kuna usemi wa Kigeni usemao "nothing is common but changes".

Hakuna kitu kitakachobaki kama kilivyo siku zote. Madhalani, wachumi watakuambia bei ya bidhaa huweza kuathiriwa na sababu mbalimbali, ikiwemo kile wanachokiita ELATICITY OF DEMAND SUPPL (sijui kama mimepatia, mimi siyo mchumi).

Kwa hiyo, ukiweza kubaini zao litakalokuwa adimu miaka mitatu ijayo, na ukalilima, kipindi hicho kitakapofika watu watasema una bahati. Na watu watakapoona unavyopata mihela kipindi hicho, wengi nao watakimbilia kulima hilo zao, na hivyo kusababisha wingi wa hayo mazao sokoni, na yakishakuwa mengi kuzidi uhitaji, hapo ndipo wanunuzi nao hushusha bei.

Hata hivyo, si lazima iwe hivyo.

Ila ni kawaida kwa bei ya mazao kubadilika sokoni. Dhahabu, almasi, na madini mengine bei zao hubadilika sokoni kwa kupanda au kushuka kutegemeana na sababu mbalimbali, na ndivyo ilivyo pia kwa mazao kama mahindi, parachichi, korosho, kahawa, n.k.

Kwa hiyo, kama una eneo kubwa, panda zaidi ya zao moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom