Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Nakubaliana mkuu ,lie picha ya mwana CHADEMA aliyeuwawa Arusha haikupaswa kubandikwa hadharani.
Aliyepiga picha amepungukiwa na ustaarabu kufikia Hali ya kumdhalilisha marehemu.
Naunga mkono hoja.Maiti haitoi ridhaa.
Bora mseme nyinyi viazi... mimi mhogo huwa naambiwa nina mizizi. Nilitukanwa sana, nilishambuliwa sana na nilipuuzwa sana wakati nilipolaani kwa nguvu zote member mmoja anayeitwa Crashwise alipotundika picha za wale vijana waliouawa Arusha juzi juzi. Na kuonyesha jeuri yake jana ameweka tena za mwenyeketi wa Chadema aliyechinjwa. Mimi nadhani uongozi wa JF una wajibu wa kukomesha huu ushenzi uliovuka mipaka. Picha za marehemu siku hizi zimegeuka burudani ya macho. Ni unyama uliopindukia.Hili nimeshalisema sana hususan kwenye thread za Crashwise na kuambulia matusi
Ustaarabu hatuna wala haihusiani na misitu wala majangwa
Alieye onyesha jeuri ni wewe na group lako mnaoendela kuwauwa...Bora mseme nyinyi viazi... mimi mhogo huwa naambiwa nina mizizi. Nilitukanwa sana, nilishambuliwa sana na nilipuuzwa sana wakati nilipolaani kwa nguvu zote member mmoja anayeitwa Crashwise alipotundika picha za wale vijana waliouawa Arusha juzi juzi. Na kuonyesha jeuri yake jana ameweka tena za mwenyeketi wa Chadema aliyechinjwa. Mimi nadhani uongozi wa JF una wajibu wa kukomesha huu ushenzi uliovuka mipaka. Picha za marehemu siku hizi zimegeuka burudani ya macho. Ni unyama uliopindukia.
Mimi ninaamini wewe MMJJ una mchango mkubwa sana JF kwanini msiweke sheria ya kuzui kuweka picha za marehemu tukajua moja kuwa hairuhusiwi.Siyo ya huyo tu; tumeliona kwenye Kanumba, tumeona wale vijaan wanne, tumeona ajali ya Mbatia na Regia, tumeona ni kama voyeurism ya aina fulani hivi!!!
nimeangalia leo ajali ya Bronx huko NY ambapo watu saba wamekufa papo hapo baada ya gari lao kuanguka kutoka 'barabara za juu kwa juu'. Hakuna mtu aliyepiga picha za maiti kuonesha na hata gari lenyewe lilipoondolewa pale kwa ajili ya uchunguzi lilikuwa limefunikwa turubai!