Bado baadhi ya Watanzania tunatabia za kimsitunisituni; tabia za kijima!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Ninaamini baadhi yetu bado tuna masalia ya tabia za kimsituni situni hivi! Kuna faida gani ya kukimbia kupiga picha marehemu ambaye hajahifadhiwa vizuri? Ni ubinadamu gani huu tulionao kwamba badala ya kumhifadhi mwenzetu na heshima ya utu wake tunachukua camera zetu na kumpiga picha kuutangazia ulimwengu? Kama siyo masalia ya ujima ni nini hiki? Kama ulikuwa unampenda au kumheshimu mtu akiwa hai kwanini usioneshe upendo na heshima yake na kumhifadhi saa yake ilipofika? Sitaki KABISA mtu anitumia picha ya mtu yeyote ambaye hajahifadhiwa kwa ajili tu ya kufurahisha macho!!

Hivi taarifa za kusema mtu kauawa au kapata ajali hazitoshi hadi uthibitishe kauawa vipi na kuwaambia wengine? Kinachonishangaza zaidi siku hizi ni kuwa baadhi ya picha zinatoka mochwari au mahospitalini kwenyewe!! Yaani, hata weledi wa kazi hakuna tena? Unaruhusu vipi watu kuingia na simu zenye picha mochwari?

JAMANI UTU WA MTU NI UTU WA WATU WOTE! Hata kama humpendi mtu heshimu na linda utu wake!! Kwani SOTE NI BINADAMU.
 
Nakubaliana mkuu ,lie picha ya mwana CHADEMA aliyeuwawa Arusha haikupaswa kubandikwa hadharani.
Aliyepiga picha amepungukiwa na ustaarabu kufikia Hali ya kumdhalilisha marehemu.
 
Nakubaliana mkuu ,lie picha ya mwana CHADEMA aliyeuwawa Arusha haikupaswa kubandikwa hadharani.
Aliyepiga picha amepungukiwa na ustaarabu kufikia Hali ya kumdhalilisha marehemu.

Siyo ya huyo tu; tumeliona kwenye Kanumba, tumeona wale vijaan wanne, tumeona ajali ya Mbatia na Regia, tumeona ni kama voyeurism ya aina fulani hivi!!!
 
Naunga mkono hoja.Maiti haitoi ridhaa.

nimeangalia leo ajali ya Bronx huko NY ambapo watu saba wamekufa papo hapo baada ya gari lao kuanguka kutoka 'barabara za juu kwa juu'. Hakuna mtu aliyepiga picha za maiti kuonesha na hata gari lenyewe lilipoondolewa pale kwa ajili ya uchunguzi lilikuwa limefunikwa turubai!
 
Hili suala lilisha zungumziwa humu na mkuu Nyani Ngabu.
Kweli ni kukosa utu kuonesha picha za maiti asie hifadhiwa
Binafsi naona hata picha za wagonjwa wasio jitambua ni same.
Pia kuna tabia ya wapiga picha kurecodi/capture vipigo vikali

Kama vile mwizi kanaswa badala ya kumpeleka polisi anachapwa
waandishi wa habari wakifika eneo la tukio wanakaa kupiga picha
hata hawakumbuki kua wanaweza kumsaidia huyo anae kula kipigo
Inasikitisha sana jamani, tubaditi tabia. na tusipromote hizo picha.
 
Last edited by a moderator:
Hili nimeshalisema sana hususan kwenye thread za Crashwise na kuambulia matusi

Ustaarabu hatuna wala haihusiani na misitu wala majangwa
 
Last edited by a moderator:
Jf na sisi tumezidi bwana! Haturiziki na maneno ya waleta taarifa mara utaona source mkuu! Mara tupia tupia na vipicha mkuu! Kwa kweli tunachemka, hebu tujirekebishe bwana! Nilistuka sana jana nilipoona zile picha za m/kiti wa CDM. Hivi unapata wapi ujasiri wa kupiga picha maiti ya mwenzio? Nyamb..ff!
 
Utandawazi umeusahau? na unafikiri karibu 90% ya simu zinauzwa zikiwa na camera ni kwa nini? wacha watu wadadavue. Wacha kuwajaza watu ujinga.

"A picture is worth a thousand words"

Hili nimeshalisema sana hususan kwenye thread za Crashwise na kuambulia matusi

Ustaarabu hatuna wala haihusiani na misitu wala majangwa
Bora mseme nyinyi viazi... mimi mhogo huwa naambiwa nina mizizi. Nilitukanwa sana, nilishambuliwa sana na nilipuuzwa sana wakati nilipolaani kwa nguvu zote member mmoja anayeitwa Crashwise alipotundika picha za wale vijana waliouawa Arusha juzi juzi. Na kuonyesha jeuri yake jana ameweka tena za mwenyeketi wa Chadema aliyechinjwa. Mimi nadhani uongozi wa JF una wajibu wa kukomesha huu ushenzi uliovuka mipaka. Picha za marehemu siku hizi zimegeuka burudani ya macho. Ni unyama uliopindukia.
 
Alieye onyesha jeuri ni wewe na group lako mnaoendela kuwauwa...
 
Siyo ya huyo tu; tumeliona kwenye Kanumba, tumeona wale vijaan wanne, tumeona ajali ya Mbatia na Regia, tumeona ni kama voyeurism ya aina fulani hivi!!!
Mimi ninaamini wewe MMJJ una mchango mkubwa sana JF kwanini msiweke sheria ya kuzui kuweka picha za marehemu tukajua moja kuwa hairuhusiwi.
 
Niliiona hiyo title wala sikuifungua zaidi ya kushangaa hivi inakuwaje mtu kutuma kitu kama hicho. Tuwaze tu kidogo kama ingekuwa ni ndugu yako ungekubali mwili wake udhalilike namna hiyo. Tustaarabike jamani.
 
Ni kweli kabisa ustaarabu huo siyo, na hii inatokana na watu kushindwa kuwa wastaarabu ktk mambo madogomadogo, mfano, wakati wa kupanda daladala jioni, watu badala ya kujipanga foleni, wanagombania kuingia bila kujali watoto, walemavu au wazee. Au bank mwisho wa mwezi watu wengine wanakuta foleni halafu wanataka kupita mbele. Au mtu anakopa pesa, kulipa mpaka mgombane. Ustaarabu tatizo la Taifa.
 
nimeangalia leo ajali ya Bronx huko NY ambapo watu saba wamekufa papo hapo baada ya gari lao kuanguka kutoka 'barabara za juu kwa juu'. Hakuna mtu aliyepiga picha za maiti kuonesha na hata gari lenyewe lilipoondolewa pale kwa ajili ya uchunguzi lilikuwa limefunikwa turubai!

Mkuu naomba kutofautiana nawe kidoogo. Kama tunataka kudhibiti hii tabia ya 'kimsitumsitu' na Ujima basi tufanye hivyo kama waafrika kwa taratibu zetu lakini sio kwa kuchukulia mfano Wamarekani maana wao katika hili la kutoheshimu maiti za watu wengine wao ndio bogus kabisa.
Wanaweza kabisa kulinda maadili pale maiti zinapokuwa ni za raia wao laki ni ziro kabisa pale linapokuja suala la maiti za raia wa nchi nyingine.
Tukumbuke kuwa tuliweza kuonyeshwa Sadam Hussein akinyongwa.
Tulionyeshwa picha za maiti za wanawe wa kiume Uday na mdogo wake zilizokuwa zimecharangwa kwa risasi.
Tulionyeshwa Yaliyompata Gaddaf wa Libya.
Miaka kama minne ama mitano iliyopita kuna shambulio la bomu lilitokea kwenye hotel mmoja yakitalii mjini Mombasa Kenya na tukaonyeshwa maiti za wafanyakazi wabantu zikiwa kwenye mabaki ya mjengo uliobomolewa.

Ninachotaka kusema ni kuwa kama tunakubaliana kuhifadhi na kuheshimu maiti za binadamu YOYOTE tuamue kufanya hivyo kwa Imani na Ustaarabu wetu wa Kiafrika lakini sio kujilinganisha na Marekani ambao kwao heshima kwa maiti ni pale inapokuwa ni ya raia wao lakini za wengine? Mmmmmmmm....!

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom