Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Ninaamini baadhi yetu bado tuna masalia ya tabia za kimsituni situni hivi! Kuna faida gani ya kukimbia kupiga picha marehemu ambaye hajahifadhiwa vizuri? Ni ubinadamu gani huu tulionao kwamba badala ya kumhifadhi mwenzetu na heshima ya utu wake tunachukua camera zetu na kumpiga picha kuutangazia ulimwengu? Kama siyo masalia ya ujima ni nini hiki? Kama ulikuwa unampenda au kumheshimu mtu akiwa hai kwanini usioneshe upendo na heshima yake na kumhifadhi saa yake ilipofika? Sitaki KABISA mtu anitumia picha ya mtu yeyote ambaye hajahifadhiwa kwa ajili tu ya kufurahisha macho!!
Hivi taarifa za kusema mtu kauawa au kapata ajali hazitoshi hadi uthibitishe kauawa vipi na kuwaambia wengine? Kinachonishangaza zaidi siku hizi ni kuwa baadhi ya picha zinatoka mochwari au mahospitalini kwenyewe!! Yaani, hata weledi wa kazi hakuna tena? Unaruhusu vipi watu kuingia na simu zenye picha mochwari?
JAMANI UTU WA MTU NI UTU WA WATU WOTE! Hata kama humpendi mtu heshimu na linda utu wake!! Kwani SOTE NI BINADAMU.