Badala kuilaumu serikali, tuilaumu bodi ya sukari

Prosper C Manasse

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
635
690
*Moja Kati Vitu Ambavyo Serikali Inatakiwa Ifanye Ni Kusikiliza Wananchi Wake Ikiwemo Sekta Binafsi.

*Viwanda Vya Sukari Vililalamika Kwamba Vinashindwa Kufanya Biashara Kwa Kuwa Sukari Nyingi Inaingizwa Kutoka Nje. Hii Inamaanisha Kwamba Sukari Ya Tanzania Inatosheleza Kabisa Na Hatuwezi Kuwa Na Mapungufu.

*Hata Hivyo Tanzania Tunaviwanda Vi4 Vya Sukari Ambavyo Ni,
1. TPC MOSHI.
2. KAGERA SUGAR.
3. KILOMBERO SUGAR (Moro)
4. MTIBWA SUGAR (Moro)

Zanzibar Nilisikia Kinajengwa Miaka Fulani Lakn Sina Uhakika Kama Kipo Au Lah.

*Serikari Ilifanya Vyema Sana Kusikiliza Bodi Ya Sukari Ambayo Ndiyo Inayoratibu Uzalishaji Wa Sukari.

*Tatzo Si Kwamba Sukari Hakuna Nchini, Ukweli Ni Kwamba, Mdudu Aliingia Baada Ya Serikali Kutoa Bei Elekezi. Whole Salers Waliona Kama Wanaonewa Maana Wao Walinunu Sukari Kwa Bie Ya Awali Na Kabla Stock Haijakata, Serikali Inatoa Bei Elekezi Ukizingatia Kuna Gharama Walizotumia Kwa Bei Ya Awali Na Si Hii Ya Sasa.

MASWALI YA KUJIULIZA.
1. Serikali Inawezaje Kuzuia Sukari Isiingie Nchini Bila Takwimu Za Bodi Ya Sukari Ambayo Ndiyo Inaratibu Uzalishaji?!.

2. Serikali Inawezaje Kupanga Bei Ya Sukari Bila Kuishirikisha Bodi Ya Sukari?!.

3. Je, Bodi Ya Sukari Ilitoa Takwimu Sahihi Au Ilikubaliana Na Serikali Kwa Nidhamu Ya Woga?!.

4. Je, Bodi Ya Sukari Iliongea Na WholeSalers Au Ilifanya Maamuzi Bila Kuwashirikisha?!.

5. Kama Bodi Ya Sukari Iliongea Na Wholesalers, Kwanin Isiwape Muda Wamalize Sukari Walonunua Kwa Bei Ya Juu?!.

6. Je, Bodi Ya Sukari Ili Ilizingatia Msimu (Low&High Season Of Production) Kwa Viwanda Vya Sukari Tanzania?!.

Wakulaumiwa Sio Serikali Bali Ni Bodi Ya Sukari Ambayo Nina Hakika Haikuwa Wazi Kwa Serikali Maana Kama Ingekuwa Wazi, Serikali Ingetoa Muda Ili Kuruhusu Stock Za Wholesalers Ziishe Kisha Itoe Bei Elekezi.

USHAURI.
Serikali Kama Haitumii Hii Njia Basi Ni Vyema Ikaanza Kuitumia Baada Ya Viwanda Kuanza Uzalishaji Maana Kipindi Cha Masika Viwanda Vyetu Husimama Kwa Miezi Mi3 Hadi Mi4 Ili Kupisha Miwa Ikuwe Pamoja Na Kufanya Matengenezo Makubwa Ya Kiwanda.

ORODHA YA VIWANDA NA USAMBAZAJI MIKOANI.

TPC MOSHI (KILIMANJARO)
1. Kilimanjaro.
2. Tanga.
3. Arusha.
4. Manyala.
5. Singida.
6. Shinyanga.
7. Tabora.

KAGERA SUGAR (KAGERA)
1. Kagera.
2. Geita.
3. Mwanza.
4. Mara.
5. Simiyu.
6. Kigoma

MTIBWA SUGAR & KILOMBERO SUGAR (MOROGORO)
1. Morogoro.
2. Dodoma.
3. Iringa.
4. Mbeya.
5. Njombe.
6. Songwe.
7. Ruvuma.
8. Rukwa.
9. Katavi.
10. Lindi.
11. Mtwara.

Mgawo Wa Mipaka Kama Hiyo, Itaisaidia Serikali Kwa wakati Ujao Kujua Wapi Kiasi Gani Kimepungua Na Nini Changamoto Za Kanda Hii Au Ile Ktk Uzalishaji.

*Tusiishie Kuilaumu Serikali Na Badala Yake Tuisaidie Kimawazo Maana Taifa Ni Letu Sote Na Kama Sisi Hatutalijenga Kwa Ushirikiano Na Badala Yake Kupigana Vijembe, Basi Tutaendelea Kurithishana Umasikini Kizazi Hata Kizazi.

MTAZAMO WANGU TU.
 
Mimi binafsi siamini kama Magufuli anajali kuna bodi ya sukari na majukumu yake ndo hayo.....
na kama kuzuia sukari kuagiza nje lilikuwa wazo la bodi ya sukari au any wataalam...
inaonekana ni kama Magufuli aliamua yeye binafsi kwa 'busara' zake..

na sasa tumefika hapa...
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari aliwahi kukiri ugumu wa hii biashara na changamoto zake ni kama biashara ya Unga/Sembe.
 
Naomba nikusahihishe mtoa mada kuwa tuna viwanda vitano (5) vya sukari hapa nchini.
Ipo Kilombero I na Kilombero II, na vyote ni vikubwa, pamoja na vingine ulivyovitaja.
 
Naomba nikusahihishe mtoa mada kuwa tuna viwanda vitano (5) vya sukari hapa nchini.
Ipo Kilombero I na Kilombero II, na vyote ni vikubwa, pamoja na vingine ulivyovitaja.
Kilombero1 Na 2 Ni Ilikuwa Kampuni Moja Tangu Miaka Ya Nyuma, Sijui Kwasasa Kama Vimetengana.
Nashukuru Kwa Mchango Wako.
 
Mimi binafsi siamini kama Magufuli anajali kuna bodi ya sukari na majukumu yake ndo hayo.....
na kama kuzuia sukari kuagiza nje lilikuwa wazo la bodi ya sukari au any wataalam...
inaonekana ni kama Magufuli aliamua yeye binafsi kwa 'busara' zake..

na sasa tumefika hapa...
Hakuamua JPM Iliamua Serikali Kwa Data Za Bodi Ya Sukari.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari aliwahi kukiri ugumu wa hii biashara na changamoto zake ni kama biashara ya Unga/Sembe.
Last Time Anaongea Alisema Kwmb, Sukari Ipo Na Inatosha Kwa Matumizi Ya Tz.
Ushahidi Umeonekana Baada Ya Waloificha Kukutwanayo, So Serikali Ilikuwa Sahihi Na Bodi Ya Sukari Pia Ilikuwa Sahihi.
 
Rais alijiridhisha kabla ya kutoa tamko?Ana tofauti gani na Anne Kilango? Hakwepi Lawama
Sasa Mkuu Wewe Unafikiri Serikali Inawezaje Kijiridhisha Nje Ya Bodi Ya Sukari?.
Huwezi Kununua Sukari Nyingi Bila Kupata Kibali Kwa Bodi Ya Sukari Na Wao Ndio Huratibu Kila Kitu.
 
Mimi binafsi siamini kama Magufuli anajali kuna bodi ya sukari na majukumu yake ndo hayo.....
na kama kuzuia sukari kuagiza nje lilikuwa wazo la bodi ya sukari au any wataalam...
inaonekana ni kama Magufuli aliamua yeye binafsi kwa 'busara' zake..

na sasa tumefika hapa...

bodo ya sukari ni agency ya serikali na ina report either directly au indirect kwa raisi. Kwa hivyo wanawajibika kusikiliza na kutekeleza maelekezo yake
 
Sukari yote iliyo fichwa haifiki tani laki moja
mahitaji ni tani laki 6
uzalishaji wa ndani ni tani laki tatu
Mkuu Si Kweli, Uzalishaji Wa Viwanda Vyote Tz Uwe Tani Laki3 Kwa Kipindi Cha Miezi 10?.

Ok Hata Nikiamini Usemalo, So Serikali Ilipata Hizo Data Wapi Mkuu Ebu Niweke Wazi.
 
Sukari yote iliyo fichwa haifiki tani laki moja
mahitaji ni tani laki 6
uzalishaji wa ndani ni tani laki tatu

Weka kwa muda basi manake unaweza sema tani laki6 kwa mwaka. Tatizo la nyie wachambuzi wa kibongo Ni to run multivariable model mmezoea x and y zikiongezeka mbili Mbele mnaingia Chaka Na kuja Na vitu vya ajabu
 
Weka kwa muda basi manake unaweza sema tani laki6 kwa mwaka. Tatizo la nyie wachambuzi wa kibongo Ni to run multivariable model mmezoea x and y zingiongezeka mbili Mbele mnaingia Chaka Na kuja Na vitu vya ajabu

kwa mwaka
 
mkuu nadhani hata hiyo bodi ya sukari inahitaji kufumuliwa na kuundwa upya...bodi inaongozwa na miCCM ambayo siku zote inawaza kuitafuna nchi unadhani kutakuwa na mabadiliko yoyote katika usimamiaji wa biashara ya sukari? la hasha! inawezekana hiyo mijitu imekula njama na viwanda vya sukari ili kuzidi kuwaumiza wananchi kwa maslahi ya matumbo yao makubwa kama matenga ya ndizi.
 
Weka kwa muda basi manake unaweza sema tani laki6 kwa mwaka. Tatizo la nyie wachambuzi wa kibongo Ni to run multivariable model mmezoea x and y zingiongezeka mbili Mbele mnaingia Chaka Na kuja Na vitu vya ajabu
Umenena Vyema Mkuu Nafikiri Aweke Muda Ili Tujadili.
 
Naomba nikusahihishe mtoa mada kuwa tuna viwanda vitano (5) vya sukari hapa nchini.
Ipo Kilombero I na Kilombero II, na vyote ni vikubwa, pamoja na vingine ulivyovitaja.
Hivyo viwanda vya Kilombero huhesabiwa ni kimoja kimantiki kwamba
1. Mmiliki mmoja
2. Wanavuna mashamba hayo hayo yaani miwa ya k1huweza kwenda K2
3. Lengo ni moja
4. Wafanyakazi huweza kufanya kokote na zipo idara nyingine ambazo hazigawanyiki nk
 
Back
Top Bottom