Bachelor sugu naomba ushauri wenu wakuu

bachelor sugu

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,689
3,641
Habari za jioni wapendwa wote.

Sawa na kichwa cha Uzi hapo juu,naombeni mchangi wenu wa mawazo katika hili.

Mimi ni mtoto wa 2 kuzaliwa katika tumbo la mama yangu nikitanguliwa na dada yangu na pia nina wadogo 3 wa kiume wa 2 na kitinda mimba wetu ni wa kike.

Nimeelemewa na ujeuri na dharau za wadogo zangu hawa wawili wa kiume hali inayonifanya nihisi kuchoka na kuhitaji kuchukua hatua ili tu niwadhihirishie kuwa mm ni kaka yao na ni mkubwa kwao.

Licha ya kuwa mm ndiye niliyewasimamia na kuwasaidia katika masomo na miongozo yote maana wazazi nguvu ziliwaishia mapema hivyo kuanzia level ya sekondari nilichukua usukani na kuwasimamia hawa madogo na niliweka nadhiri ya kuhakikisha wanapata pa kushika ilimradi kila mmoja aweze kupata namna ya kujipatia mkate wake wa kila siku.
Nashukuru Mungu kuwa mmoja alishaajiriwa serikalini tangu 2014 na huyu mmoja anaingia mwaka wa NNE hapo UDSM katika kozi flani ya mambo ya Sayansi
Jana katika conversation moja na huyu wa UDSM tukiwa tunabishana kuhusu namna ya kumuendeleza huyu kitinda mimba wetu ambaye amemaliza form four mwaka Jana na kupata matokeo mabaya huyu dogo kutokana na kujua kwake akampa amri huyu binti kuwa anatakiwa kusema Veta-Laboratory technology hivyo nililazimika kumuhoji kama kuna channel ameipata ambayo atampachika huyo binti pindi atakapomaliza hiyo kozi lakini hakuweza kunipa maelezo yaliyonyooka hali iliyopelekea mm kukataa huyu mtoto kusema hiyo kozi nikitoa altenative kuwa afunguliwe mradi ili ajiajiri.

Kiukweli mdogo wangu huyu msomi alijibu jeuri kubwa kuwa DOGO ATASOMA KOZI HIYO VYOVYOTE ITAKAVYOKUWA na kwa kuwa mie ndiye maamuzi nilimwambia hicho kitu hakitakuwepo na mlengwa mwenyewe hawezi ends kinyume na mm sababu anajua ni gharama zangu kiasi gani nimepoteza kwa ajili yake.
Kila nikiyarejea mazungumzo ya SMS tuliyoyafanya Jana kiukweli napata na hasira sana maana huyu dogo imekuwa ndio tabia yake kwa muda mrefu sasa hivyo naombeni ushauri ndugu zangu nimfanyeje ili aweze kutambua kuwa mm ni mkubwa kwake na adabu ichukue mkono wake?

Sincerely,Bachelor Sugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwanini mnalizimisha mty kusoma mnachotaka wewe na mdogo wako wa chuo?

lipa karo, shauri pale unapoona wanaelekea pabaya....hayo ni maisha yake...mpe uhuru wote wa kuamua anavyotaka kuwa.
 
Sasa kwanini mnalizimisha mty kusoma mnachotaka wewe na mdogo wako wa chuo?

lipa karo, shauri pale unapoona wanaelekea pabaya....hayo ni maisha yake...mpe uhuru wote wa kuamua anavyotaka kuwa.
Mkuu huyu mtoto anayetakiwa kusomeshwa sio kuwa ndo kachagua hiyo kozi bali huyu msomi wetu wa UD ndo analeta falsafa hizo kuwa akasome hiyo kozi na mm kwa mtazamo wangu wa mbali sioni future yake kwa huyu mtoto hasa kulingana na hiyo level na pia soko la ajira kwa nyakati hizi ndo maana nimelikataa.

Ndiyo maana nikauliza mbona wewe na msomi mwenzako mnakuwa vifront front kumchagulia na kugombana kwasababu ya future ya mtu.

Mpeni uhuru yeye aamue anataka nini kisha muanze kumshauri akikataa basi. Au naye ndiyo wale wasiojua hata wanataka kusoma nini?
 
Ukiwa na dogo kama huyo hakuna namna zaidi ya kugawana majina ya ukoo na la baba either achukue la ukoo na mimi nichukue la baba ... Basii. ..

a e i o u
 
bachelor sugu mimi najua mwenye hela ndo ana sauti kwa familia zetu nyingi za kibongobongo na ndo anayesikilizwa wewe unakosea wapi?
MWENYE MAAMUZI NINI ASOME AU AFANYE NI HUYO FORM FOUR FAILURE.
Msikilizeni acheni malumbano
 
Atakuwa la saba mwenzangu... sasa dogo wa chuo anaona huyu kaka kama alifeli la saba ya chuo atatoa ushauri gani?
 
Ndiyo maana nikauliza mbona wewe na msomi mwenzako mnakuwa vifront front kumchagulia na kugombana kwasababu ya future ya mtu.

Mpeni uhuru yeye aamue anataka nini kisha muanze kumshauri akikataa basi. Au naye ndiyo wale wasiojua hata wanataka kusoma nini?
Mkuu kiufupi huyu mtoto kichwa ni kizito na ndo wale wanaohitaji mwongozo kwa kila kitu.Nimecheza kamari kwa miaka 4 na kupoteza not less than 9m kwa miaka yote hiyo coz nilimsomesha private ila kwa sasa naona bora tu nimuanzishie mradi hata afuge KUKU tu maana hata mie nguvu zinaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bachelor sugu mimi najua mwenye hela ndo ana sauti kwa familia zetu nyingi za kibongobongo na ndo anayesikilizwa wewe unakosea wapi?
MWENYE MAAMUZI NINI ASOME AU AFANYE NI HUYO FORM FOUR FAILURE.
Msikilizeni acheni malumbano
Kumbe haka ka upepo kapo sehem nyingi.Money is power.
Kwa upande wako bachelor Sugu.Dogo kama ana dharau cha msingi ni kutomshirikisha mambo za muhimu cause wewe ndio unatoa support.Remove him from the equation akianza toa povu u can tell him kuwa he is arrogant and disrespectful kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakuwa la saba mwenzangu... sasa dogo wa chuo anaona huyu kaka kama alifeli la saba ya chuo atatoa ushauri gani?
Hahahahaha hapana mkuu namshukuru Mungu kwa hiki kielimu kidogo nilichonacho na ndicho kimeniwezesha kuwafikisha hawa madogo hapa walipofika.

Haina maana kuwa huyu dogo ndio mwenye decision nop mi ndo wa mwisho katika maamuzi na nimeshaamua kuwa DOGO atajiajiri no one can add a word.
Ushauri niliouomba ni kuhusu nimfanye nn huyu dogo ili ajue mm ni kaka yake,?Ninafikiria kuwa natakiwa Kumtandika japo one day ili adabu irudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe haka ka upepo kapo sehem nyingi.Money is power.
Kwa upande wako bachelor Sugu.Dogo kama ana dharau cha msingi ni kutomshirikisha mambo za muhimu cause wewe ndio unatoa support.Remove him from the equation akianza toa povu u can tell him kuwa he is arrogant and disrespectful kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks mkuu I've got your point.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bachelor sugu mimi najua mwenye hela ndo ana sauti kwa familia zetu nyingi za kibongobongo na ndo anayesikilizwa wewe unakosea wapi?
MWENYE MAAMUZI NINI ASOME AU AFANYE NI HUYO FORM FOUR FAILURE.
Msikilizeni acheni malumbano
Of course wanasema heshima pesa shikamoo kelele tu but intention yangu nadhani ninastahili kufanya kitu kwa huyu dogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaha hapana mkuu namshukuru Mungu kwa hiki kielimu kidogo nilichonacho na ndicho kimeniwezesha kuwafikisha hawa madogo hapa walipofika.

Haina maana kuwa huyu dogo ndio mwenye decision nop mi ndo wa mwisho katika maamuzi na nimeshaamua kuwa DOGO atajiajiri no one can add a word.
Ushauri niliouomba ni kuhusu nimfanye nn huyu dogo ili ajue mm ni kaka yake,?Ninafikiria kuwa natakiwa Kumtandika japo one day ili adabu irudi

Sent using Jamii Forums mobile app

Usimfanye kitu bhana...mdogo wako huyo kutofautiana kupo msamehe tu.

Mzee baba ulitakiwa uwe mkali toka zamani. Mimi wadogo zangu walikuwa wananiogopa zaidi ya baba yao hasa wa kike. Na nadhani hadi sasa wananiogopa.
 
hakuna haja ya kuumiza kichwa
huyo binti anatakiwa achague aidha akusikilize wewe au huyo dogo wa ud....

inginiaringi ya udaktari mueshimiwa
 
Usimfanye kitu bhana...mdogo wako huyo kutofautiana kupo msamehe tu.

Mzee baba ulitakiwa uwe mkali toka zamani. Mimi wadogo zangu walikuwa wananiogopa zaidi ya baba yao hasa wa kike. Na nadhani hadi sasa wananiogopa.
Mkuu huyu dogo ana ka nature ka ujeuri coz hata huyu mkubwa wake wanaefuatana alikuwa akimdharau na kumnyanyasa sana mpaka siku bimkubwa alikereka akawaweka ulingoni akawaambia nataka mpigane mbele yangu atakayetoa machozi namuongezea fimbo basi mpambano ukaanza aisee kalinyukwa na kaka yake kakaanza kulia na bimkubwa akatimiza ahadi akakaongezea fimbo na kukapa warning kaache utovu wake wa nidham.Sasa huyo yy kidogo kanamuogopaogopa ila mi mkubwa zaidi kananizingua ndo maana nahisi upole wangu utanigharimu kwa huyu dogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom