Inasikitisha sana. Kwenye haya maisha tuishiyo, busara inatuelekeza kumuheshimu mwingine katka namna zote. Achilia mbali heshima ya mdogo kwa mkubwa and vice versa. Heshima ya ndani ya familia misingi na mipaka yake inajulikana. Inapotokea mmoja anakwenda. Kinyume na misingi hiyo, moja ya matokeo ni kama hali unayopitia
bachelor sugu. Pole sana. Napata hisia kwamba hali hiyo umeilea mwenyewe hatimaye mdogo wake imekuwa ni jadi yake kubishana na ww kwa njia zisizongatia misingi ya nidhamu, utii na adabu. Hata kama alikuwa na mawazo mbadala kwny jambo mnalobishania, bado angaliweza kutumia maneno yenye Hekma, busara na utii ktk kuwasilisha mawazo yake.
Binafsi nashindwa nikushauri ufanye nini kwa kuwa wewe ndiye mwenye nafasi zaidi ya kuchukua maamuzi na hatua ili kuirejesha nidhamu ya mdogo wako kwny misingi yake. Pole sna
Sent using
Jamii Forums mobile app