Bittah
Senior Member
- Jul 14, 2018
- 135
- 37
- Thread starter
- #21
Bro asante kwa ushauri wako ngj nikuchek pm kabisaMtu yoyote mi kwa sasa akiniuliza kozi ipi akasome basi IT, Computer Science, software engineering etc hizo ndizo naweza nikakushauri.
Kwa nn? Hizi ni kozi ambazo skills zako ndio mtaji wako kiasi cha kwamba unaweza ukajiajili huku ukiwa umejifungia ndani.
Kivipi? Ulimwengu wa sasa huu wa internet mtu mwenye skills za IT ana uwanda mpana wa kufanya projects za watu kutoka sehemu tofauti kwa mfano web kama freelancer, upwork na fivver kuna projects watu wanapost wakitafuta wataalamu wa kuzifanyia kazi lkn kikubwa "SKILLS".
Hapo sijarejea namna ya kutumia skills zako kwenye youtube, teachable, blogs
Unapoenda huko kama unataka kuwa competent usisome kwa ajili GPA soma ili uwendane na market trends ya tech kwa mfano ukienda huko hutofindishwa jinsi ya kuunda android apps, iphone apps lkn ww mwenyewe unaona matumizi ya smartphones jinsi yalivyo na apps zinaweza kukupatia pesa, hutofundishwa framework za e-commerce kama woocormerce lkn leo manunuzi ya mtandaoni yanaongezeka, hutofundishwa kuhusu SEO (search engine optimization) lkn google.com ndio mtandao unaongoza kwa kutembelewa TZ. Ukiwa chuo utafundishwa html,css,mysql na javascript vitu ambavyo havitoshi kwa sasa.
Kiufupi unatakiwa ujiongeze na uhakikishe kitu unachokisoma unakimaster vizuri kabisa ili uwe na uwezo wa kufanya projects kubwa na nzuri kumbuka huko chuo utachopewa ni basics sana unatakiwa usome vitu vingine vya IT.
Changamoto ambayo issue nyingi za IT Mpaka zianze kukulipa zinachukuwa muda kidogo hivyo nakushauri kipindi utakapokuwa chuo tangu mwaka wa kwanza au wa pili fanya tafiti na utengeneze project ambayo utaendelea nayo hata baada ya kumaliza chuo kwa mfano umemaster vizuri kuhusu graphic designing basi ukamua kuwa unatengeneza animations video na kuziweka youtube huku ukihakikisha baada ya miaka mitatu hiyo channel ya youtube ianze kukutengenezea pesa.
Ngoja niishie hapa kwa leo ila nina mengi.
Sent using Jamii Forums mobile app