Baby Boomers: Kizazi cha watu wabinafsi kuwahi kutokea duniani!

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,197
Katika utafiti wangu usio rasmi, nimegundua hiki kizazi cha hawa Baby Boomers (watu waliozaliwa mwishoni mwa miaka ya 1940 na mwanzoni mwa miaka ya 1960 i.e 1946-1964), ni kizazi cha watu wabinafsi kuwahi kutokea duniani.

Wengi wao, katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania, walipoingia tu kwenye vyombo vya kufanya maamuzi, mambo yakaanza kwenda kombo!

Baby Boomers wengi wamekuta dunia ikiwa na uchumi imara sana, maendeleo na ubunifu/uvumbuzi wa sayansi na Teknolojia vikiwa katika kilele chake.

Wengi mtakumbuka, ni katika kipindi hicho cha miaka ya 50 na 60 ambapo dunia ilikuwa sehemu salama na nzuri ya kuishi. Maisha yalikuwa rahisi hali iliyopelekea watu wengi kuzaa watoto wengi (hawa watoto waliozaliwa kipindi hiki wanaitwa Baby Boomers kwa sababu waliozaliwa wengi sana kipindi hiki).

Lakini kipindi cha Baby Boomers tumeshuhudia maanguko mengi ya uchumi, kuanzia wa dunia hadi wa nchi moja moja ikiwemo Tanzania. Tumeshuhudia mabadiliko ya sera ambazo nyingi zinawekwa kuwakandamiza wanyonge n.k.

Hivyo, nathubutu kusema hiki kizazi, ni kizazi cha hovyo kabisa kuwahi kutokea duniani. Huenda dunia itakuwa salama tena mara baada ya kizazi hiki chote kuondoka kwenye uso wa dunia.
 
Baby Boomers Wamekusikia Mkuu.

TEGEMEA LOLOTE KUANZIA SASA!

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hichi kitu kama kuna mahali nilisoma juu juu tu kwenye maktaba ya chuo nilichokuwa nasoma. Kuna ka ukweli kiasi fulani!
 
Back
Top Bottom