Babu yangu ametimiza Miaka 100, ameshajiandalia vifaa vyake vya mazishi

Inatakiwa ifikie wakati tukubali tu kifo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Hivyo hatutakiwi kukiogopa sana.

Ingawa kusema ukweli kifo kinauma aisee! Halafu kinaogopesha.
Hakika, na naamini wale wanaokikubali kifo pale kinapo wapigia hodi, huwa wanakufa happier. Hawapati maumivu makali kama wale ambao wanakipinga!
 
Babu kajifunza somo
Katika hali ya kustaajabisha,mwaka juzi 2021 nilipoenda kijijini kusalimia wazee nikakuta mwembe dodo mkubwa wa Nyumbani kwa babu haupo tena. Ni nyumba tu ndiyo inaonekana na miti mingine Kama misonobari,ila ule mwembe maarufu ambao tulipokuaa watoto tulipenda kushinda chini yake kusubiri embe haupo tena.

Baada ya kusalimiana nikauliza imekuwaje ule mwembe dodo haupo? Kwa nini mmeukata?

Wote wakakaa kimya kwa muda na kutazamana Kisha wakamwangalia babu ambae alikuwa amekaa kwenye 'kiti Cha uvivu' (kiti fulani kina Kama mtumbwi hivi). Shangazi yangu (mtoto wa pili wa babu) ambaye kwa wakati huo alirudi kijijini kuwalea wazee baada ya yeye kustaafu kazi ya ajira mjini akanijibu "unajua mwanangu babu yako ni mtu wa ajabu Hadi kila mmoja anamshangaa hapa kijijini"

Wakati nimeduwaa kutaka kujua babu amefanya nini akaendelea "huo mti wa mwembe unaouzungumzia yeye ndiye kamuita mtu wa chainsaw aukate Kisha wakamtengenezea mbao vizuri akazihifadhi ndani kwa lengo la kutengeneza jeneza lake. Alitaka atengeneze jeneza kabisa aliweke ndani ila tumemkataza maana huo ni uchuro, kwa hiyo amezichonga mbao zake vizuri na kuziweka chumbani kwake pamoja na sanda aliyoinunua muda mrefu".

Hii taarifa hata Mimi ilinistua na kunishangaza.

Babu amekata mwembe ili kuchonga jeneza!!?

Alafu ana sanda pia huko chumbani!!! Si uchuro huu!!?

Mbona ana watoto na familia ambayo inaweza kumfanyia hayo yote bila shida endapo mauti yatamfika? Why afanye hivi?

Babu bila wasiwasi akiwa amekaa kwenye kiti chake na kikombe chake Cha kahawa kwenye stuli akaniuliza "Satoh umeniletea kahawa yangu?" Huwa nampelekea kahawa nikiendaga kijijini na anaipenda Sana,siyo ile ya kununua ya kwenye makopo,Bali ni kahawa original kutoka hapa nyumbani Tanzania niliyomsagia mwenyewe Kisha nikapark kwenye kifungashio kizuri nikaenda nayo kijijini. Inanukia vibaya mno!!

Nikamjibu,"yeah babu kahawa Nimekuja nayo,ila hii stori ya shangazi ina ukweli?".

Babu siyo mtu wa papara kwenye kuongea.

Akaniambia kaa kwenye kiti kijana mdogo,Kisha akaendelea...

"unajua sisi watu weusi tumaogopa Sana kifo eeh? Nilipokuwa nafanya kazi Israel nilijifunza vitu vingi Sana,na mojawapo ni wayahudi hawaogopi kifo.

Yes,

wenzetu wayahudi(waisrael) hawaogopi kifo tofauti na sisi waafrika ambao tunatishana kila siku kuhusu kifo. Si tunasoma kwenye Biblia Yesu alizikwa kwenye kaburi la mzee yusuph wa Alimataya? (Akamikumbusha mstari wa bibilia kuhusu habari ya mazishi ya Yesu). Maana yake wenzetu tangu mwanzo wanajiandaa na kifo maana kifo ni wajibu na haki..hawaogopi kufa Kama sisi".

"Leo 2021 nimebakiza Miaka miwili tu ili niweze kufikisha Miaka Mia,hiyo Ni baraka kubwa sana kutoka kwa Mungu. Endapo Mungu atanitwa kabla ya kufikisha Miaka Mia itakuwa heri lakini endapo nitafikisha Miaka Mia moja itakuwa ni Jambo la heri zaidi,na hakika nitafanya sherehe kubwa ya shukrani kwa kufikisha Miaka 100".

Babu akaendelea;

"Hivyo vitu nilivyoweka ndani kwenu nyinyi mmelichukulia katika mtazamo wa mkosi na nuksi Ila kwangu Mimi ni ishara ya shukrani kwa Mungu na kujiweka tayari kumpokea rafiki huyu asiye mnafiki Wala konakona aitwaye kifo. Kifo kinakuwa kibaya kwa wale watendao mabaya na wasio shukrani,ila kwangu Mimi kifo ni rafiki. Mnaogopa kufa kwa sababu mmejaza visasi,chili,eoho mbaya,unafiki,uzinzi,ulevi na uchafu mwingi sana kwenye nafsi zenu". Akacheka.

"Mjukuu wangu,unaishi mjini. Jitahidi kadili uwezavyo kuwatendea watu vile ipasavyo. katika kipimo kile ambacho wewe ungetamani upimiwe,wapimie hiko wengine. Usiumize watu. Mimi nimeishi mjini miaka mingi kuliko nyinyi nyote hapa. Mjini Kuna vingi na mengi ya hovyo,jaribu kuwa mtu bora na uliyejawa Moyo wa upendo na shukrani. Jitahidi kufanya kazi na kutafuta vya halali na jitahidi kula mlo wenye manufaa kwa mwili,pia ufanye mazoezi usiwe mzembe.Si unaniona Mimi naonekana kijana Kama wewe?" Sote tukacheka Kisha akaendelea, "Kubwa kuliko yote ni kumkumbuka Mungu wako kwa kusali na kuomba,ukiyafata haya utakuwa mtu bora sana".

Babu Anaishi na familia yenye watu Kama 8 hivi.

Bibi siku zake zilikoma mwaka 2018.

Alifariki akiwa na Miaka takriban 90.

Miezi Kama miwili nyuma babu ametimiza Miaka 100.

Kama alivyoniahidi mwaka juzi,siku aliyotimiza Miaka 100 alifanya sherehe. Ilifanyika ibada nyumbani,waumini wengi walihudhuria na padre akaendesha ibada hapo.

lakini Babu hawezi tena kwenda kanisani. Hana nguvu,anasali nyumbani. Na Kuna siku waumini huwa wanaenda kumsalimia wakitoka kanisani.

Mara nyingi hutumia muda wake kushinda kwenye kaburi la Bibi lililojengwa kwa naksi kando ya nyumba na Mara kadhaa hufanya ibada hapo.

Ni miezi michache iliyopita nilienda kumtembelea tena kijijini. Kipindi hiko ilikuwa zimebaki siku chache Kama 21 atimize Miaka 100.

Aliniwekea mikono kichwani ishara ya kunibariki.

Niliinamisha kichwa Kisha akaniwekea mikono na kusema maneno haya " Mjukuu wangu zimebaki siku chache kabla sijafikisha Karne moja ,Nina uhakika Mungu hawezi kunichukua kabla sijafika ile siku yangu ya kwanza,siku niliyozaliwa. Nakuachia baraka zangu,na Sasa nipo tayari kwenda zangu (kufa) kwa amani".

Babu amebaki peke yake kwenye nyumba mabayo enzi hizo ilikuwa na pilikapilika nyingi,Bibi hayupo tena. Ni Nyumba yenye historia kubwa maana wengi walizaliwa humo. Nyumba ambayo ina vifaa vya jeneza na sanda kwa ajili ya maandalizi ya mazishi ya Babu!!

Nyumba ambayo waziri wa mambo ya nje mstaafu hayati BERNARD KAMILIUS MEMBE alikuwa akipata nafasi haachi kuja hapo kupata baraka na mawaidha kutoka kwa babu yangu. Babu alizoea kumuita MEMBE kijana wake.

Nakumbua mwezi uliopita lilipotokea kifo Cha mh Membe kwenye wasifu wa marehemu nikaona alisoma Namupa seminary,nikakumbuka ile siku nimechaguliwa kwenda kufanya mtihani wa hiyo shule na nikafaulu Kisha kuchaguliwa kwenda kusoma kwenye hiyo shule ya kikatoriki iliyokuwa na heshima kubwa,lakini mzee(baba yangu mzazi) ambaye pia nae ni msomi zao la shule hiyo aliposikia mwanae nimechaguliwa kwenda kusoma Namupa seminary akakataa katakata hataki niende kusoma hapo.

Time is fleeting!!

Babu,Amenifundisha Somo kubwa juu ya mtazamo wa kuhusu kifo na maisha,somo kuhusu kuwatendea watu yaliyo mema bila kujali huyu ni nani,bila kubagua mkubwa Wala mdogo,masikini Wala tajiri.

Heri yako kwa kutimiza umri wa Miaka Mia moja (Karne moja) BABU YANGU!!

Satoh Hirosh.

Nimejifunza, ana point, hata akichimba kaburi lake ni sawa, ila kwa nini uo muembe? Hapo pana siri, kuna mizimu.
 
Ukijua kwanini Yesu alimfufua Lazaro,

ukajua kwanini akamfufua mtoto wa kiume na wa pekee wa yule mjane alipokua njiani kwenda kuzikwa,

Na kwanini alimfufua yule binti wa Yairo

Utaelewa kwenye kifo na mazishi kuna mambo mengi sana ya kishetwani

Hivi unajua shetani alivyohangaika kuutafuta mwili wa Nabii Musa?

Misiba tunaichukulia powa na matokeo yake ni mabaya sana kwetu tunaobaki
Ewe mtume mama D Naomba hicho kisa cha shetani alivyohangaika kuutafuta mwili wa Musa! No wonder ndio maana Mungu alificha kaburi la Nabii Musa lisionekane abadani
 
Kuna muda inabidi ujichongee tu jeneza lako,ukiwa hai hakuna anayekutazama ukifa wachongewa jeneza la Malaki.Unafki tu.Hata ivo hayupo wa kuishi daima
Unaweza ukaandaa jeneza ukafa kwa kuungua moto na kua majivu au kuliwa na mnyama bahari au Porini na mwili wako usipatikane kabisa we andaa pesa bank gawa password basi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ewe mtume mama D Naomba hicho kisa cha shetani alivyohangaika kuutafuta mwili wa Musa! No wonder ndio maana Mungu alificha kaburi la Nabii Musa lisionekane abadani

Kumbukumbu la Torati 34:5-6
"Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana.
Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo."


Yuda 1:9
"Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee."


Hatari tupu

Ibilisi anautafuta mwili wa Musa tangu BC mpaka AD.
 
Back
Top Bottom