Babu wa loliondo ni ilani ya ccm!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa loliondo ni ilani ya ccm!!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Pdidy, Mar 17, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,376
  Likes Received: 5,662
  Trophy Points: 280
  SAASA NAOANAA KUNA HATARI YA KUCHELEWA KUNYWA MAJI YA BABU..EWE BOSI WANGU NAOMBA NIKUBALIE LIKIZO YANGU KAMA NILIVYOOMBA ANGALIA HAWA WABUNGE WANAVYOANZA KUPELEKA WATU WAO NA SIE WATUPA SIKU 7 TUWE MAKAZINI.....
  NIMEFURAH JANA NILIKUWA NA DIWANI WA CCM AKANCHEKESHA SANA NA KUDAI UUNAJUA BANA HII YA BABU SIO AJABU UKIMSIKILIZA RAIS JK WAKATI WA KAMPEN ALISEMA MAMBO MAKUBWA YA AJABU YANAKUJA MKINICHAGUA KUWA RAIS SASA KWA TUNAOJUA HAYA NI MADOGO YAPO MAKUBWA ZAIDI ...KAZI IPO NJOO NA ARUSHA KULA HIYO

  Loliondo yageuzwa kete ya wanasiasa  *Mbunge atenga milioni 12/-kupeleka wapigakura

  Na Glory Mhiliwa, Arusha

  TIBA ya miujiza inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile sasa imegeuzwa kete ya wasiasa ambao wameendelea
  kujitokeza kwa lengo la kutaka kuungwa mkono kwa kuwapeleka wapiga kura wao kunywa dawa hiyo inayodaiwa kutibu maradhi sugu.

  Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Godbless Lema amekuwa mwanasiasa wa tatu kutangaza kuwasafirisha wananchi 200 kutoka kwenye jimbo lake kwenda Loliondo kunywa dawa.

  Mbunge huyo aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa amefanya hivyo baada ya kupata taarifa sahihi kutoka kwa ndugu na marafiki waliokwenda kutibiwa kuwa wamepona.

  "Nimetenga shilingi milioni 12 kwa ajili hiyo. Lengo langu ni kuwasaidia wenye maradhi mbalimbali jimboni kwangu watibiwe," alisema Lema.

  Mbunge wa kwanza kujitolea msaada kama huo alikuwa Bw. phillemon Ndesamburo wa Moshi Mjini (CHADEMA) ambaye awali alitoa helkopta kusafirisha wagonjwa waliozidiwa wakisubiri dawa na baadaye kukodi magari kusafirisha wananchi kutoka Moshi kwenda Loliondo.

  Jana gazeti hili liliripoti kuwa Mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani, Bw. Edward Lowassa naye amekondi magari kila kata kwenye jimbo lake kupeleka wananchi kunywa dawa hiyo.

  Kila mwanasiasa anayejitokeza anasema ameamua kuwasaidia wanancbhi wake wenye matatizo ya maradhi hayo ili waweze kupata dawa hiyo ambayo imegeuka gumzo nchini.

  Akifafanua zaidi sababu za msaada huo, Bw. Leama alisema pia maelezo ya Mchungaji Mwasapile kuwa ameoteshwa yamemsukuma, hivyo kuwataka watu wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali kufika ofisini kwake ili wapewe utaratibu na magari ya kwenda Loliondo.

  "Nitakuwa sijawawatendea haki wananchi wa jimbo langu kama msaada wa uponyaji unapatikana katika mkoa wangu nikashindwa japo kuwasaidia. Ndio maana nimetenga fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wangu ambao hawana uwezo wa kenda huko," alisema.

  Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi, akiwasihi wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kusaidai watu mbalimbali ambao hawana uwezo ili waweze kunywa dawa na kupona magonjwa mbalimbali.

  Kwa mujibu wa mbunge huyo kuna watu wengi wenye maradhi kama ya shinikizo la damu, kisukari ambao wanatamani kwenda kupata dawa hiyo kutoka kwa Mchungaji mwasapile lakini wameshindwak kutokana na gharama za usafiri kuwa kubwa.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wakati tukiendelea na tiba ya loliondo WATANZANIA msisahau kumwatch out JK maana naona hata media zimempa pumzi kwa sasa hazimwandami JK kama mwanzo.

  Nadhan JK anapata likizo ya mawazo manake haangazwi tena na media namna anavyoendesha serikali kijinga.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,376
  Likes Received: 5,662
  Trophy Points: 280
  Merytyna ni kweli ila
  tumechoka kurekebisha mitumishi ya shetan isyo badilika wacha tutukuze
  watumishi wa mungu waliotumwa kwa miujiza..tangu naijua jf thread nyingi zimeandikwa na nyingine zikimjulisha kitakachotokea kwenye mavikao yao ya kishenzi na kweli kinatokea akuna marekebsho kuna haja ya kumjadili..ukijisikia kumjadili nenda shika baibo usome ufikiriwe hata kwenye kale kaufalme adimu
   
 4. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  mbona kichwa cha habari na habari yenyewe vinakinzana?
  huyo aliesema hivyo ni nani ili wananchi tumjue maana tunaishia sema ni tetesi tu.hakuna mambo ya msingi zaidi ya kujadili zaidi ya kukurupuka na kuropoka?
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  unatumia vigezo gani? vya kanisani?
   
 6. tsar

  tsar Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  toa hii crap tafadhali maana hujui hata usemalo
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  yanakuja makubwa zaidi ya mabomu ya gongo la mboto mhhh
   
Loading...