Babu wa Loliondo kuburuzwa mahakamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa Loliondo kuburuzwa mahakamani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gamba la Nyoka, Dec 8, 2011.

 1. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,594
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi Wetu

  MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’, anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.

  [​IMG]
  nyumba yake mpya.

  Wanaharakati wameeleza kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo wanamfungulia Babu Ambi, mojawapo ni kumfilisi mali zote alizochuma endapo atakutwa na hatia ya ulaghai, wakati wa kutangaza maono aliyopewa na Mungu kuhusu tiba ya kikombe.

  Wanadai kuwa Babu Ambi, mkazi wa Kijiji cha Samunge, Loliondo, alitumia matatizo ya Watanzania ya kuugua maradhi sugu ili kujinufaisha, hivyo akatengeneza ulaghai wa tiba ya kikombe kwa maelezo kwamba ni ufunuo aliopewa na Mungu.

  Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).

  Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.

  [​IMG]
  ...sola anayotumia nyumbani kwake.

  Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo.

  Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika.

  Mali zote hizo, wanaharakati wanataka zifilisiwe kwa sababu zimepatikana kwa njia ya udanganyifu.

  Muungano wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Tanopha) ni wanaharakati wa kwanza kutoa tamko la kumburuza mahakamani.

  Tanopha wanasema, miongoni mwao, walitumia kikombe cha Babu Ambi lakini hakuna hata mmoja aliyepona.

  Wanasema, kila walipokwenda kupima ili waone matokeo ya tiba ya kikombe, majibu yalikuwa ni yaleyale kwamba hakuna mabadiliko.

  [​IMG]
  ...babu akiwa amepozi nyumbani kwake.

  “Hatuwezi kupoteza muda na fedha zetu kwa kwenda kunywa dawa ambayo haitibu, hii ni kuwarubuni wananchi, wengi wameuza mali zao, wengine kutumia akiba ya fedha walizokuwanazo kwenda Loliondo wakijua wangepona lakini cha kushangaza ni kwamba baadhi yetu wanakufa.

  “Wengine wako mahututi baada ya kupewa kikombe, tulikuwa na matumaini ya kupona hadi tuliacha kutumia vidonge vya kurefusha maisha vya ARV, hatuna mengi zaidi ila tunaomba umtafute mwenyekiti wetu akueleza zaidi,” alisema mmoja wa wanachama wa Tanopha.

  Mwenyekiti wa Tanopha, Julius Kaaya, aliliambia Uwazi kwa njia ya simu kuwa taasisi yake ilipeleka watu 14 kunywa dawa Loliondo lakini hakuna hata mmoja aliyepona.

  “Nakumbuka kwamba kipindi tunaenda huko Loliondo Machi 19, mwaka huu, tulifanya mkutano na waandishi wa habari, tulifika Samunge Machi 22, ambapo Machi 24 walikunywa dawa hiyo kila mmoja akiwa na matumaini ya kupona.

  “Baada ya siku 20 tangu wanywe dawa hiyo walienda hospitali kuangalia kama wamepona, daktari aliwaambia hakuna hata mmoja aliyepona, siku 90 baadaye majibu yakawa yaleyale,“ alisema Kaaya.

  MCHUNGAJI MTIKILA

  Naye Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikila kwa upande wake amesema kwamba dawa hiyo haitibu na analishughulikia suala hilo ili kumfikisha mahakamani pamoja na mawaziri, wabunge na viongozi wa juu waliokunywa kikombe.

  [​IMG]
  ...mjengo wake mpya.

  “Mawaziri hao wamewahamasisha wananchi kwenda Loliondo kunywa dawa, lazima tuwashitaki pamoja na viongozi wa dini waliopiga debe,” alisema Mtikila. Viongozi wa dini waliohamasisha ni Askofu Thomas Laizer na Martine Shayo.

  Baadhi ya Mawaziri waliopata kikombe ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli. Wengine ni wabunge Augustino Mrema, Edward Lowassa na wakuu wa mikoa Yohana Balele na Abbas Kandoro.

  TAMKO LA WIZARA

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda, alisema hivi karibuni kuwa kikombe cha Babu siyo tiba na kwamba wote waliokwenda Loliondo, walipoteza muda.

  Kauli ya waziri, ilifuatia ripoti ya uchunguzi wa madaktari bingwa kwamba kikombe cha Babu wa Loliondo, hakitibu.

  WABUNGE NAO

  Katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 10, baadhi ya wabunge walitaka Babu wa Loliondo achukuliwe hatua kwa sababu dawa yake haitibu.

  Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, alikwenda mbali zaidi kwa kutaka mawaziri waliokwenda Loliondo, wahojiwe na waseme kama wamepona, kwani wao kwa kiwango kikubwa walihusika kupotosha umma.

  [​IMG]
  ...babu Ambi akiwa amepozi, pembeni ni bafu la kisasa analotumia kwa sasa.

  UTETEZI WA BABU

  Kwa upande wa Babu Ambi, ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa dawa yake imeponyesha wengi.

  “Kama hawajapona siyo makosa yetu. Tuliwaambia kabla kuwa katika tiba hii kigezo cha kwanza ni kuwa na imani na hapa tuna uthibitisho wa kutosha wa watu walioponywa na maajabu ya dawa hii wakiwemo wagonjwa wenye Ukimwi,” alisema Babu Ambi na kuongeza kuwa anapigwa vita na wengi kwa sababu ya wivu.

  Kuhusu utajiri wake, alisema kuwa yeye hana mamilioni ya fedha kama inavyodaiwa ila akakiri kumiliki nyumba ya kisasa pamoja na magari mawili ambayo amesema yanamsaidia kubeba dawa pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Loliondo.

  KUHUSU KIKOMBE

  Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa KKKT Arusha, Thomas Laizer, zaidi ya watu milioni tatu wameshatibiwa Loliondo. Kila mgonjwa alikuwa analipa shilingi 500, hivyo kwa hesabu ya watu milioni tatu, maana yake kikombe kimeshaingiza zaidi ya shilingi bilioni 1.5.
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  kazi kweli kweli, hili likifanikiwa nadhani itakuwa mwanzo wa matatizo ktk sekta nzima ya 'born again faith'
   
 3. libent

  libent JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hakuna aliyewapeleka waliambiwa mwanzoni wakabisha sasa wamshtakie nini babu wa watu wanjinga ndio waliwao. Nashut down
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Katika hili serikali nayn ilikuwa na uzembe mkubwa kwakusema kuna watu ambao watachukuliwa vipimo na matokeo kutolewa kinachonishangaza mpaka leo kimya
   
 5. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  kila siku tunasema watanzania tuna matatizo makubwa matatu!!!ujinga wa watu kushindwa kusikilza,matokeo yake mzee wa watu anamalizia maisha yake raha mstarehe!!!!kwa hili apaswi kufilisiwa ila University of Dar e es salam wampe degree ya heshima,Phd kwa kubuni alichobuni na kufanikiwa kupata popurality.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Umbe wao, hawajawahi kuiweka tangazo popote kuwa anatibu hata kwene magazeti ya kizushi hajkawahi kuweka kilichowapeleka huko ni kitu gani??
   
 7. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  ......ila University of Dar e es salam wampe degree ya heshima,Phd kwa kubuni alichobuni na kufanikiwa kupata popurality.


  hilo halina ubishi, huyu mzeee anapaswa kuwa awarded kwa kile alichokifanya.
  kila kitu mzeee wetu kapata katika kumalizia uzee wake hapa duniani, kapata nyumba nzr yenye kila kitu, kapata mwili (cheki shavu dodo) sasa anapaswa apate na mke wa kumburudisha na kumfariji anapoimalizia safari yake ya mwisho hapa duniani......!!!

  Bravo babu ambi......!!!!!!!

  [/QUOTE]
   
 8. R

  RUKAKA Senior Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Babu alisema hajaweka Bango ila watu ndo waalimfagilia na dawa yake isitoshe wizara ilihusishwa na wlieleza kuwa dawa haina madhara. Babu atawashinda kwani dawa ilikuwa ya kiimani zaidi. Labda waliokunywa wasipone walikuwa hawana IMANI. Kabla ya kumbuluza Babu ebu Tuombe wizara yenye Dhamana Itoe tamko kama ilivyofanya awali tujue Kulikoni?
   
 9. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona hata Aruu nazo mm haziniponyeshi na serikali inaendele kuzipigia debe.Kwa hiyo niuungane na wengine wasioponyeshwa na dawa hiyo kuiishitaki serikali yetu?Mara ngapi tumekuwa tukipata dawa hospitalini zinashindwa kutusaidia?Wenye wivu na Babu Ambi mm nasema wajinyonge tu.
   
 10. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Photoshop.
   
 11. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  [/QUOTE]

  homeboy una akili sana!!!tena sana!!na hivi vyuo vyetu vingekuwa vinajua namna ya kuwatunuku watu hizo honorary degree,huyu mzee alipaswa kabisa!!!!maana alibuni kila level ya elimu!!!amini usiamin kuna madaktari wa binadamu walikunywa kikombe cha babu!!!anapaswa apewe Phd!!!!
   
 12. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  mbona dawa ilikuwa Jero tu!.
   
 13. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Freemason were at work na watu kwa ujinga wao wakakimbilia huko kwani aliwalazimisha?
  Wewe kama dawa inaponya kwa imani na imetoka kwa Mungu ni kwa nini wasingeomba kwa imani na kuponywa. Asante babu kwa kuitangazia dunia ukilaza wa waTz kuanzia rais mpaka raia wa kawaida(mkulima).
   
 14. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huyu babu awe Mkweli au Muongo hana makosa. Ubunifu wa namna hii ndio tunautaka kwenye fund raising. Mawaziri na wabunge wetu wote wamechanga, ndugu zangu wasafirishaji wameneemeka na hatimaye Samunge imetangazika. Babu anachotakiwa kufanya ni kujenga 'Fools Memorial Tower' pale Samunge na majina ya viongozi wetu walionda kupiga kikombe yawe ya mbele kwenye orodha.
   
 15. M

  Mwiburi New Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg zangu wanaJF sitaki kusema kwamba namtetea Babu ila tu ifahamike kwamba, hapa duniani haijawahi kupatikana dawa ambayo inaweza kutibu watu wote kwa namna sawa. Miili ya binadamu inatofautiana sana katika mfumo mzima wa kinga na ndo maaana kuna baadhi ya watu hutibiwa kabisa na dawa fulani wakapona lkn dawa hiyohiyo inashindwa kufanya kazi kwa mtu mwingine. Lkn pia naomba ifahamike kwamba mambo ya kisayansi hasa haya yanayohusisha magonjwa na tiba ni vigumu sana kumhukumu mtu bila kufanya utafiti wa kina tena wa muda mrefu. Hata records za WHO zinatambua kuwa ili dawa iidhinishwe kuwa tiba sio lazma iwe na uwezo wa kutibu ugonjwa husika kwa 100%. Tena dawa ya Babu inakuwa complicated zaidi pale unapoweka aspect ya IMANI katika sayansi. Kwa ushauri na maono yangu naona ni vigumu sana kwa watakaomshitaki Babu kufanikiwa katika adhma yao. Nawasilisha
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  akitoa tangazo la kuwa anataka mke, semeni kuna mtu anataka,
  mimi sipo lakini.
   
 17. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna aliyeitwa kwake ni dhiki zao/zetu ndizo zilizoleteleza haya yote, mwacheni babu ale bata jamani mbona mna wivu bunini kamuhogo kenu na nyinyi!!!
   
 18. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,705
  Likes Received: 2,388
  Trophy Points: 280
  Mucho agreed !i propose to start fact finding for all viongozi waliopata tiba kule na kwa maradhi gani then wataalamu wetu wa virtual graphic humu ndani watujengee virtual mnara humu tubandike majina yao untill end of time!
   
Loading...