Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Huyu Mzee Mungu ambariki, kazi yake inaonyesha alivyo mtiifu kwa Mungu.....
Wanaomlaani, Mwenyezi Mungu awaadhibu.
...


Amen! mimi ndugu zangu wawili wamepona yani nakosa maneno ya kusema, Mungu ni Mwingi wa Rehema na kupitia Babu wengi watapona. Wanoamini waendelee kuamini na wasio amini wakae kama walivyo!
 
waanagalie tu wasije wakasababisha babu akakosa nguvu ya kuendelea kutoa dawa tena
 
Aisee ndo yamekuwa hayo tena? Kwa kweli hizi ni taarifa mbaya kwa watu ambao walikuwa wamejiandaa kwenda kule. Haf Mambo ya Mungu hayawezi kuthibitishwa na sayansi, hapo ndo shetani sasa anaanza kuingilia. Nina imani atashindwa na kulegea.
 
Sasa dawa ambayo imeshapikwa na Babu aimwage au? nini kuhusu hao wanachi waliokopa laki na nusu za kufika hadi huko halafu warudi watupu na magonjwa?

Serikali inaleta masihara kama hii habari ni ya ukweli.
 
Utafiti huo utachukua miaka mingi, na huenda matokeo yasitolewe hadharani..
 
Sasa dawa ambayo imeshapikwa na Babu aimwage au? nini kuhusu hao wanachi waliokopa laki na nusu za kufika hadi huko halafu warudi watupu na magonjwa?

Serikali inaleta masihara kama hii habari ni ya ukweli.
Wanataka machafuko yatokee........
 
utafiti wa nini wakati watu wamepona? Au utafiti utazuia asitoe huduma? Upuuzi mtupu . Wenye biashara za dawa wameanza upuuzi wao. Waashindwe na walegee
 
Hivi hii serikali iliyoshindwa majukumu yake inahusikaje na shughuli za babu wa Loliondo? Jamani ama kweli tunashida sana nchi hii serikali ya marufuku imetoka wapi? yaana baada ya kusaidia kuboresha mazingira watu wapate huduma wao wanapiga marufuku? hivi wananchi ni mabwege kiasi hicho mbona hawapigi marufuku hospitali yao ya ocean road inayoendelea kuua watu wasio na hatia kila siku hebu tuamkeni watanzania wenzangu hawa majuha kalulu tukiwaachia tutaigia nao msikitini
 
Wakati utafiti ukiendelea viongozi watakuwa wakienda kwa siri kutibiwa , wengine watakuwa hawaruhusiwi kufika huko.
 

Siamini habari hii....kama ni kweli litakuwa jambo la ajabu kabisa itabidi huduma hata za maombezi pia zifungwe ili hadi zije kuthibitishwa.....
 
Kama ni kweli basi angalau, at least kuna watu bado wana akili timamu serikalini.
 

Felister,

1. Wagonjwa wenye shida ambao hawana nauli watafikaje kwa babu kama yeye peke yake
ndie anayetoa hiyo dawa na si mwingine?

2. Southern countries ndio zilizoathirika sana kwa ugonjwa wa UKIMWI, are you telling me all
those people should come to TZ to get this treatment from him ONLY?

3. Kama kweli hii dawa Mungu ndiye aliyemfunulia, vipi kuhusu wagonjwa ambao wanafia
njiani wakielekea huko Loliondo? Hawakustahili kupata hii dawa ili wapone?

4. How come we only hearing story from people but we havent actually see someone who got
healed, utasikia tu mtoto wa rafiki yangu, mama yake rafiki yangu, mjomba wangu
anayekaa mbeya etc?
 
Nchi hii ina matatizo mbona za Shekh Yahya alipoamua kumwongezea ulinzi mkuu wa kaya wizara ya afya haikumuomba kuzifanyia utafiti kuona kama zitamdhuru. pia mabango ya waganga yamejaa jiji la Dar hakuna anayefuatilia au kwa kuwa kwenda Loliondo kuna allowance ...
 
huo mti kama unajulikana si wachukue sample waifanyie utafiti ina kitu gani? tatizo kuna nguvu za maombi ndio dawa ifanye kazi sasa hapo sijui wizara ya afya ina role gani.. kwa kua wanatumia kodi zetu kwa ajili ya hiyo safari cha maana waweke vizuri mazingira ili kujiandaa kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kulipuka huko kutokana na uwingi na mikusanyiko wa watu
 
hivi hawa wizara ya afya wana nini, mbona siwaelewi, kama wagonjwa si wao, wao wanataka kufanya utafiti, halafu iweje, lini watamailza utafiti...???? jamani wawaache watu watibiwe, KILA MTU ANAENDA KWA BABU KWA HIARI YAKE, kama vile anavyokwenda kweny zahanaTi au kituo cha afya kingine, , ni hari ya mtu, WAACHENe WANANCHI KWATIBIWEEEE, grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Mkuu kuchukua wagonjwa eg wa HIV na kuwatumia kwenye majaribio kama wameponywa na hiyo dawa ni kinyume na medical ethics,utakuwa unaingilia haki ya privacy sharti hiyo dawa ipatikane ifanyiwe majaribio kwanza,hapo imekaaje?


kwani watawalazimisha? Si watafute ambao wako tayari kufanyiwa vipimo? Kama wanaweza kushuhudia wamepona kwenye vyombo vya habari wataacha ku colaborate na serikali?
 
Jamani mi nimeona vitu lakini hiki cha loliondo kimenishtua sana, kwasababu Mzee huyu ni wa ajabu na ameweza kujipatia njia nzuuurii ya kutafuta Pesa bila kutumia unyang'anyi wala Ndumba, bali kwa kutumia Akili yake.
Hakuna uthibitisho wa kisayanxzi kwamba dawa hiyo inaponesha, na kimachoshangaza Eti Dawa hiyo huponi ukichota mwenyewe mpaka achote kwa mkono wake.
naomba tuwege makini, na naomba uthibitisho ili na mimi niende bana

Eti wadau ni njia ya kutafuta Ela au Dawa kweli?
 

Mkuu.
mchango wako poa tu lakini umeutia kasoro hapo penye rangi ya buluu. Katika hao wanaokwenda kwa babu wamo wanaokwenda msikitiki. Pia ni wananchi na watanzania wenzako.

Naelewa kuwa maamuzi mengi ya serikali iliyopo hivi sasa yanaudhi na yanaumiza wananchi lakini huwatendei haki hao wanaoingia msikitini kwa kauli yako. Wao pia wanaumia na maamuzi ya "hawa majuha". Na kauli yako hiyo ni kiashiria cha ubaguzi au unahubiri mgawanyiko wa wananchi wenzako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…