Babu Duni ajenda yako nini dhidi ya CHADEMA?!

Babu Duni ajenda yako nini dhidi ya CHADEMA?!

Labda hajasikilizwa mzee wa kifo cha Mende,ndio maana anatumia media kutoa ya moyoni.
 
Nimesoma kwenye vyombo vya habari Mh.Juma Duni Haji aliyekuwa mgombea mwenza wa Lowasa kwa tiketi ya CHADEMA.

Akilalamika kuhusu siasa za ndani ya CHADEMA kwenye media baada ya kurudi CUF.

Kwanza alidai ndani ya CHADEMA kila mwanachama anasharubu,kwa maana kiongozi wa ngazi ya chini anaweza kupinga maamuzi ya ngazi za juu.

Pili leo nimesikia tena anadai ndani ya CHADEMA kuna siasa za ubinafsi(kujali maslahi yao) kuliko wengine/vyama vingine.

Yawezekana yote hayo ni kweli kwakuwa hakuna chama kisichokuwa na mapungufu (mfano CUF toka imeanzishwa nafasi ya katibu mkuu imeshikiliwa na MAALIM S.S.HAMAD,sio kila mtu anafurahia hilo wanaona ni kasoro lakini wapo kimyaa kulinda maslahi Mapana ya CUF.

Hizi habari zinazozagaa kwenye media hazijakanushwa na Babu Duni, inatufanya tuamini kuwa ni kweli kasema.

lkwa kiongozi mkubwa wa kitaifa kama Babu Duni naamini anapaswa kuwa makini katika ukosoaji wa siasa za ndani ya chama wanachoshirikiana UKAWA kupitia kwenye media badala ya ushauri katika vikao vya ndani au viongozi wakuu wa CHADEMA wenye ushawishi.

Vinginevyo anaweza kujikuta anaungana na akina ZZK kubomoa chama ambacho yeye pia ana maslahi nacho katika check and balance dhidi ya serikali ya CCM.

Mchango wake unaheshimika/kukubalika katika uchaguzi wa 2015.keep your legacy Babu Duni,Dont mess! your common enemy is Tanzanian poverty.

Haya tu.ni mtizamo wangu.Maoni tofauti yanakaribishwa.

Cuf ..au babu duni atakuwa anakosea sana na kuwa mpungufu wa Shukrani kwa kuwa tangu ianze Cuf viti vingi vya kura kupata Bara ni viwili .....Mwaka huuu kupitia ukawa viti vya kura kumi.......haoni ukawa imesaidia
Angetakiwa kwa Sasa aongelee. ..mustakabli wa znz ...na kufikiria Nani wa kumpokea Maalim Kijiti ambaye umri umeenda ...kuliko uchonganishi
 
Babu Duni ni mtu makini hawezi kuripoka ktk media hayo ni majungu yanayofanywa na CCM ili kuvuruga UKAWA!
 
Cuf ..au babu duni atakuwa anakosea sana na kuwa mpungufu wa Shukrani kwa kuwa tangu ianze Cuf viti vingi vya kura kupata Bara ni viwili .....Mwaka huuu kupitia ukawa viti vya kura kumi.......haoni ukawa imesaidia
Angetakiwa kwa Sasa aongelee. ..mustakabli wa znz ...na kufikiria Nani wa kumpokea Maalim Kijiti ambaye umri umeenda ...kuliko uchonganishi
Halioni hilo mkuu.anafikiria kuleta fitna ndani ya CDM
 
Babu Duni itakuwa wachaga wamemzika mgao wake wa pesa walionunuliwa na Mbowe.
 
Back
Top Bottom