Simplicity., haya mambo nimeyasikia sana tu, wala si kidogo kwa namna mbili tofauti. Kwa zamani, wadada walikuwa wakiwafanyia hivi waume zao pale ambapo walikuwa wakipata manyanyaso toka kwa wifi, ndugu za mume au mume mwenyewe kuwa kwanini tangu aolewe hajazaa! Kwa mantiki hiyo, baadhi yao walikuwa wanatoka nje ya ndoa kimya kimya, na kwenda kujaribu nje kisha kuleta mimba za nje ndani kuondoa adha ya kusemwa na kunyanyaswa. Na enzi hizo technolojia ilikuwa si kubwa, hivyo kugundua mtoto si wako haikuwa rahisi, labda kwa muunekano awe tofauti kabisa.
Kwa nyakati hizi, nafikiri kukuwa kwa utandawazi, kumomonyoka kwa maadili, kuingia kwa tamaduni za nje, watu kutokumuogopa Mungu, kutokuheshimu ndoa, migogoro ya ndani ya ndoa, nk kumesababisha baadhi ya wanandoa kutokuwa waaminifu na kuwa na mahusiano na watu wengine. Mahusiano yanapozidi, uangalifu hupungua na matokeo yake ndiyo hiyo unakuta mke/mume wa mtu kazaa nje ya ndoa yake au mume anabambikwa mtoto.
Sasa tukirudi kwenye mada yako na hasa swali lako "Jamani hili swala la akina mama kuplagiarise watoto na wapambe wao kujaribu kuwanusuru kwa kuwapa watoto fake brands mbona linakua kwa kasi sana siku hizi?" Ni kuwa binafsi naona sababu ya kubambikwa mtoto, kama si kosa la mke kuwa mzinzi na kujikuta kabeba mimba ya mwanaume mwingine, basi mume mwenye mke anaweza kuwa chanzo. Maana matatizo ya uzazi yapo, na yanaweza kuwa kwa mke au mume. Wengi wa wanaume hukiria tatizo ni mwanamke na kuanza kumlaumu na kumnyanyasa mkewe kwa kutokushika mimba badala ya kukaa chini na kuhangaika kwa pamoja kujua kiini cha tatizo.
Wanaume twapasa kubadilika tunapokuwa na changamoto za kupata watoto ndani ya ndoa kwa kushirikiana na wenzetu ili kuepuka matatizo kama haya.
BTW, huyo mume wa huyo dada alifahamu kuwa huyo mtoto si wake?