Ndio, Mama yangu aliniambia mwanamke anajifunza kupenda. Hivyo nichague mwanaume mwingine kwa kutumia akili( yani awe na vigezo vyangu vingi ninavyo vipenda). Baada ya kuchagua niolewe. Nikafanya hivyo.
Nikaolewa wakati moyoni yupo mwanaume mwingine, harafu nikajifunza kumpenda mme wangu.
Mme wangu akawa ananipenda sana, maana nilikuwa simuhesabii makosa, yani hata akinikosea sioni shida maana nilikuwa namkubali sana ila sio kumpenda.
Miaka ikapita nikawa namsahau x taratibu, ila nikimkumbuka naliaaaa napoa naendelea na maisha.
Nikawa namkumbuka baada ya mwezi! Mara inapita miaezi mitatu ndio namkumbuka, mara miezi nane mpaka nikawa simsikii tena. Nikaanza kumiss mme wangu.
Mme wangu akisafiri naugua, wakata awali mme wangu alikuwa akisafiri nakuwa ido namuwaza x.
Nikaangukia kwenye penzi zito la mme wangu !!!
NB: past inauma lakini unaweza ukaikimbia na ukaenjoy the present.
Sent using
Jamii Forums mobile app