Babati kwawaka Moto!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babati kwawaka Moto!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tusker Bariiiidi, Jan 29, 2011.

 1. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wanakijiji wa vijiji 4 katika Bonde la Kiru wamechoma moto viwanda vi2 vya sukari,mashamba na Matrekta 20 mali wawekezaji fake wa Kihindi... My take; Wananchi wamechoka jamani,wananyanyasika katika ardhi yao... PEOPLE.'S POWER!!!
   
 2. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  safi sana hiyo.....
   
 3. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hayo ndo matokeo ya kugawa ardhi ya wananchi kwa wageni bila ya kuwashirikisha!! Viongozi wakae macho...dalili ya mvua ni mawingu!
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Vuguvugu hizi zinaonyesha wazi kuwa wananchi wamechoka kuonewa pamoja na hali ngumu ya uchumi,huku tukidanganywa na kuambiwa kuwa uchumi wetu unapaa... Mara nyingi 1.Ogopa Maji yaliyotulia 2.Simba mwenda pole ndio mla nyama ... Wa-Tanzania sasa wameamka!!!
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sasa wageni wanaogawiwa cash money itakuwaje mungu wangu
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Si wageni mkubwa, ni wenzetu humuhumu tulowaamini na kuwapa majukumu sasa wametugeuka wanachukua hela zetu kwa mgongo wa wageni!!!
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Duh busara itumike badala ya maguvu
   
 8. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ndio maana kila baada ya nyumba 3 huku Uswazi kama haukuti Msanii wa Bongo Flava basi Mamiss au Waigiza Filamu... Yaani...
   
 9. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Busara ilitumika toka miaka ya Themanini... Lakini mwekezaji hakujali!!! Sasa vijana walioona Baba zao wakitumia Busara miaka hiyo ujue sasa wamechooooookaaaaa!!!
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  safi sana bora wananchi watoke ucngizini na kudai haki yao hapaitaji busara kujadiliana mafisadi watakwambi tukiwapokonya watatudai fidia kubwa
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huyu mgeni anakuja mikono mitupu akijiita mwekezaji, anakopa kwenye benki zetu wenyewe, tunampa ardhi yetu anawekeza kisha anatuajiri kama vibarua kumfanyia kazi kwa ujira mdogo. Akivuna faida anapeleka kwao, sio tunaita wawekezaji!!!????!!

  Enzi za Mwalimu hizi mali zilikuwa hazichomwi moto bali zinachukuliwa na umma. Hiyo pipoooz waliofanya hawa wanavijiji ni ya kumwaga ugali na mboga tukose wote. Hivi tunashindwa nini mbona Bob Mugabe aliweza pale Zim?
   
 12. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Safi sana, na ole wao hao wawekezaji fake wajaribu wapige raia waone. Wembe uendelee na maeneo mengine kama mbarali na barrick ili tupate haki zetu tunazonyonywa.
   
 13. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Good!... Very good!...
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Hii mara nyingi ndio dawa rahisi ya watu wanaoonewa na hawasikilizwi na hawa matapeli wanaogawana nchi yetu kama vile wengine hawapo.
   
 15. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  natoa baraka zangu kwa wazalendo wa babati na pia natoa wito kwa watanganyika wooote kuiga mfano wao.
   
 16. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii inatia huruma!
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wana haki ya kupigania haki yao!Angalau wanajua hilo!
   
 18. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huko kiru wahindi wamewatesa sana wananchi. halafu huyo mtu sijui ndugu yake leo ndiye mbunge wao. what a shame.
   
 19. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #19
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ................. ndio gia zao ! ...... kama yule wa Igunga ! ........... nimehemkwa sana, nitumie utaratibu gani kujiunga nao mstari wa mbele !
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Mwanza, Manyara balaa
  • Wananchi wachoma kiwanda cha sukari

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] MIKOA ya Mwanza na Manyara, jana ilikumbwa na machafuko yaliyosababisha uchomaji wa viwanda viwili vya sukari, matrekta 20, uharibifu wa mali pamoja na vipigo kati ya wafanyabiashara ndogo ndogo (Wamachinga), polisi na askari wa jiji.
  Mkoani Manyara vurugu kubwa zimetokea ambapo wanakijiji wa vijiji vinne vya bonde la Kiru, Babati, Manyara wamechoma moto viwanda viwili vidogo vya sukari, mashamba ya miwa na matrekta yasiyopungua 10.
  Kwa mujibu wa wakazi wa kijiji hicho waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, kwa sharti ya majina yao kutoandikwa, walisema sababu ya vurugu hizo ni mgogoro wa ardhi baina ya wanavijiji na mwekezaji mwenye asili ya India, aliyetambulika kwa jina moja la Mugesh.
  Walisema kuwa vurugu kama hizo ziliwahi kutokea mwaka 2005 ambapo wawekezaji watatu wenye asili hiyo waliuawa, matrekta zaidi ya matatu na mashamba yalichomwa moto.
  Miongoni mwa viwanda vilivyokumbwa na vurugu hizo ni Suba Agro, ambacho huzalisha mbegu za mahindi, mtama, choroko na miwa.
  Walibainisha kuwa vurugu za jana zilisababishwa kukamatwa kwa mwanakijiji mmoja ambaye alidaiwa kuvamia kwenye shamba la mwekezaji mmoja ambaye aliamua kuwaita polisi ambao walimkamata.
  Walisema mbali na kukamatwa kwa mwanakijiji huyo pia kuna ng'ombe walikamatwa kwa madai ya kuchungwa kwenye eneo la mwekezaji huyo.
  Waliongeza kuwa kutokana na tukio hilo jana alfajiri wananchi waliamua kuvamia mashamba ya wawekezaji hao na kuanza kuyachoma moto pamoja na matrekta na viwanda vidogo vya sukari wanavyovimiliki.
  Walisema kuwa mwekezaji huyo kwa muda mrefu alikuwa na mgogoro wa ardhi na wanakijiji hao ambapo alifungua kesi kwenye mahakama na Septemba mwaka jana na alishinda.
  Wananchi hao waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa vurugu hizo zilishindwa kutulizwa na askari kutokana na uchache wao.
  Juhudi za Tanzania Daima Jumapili, kuwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Manyara, Parmenas Sumary, ziligonga mwamba kutokana na mawasiliano kutokuwa mazuri.
  Tanzania Daima Jumapili, liliwasiliana na Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo Benedict Msuya, ambaye alisema hakuwapo eneo la tukio hivyo hawezi kuzungumzia vurugu hizo.
  "Ndugu yangu kwa bahati mbaya mimi nilikuwa safarini Dar es Salaam na hivi sasa nipo njiani narudi Manyara, siwezi kukusaidia, wasiliana na RPC," alisema.
  Mwanza
  Mkoani Mwanza vurugu kubwa zilizuka kati ya wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga), mgambo wa jiji na askari polisi, hali ambayo ilisababisha kipigo na kusimama kwa shughuli za uzalishaji mali.
  Mapigano hayo yalianza majira ya saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni, na yalisababishwa na wachinga kukaidi amri ya Halmashauri ya Jiji iliyokuwa ikiwaondoa kwa nguvu kwenye maeneo ya katikati ya jiji walikokuwa wakifanyia biashara zao.
  Wafanyabiashara hao waliamua kupambana na askari wa jiji kwa kuwarushia mawe, hali iliyosababisha uharibifu wa magari, pikipiki pamoja na maduka.
  Hata hivyo askari wa jiji hawakuweza kuhimili vurugu za wamachinga hao hivyo kuamua kukimbia, jambo lililowafanya wafanyabiashara hao kuandamana hadi ofisi za jiji.
  Katika ofisi hizo walikutana na Mkuu wa Mkoa, Abass Kandoro, Mkurugenzi, Wilson Kabwe, baadhi ya madiwani na viongozi wengine waandamizi wa serikali ambao walifanya nao mazungumzo.
  Kandoro alizungumza na wamachinga hao chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU), ambapo aliwaambia kuwa serikali imeshatenga maeneo katikati ya jiji, eneo ya Makoroboi, Mirongo, Mlango Mmoja pamoja na Vitunguu dampo kwa ajili yao.
  Alisema maeneo hayo wanaruhusiwa kuendeshea biashara zao lakini wasijenge vibanda wala kupanga meza.
  Baada ya kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, baadhi ya wamachinga waliondoka katika ofisi za jiji na kurudi mitaani kuendesha vurugu tena, na hapo ndipo askari wa FFU walipoingia nao mitaani na kufukuzana nao, hali ambayo iliendelea kuzua hofu na tafrani kubwa.
   
Loading...