Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Clayton Chipando almaarufu kama Babalevo, aliyekuwa mtiania na mgombea wa ndani wa Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kigoma Mjini amejiharibia. Kama ulikuwa ni mtego, umemnasa.
Kitendo chake cha kumpora 'kihuni' karatasi ya matokeo Katibu wake wa CCM wa Wilaya, aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa mgombea wa CCM jimboni humo, ni ukosefu wa nidhamu na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za chama chake-CCM.
Soma >>> GE2025 - Baba Levo akinukisha, ataka kura zihesabiwe upya
Alipaswa kuwa mtulivu na msikivu. Kama kuna malalamiko yoyote aliyonayo, alipaswa kuyawasilisha kwa viongozi wake kwa mujibu wa taratibu za chama chake. Taarifa bado zitawasilishwa Kamati Kuu na uamuzi wa nani hasa ni mgombea wa CCM Kigoma Mjini utafanywa huko.
Ni kwakuwa hazijui taratibu za kichama au alikuwa na ajenda zake zilizojificha kuhusiana na uhalali wa uchaguzi ndani ya chama chake? Si mara moja wala mbili, Kamati Kuu ya CCM imewahi kuwapitisha walioshika nafasi za pili, tatu na hata nne kwenye kura za maoni. Fujo zake zimemharibia kabisa.
Pia soma >> GE2025 - Baba Levo aangukia pua, Ng’enda aibuka mshindi Kigoma Mjini kwa kura 2,168 dhidi ya 2,080