GE2025 'Babalevo' amejiharibia, amepiga teke fuko la pesa!

GE2025 'Babalevo' amejiharibia, amepiga teke fuko la pesa!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwanini asishinde na ccm wako peke yao kwenye huo uchaguzi.

Useme kwasababu atagombea na Zitto kabwe ccm B hivyo ccm wanao uwezo kumpa Zitto jimbo ili kuhalalisha wizi wao.

Ili waseme act wameshinda hivyo kuondoa dhana ya upinzani kulalamikia kanuni za uchaguzi.
Sisiemu unawajua vizuri wao wakiwa wanataka kuiba kura huwa hawaangalii sijuo zito , sijui nani hata 2020 watu walitegemea kitu Kama hicho
 
Baba Levo ameshinda kihalali inabidi apewe ushindi wake halali na ninachojua huyo Baba Levo atateuliwa na Sisiemu kwakuwa katumwa na Diamond sio kwamba kajituma na Diamond anawasaidia sisiemu katika mambo yao ya kampeni so is about win win game.

Swala la integrity litajulikana Ila huyo Mbunge aliyekuwa nafasi ya kwanza hawezi kushinda .
The chawa!
 
Sisiemu unawajua vizuri wao wakiwa wanataka kuiba kura huwa hawaangalii sijuo zito , sijui nani hata 2020 watu walitegemea kitu Kama hicho
Haya ya Zitto ni mpango wao pia, ACT wana ruzuku kubwa na ccm inataka kujiosha kimataifa.
 
Clayton Chipando almaarufu kama Babalevo, aliyekuwa mtiania na mgombea wa ndani wa Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kigoma Mjini amejiharibia. Kama ulikuwa ni mtego, umemnasa.

Kitendo chake cha kumpora 'kihuni' karatasi ya matokeo Katibu wake wa CCM wa Wilaya, aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa mgombea wa CCM jimboni humo, ni ukosefu wa nidhamu na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za chama chake-CCM.


Soma >>> GE2025 - Baba Levo akinukisha, ataka kura zihesabiwe upya

Alipaswa kuwa mtulivu na msikivu. Kama kuna malalamiko yoyote aliyonayo, alipaswa kuyawasilisha kwa viongozi wake kwa mujibu wa taratibu za chama chake. Taarifa bado zitawasilishwa Kamati Kuu na uamuzi wa nani hasa ni mgombea wa CCM Kigoma Mjini utafanywa huko.

Ni kwakuwa hazijui taratibu za kichama au alikuwa na ajenda zake zilizojificha kuhusiana na uhalali wa uchaguzi ndani ya chama chake? Si mara moja wala mbili, Kamati Kuu ya CCM imewahi kuwapitisha walioshika nafasi za pili, tatu na hata nne kwenye kura za maoni. Fujo zake zimemharibia kabisa.

Pia soma >> GE2025 - Baba Levo aangukia pua, Ng’enda aibuka mshindi Kigoma Mjini kwa kura 2,168 dhidi ya 2,080
Kukiuka taratibu ni kawaida ya chama.
 
Back
Top Bottom