Plot4Sale Baba yangu anauza kiwanja chake, amekwama anahitajika akatibiwe

Anko Elly

Member
Feb 22, 2017
69
70
Habari zenu wapendwa, matumaini yangu kuwa hamjambo na mnaendelea na majukumu ya kusukuma gurudumu la maisha.

Nisingependa kuweka personal life yangu hapa, sema imenibidi kulingana na hali halisi iliyopo hivi sasa.

Nimepambana sana na Mzee wangu kutafuta matibabu lakini imeshindikana, ndio tukapata shauri la kuuza eneo lake ili tuweze kupata hela ya kwenda kutibiwa nje.

Nimeambatanisha na picha ya eneo ambalo lipo Madale nyuma ya kiwanda cha wazo, kiwanja hakina hati sema kina nyaraka zote muhimu na kinatambuliwa kuanzia ngazi ya shina mpaka serikali za mitaa.

Kwa yeyote yule aliyte ayari anaweza kunicheki PM. Bei yake inaanzia milioni 20 mazungumzo yapo, pia mnunuzi anaweza kulipa kwa awamu mbili kulingana na bei tutakayoafikiana

Huduma za msingi karibu zote zimefika, ikiwemo maji, barabara, umeme n.k

Karibuni sana
 

Attachments

  • Iamge2.jpg
    Iamge2.jpg
    11.5 KB · Views: 96
  • Iamge3.jpg
    Iamge3.jpg
    18.1 KB · Views: 92
  • Iamge4.jpg
    Iamge4.jpg
    29.1 KB · Views: 100
  • Iamge5.jpg
    Iamge5.jpg
    25.7 KB · Views: 92
  • Image1.jpg
    Image1.jpg
    21.5 KB · Views: 92
Pia usalama na uhakika na eneo toka kiwanda mipaka yake vipi sababu kuna miaka kulikuwa na migogoro na kiwanda cha cement
 
mbona hujaweka size ya hicho kiwanja???

watu wanasema utapeli sababu madalali wanakuwaga na maneno ya mgonjwa ili uingie kichwa kichwa ubabuliwe fasta
Ukubwa wa kiwanja kwa ujumla ni heka mbili, lakini tunachouza ni heka moja, na sisi tubakiwe na heka moja ya akiba hapo baadae
 
Pia usalama na uhakika na eneo toka kiwanda mipaka yake vipi sababu kuna miaka kulikuwa na migogoro na kiwanda cha cement
Hatupo kwenye upande wa mgogoro na kiwanda, kiwanja kipo Flamingo karibu kabisa na kituo kidogo cha Polisi, nyuma ya kiwanda cha saruji wazo. Karibuni sana
 
Ndugu bunju wiwanja milioni nyingi zaidi nimeshau bei niliona juzi, ongez bei tafadhali iwasaidie katika matibabu na mbeleni.

Labda kama mnakata kipande na kuacha kingine, matibabu huwa ningharama sana na utokea mtu ukianza kutibiwa.

Mola amsimamie mzee wako apone.

Asante sana kwa ushauri, kulingana na hali ilipofikia tumeona tuuze hekari moja haraka, ibakie nyingine, maana hali ya sasa hivi ukiweka bei kubwa sana unaweza usipate mtu huku hali ya mzee ikiendelea kudorora
 
Kujua uhakika wa uwanja ni kuwafanya majirani wa pande NNE za uwanja au Shamba ndo mashahidi na hakikisha wana nyumba au makazi ya kudumu wakigoma jua hilo ni fafafa utalizwa
Kuhusu hilo wala halina tabu, hata wakitaka wazunguke kwa majirani au mtaa wote, biashara ipo wazi kabisa.
 
Hiyo ni Madale karibu na kwa Mzee Kawawa...
ila kuhusu ukubwa wa eneo na bei yake ni km Ardhi na Mbingu..
Angalizo..
Wanunuzi wa hilo eneo wawe zaidi ya makini...
 
Back
Top Bottom