Baba yangu anashinikiza mama aondoke nyumbani, kisa kuhudhuria vikao vya chama

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,930
Habarini ndugu zangu poleni na majukumu,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 38, nina elimu level ya degree. Yapata miezi 6 sasa siongeai kabisa na baba yangu kisa tu alinifukuza nyumbani nilipokuwa nakaa (nadhani nilishaeleza hapo nyumba kwenye nyuzi zangu) labda nikumbushie kidogo, mimi ni kada mtiifu wa Chama cha Mapinduzi, nilijaribu kumshawishi baba ajiunge na chama na apigie kura Chama cha Mapinduzi kipindi kile cha uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hiyo ilikuja kuibua mtafaruku mkubwa sana kati yangu mimi na baba yangu na kupelekea kunitaka niondoke nyumbani kama najiusisha na mambo ya siasa, tulipelekana mpaka kwenye ofisi ya kata maana sikustahili kuondoka nyumbani wakati pale ni kwetu na mimi ni mtoto wake.

Sasa baada ya mzee kutokunielewa mimi, mama yangu alinielewa vizuri kabisa na alikuwa ni mhudhuriaji mkubwa sana wa vikao vya chama, juzi mama alinipigia simu usiku akaniambia baba amebadilika amekuwa ni mtu wa matusi na kelele nyingi akirudi, anamuambia mama kwenye nyumba yake hataki kabisa watu waojiusisha na mambo ya siasa hususani mambo ya Chama cha Mapinduzi, mama alisema Jumapili walikuwa na kikao cha chama cha shina, aliporudi nyumbani jioni mzee alimtukana matusi mazito sana na kumtaka aondoke mara moja pale nyumbani kama anajishughulisha na mambo ya CCM.

Nimemshauri mama kama vipi aende mahakamani adai talaka ili wagawane mali ili mama atafute sehemu yake ya kukaa na mimi niwe karibu nae maana kwa sasa baba alishanifukuza nyumbani sina pa kukaa nakaa kwa rafiki yangu tu huku Buguruni,

Baba yangu amekuwa na tabia za ajabu sana yani huyu mzee.

Naombeni ushauri wenu wakuu, ili nimshauri mama ikiwezekana kwenye mali apate sehemu kubwa ya mali maana huyu baba ni mnyanyasaji sana.

pia kama kuna mtu ana kazi naomba anisaidie ndugu zangu nimesomea marketing degree, maana nahishi maisha magumu mnooo na baba alinifukuza nyumbani kisa mimi mpenzi wa Chama cha Mapinduzi.
 
Mimi nina miaka 37 lakini siyo kijana. Mwenye tatizo ni wewe. Kwa bahati mbaya haulioni. Una miaka 38 wala hauoni kuwa ni mzee. Your father sets the rules nyumbani kwake. Kama haukubaliani naye, ondoka na ukawe na sehemu yako so that you set your own rules. Mzee wako ana akili sana. Angalau anajua dhuluma ambayo CCM imekuwa ikifanya. Hata haya mambo ya kufungia vyombo vya habari wewe bado haujayaelewa tu? Matoto mengine kama ungeonyeshwa mapema, unalitolea bafuni inaenda kwenye tanki la maji machafu kabisa.
mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 38
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom