Baba yake Joyce Kiria afariki dunia

Baba yake Joyce Kiria afariki dunia

Kila kitu kina mwanzo na mwisho,na dunia ni mapito,pia hakuna barabara isiyokuwa na kona,na kifo chako wewe ndiyo mwisho wako wa dunia kwani dunia haina mwisho ila binadamu tuna mwanzo na mwisho......kikubwa ni kukubaliana na kila linatokea ndani ya kipindi hiki kigumu kwa bi joyce kiria haya ni zaidi ya mateso kwake na mungu alivyo na makusudi leo anakuliza na kesho anakuchekesha kwa njia zake mwenye anazozijua,tufarijiane na tupeane moyo tunapokumbwa na matatizo kwani haya machungu na matamu tumeumbiwa mimi na ww na sio kunatoleana maneno ya kashifa na dharau kwa marehemu wetu kwani hata kifo ni jirani tunaetembea nae mda wote na mara nyingi anatutunzia siri na kutuvumilia kwa mengi ila tusivyokuwa na haya tuna mdhihaki kwa matusi yetu ya ucdm or uccm..

Pole sana da joy na mungu akutie nguvu zaidi ili umalize msiba wa mzee kwa amani kisha urejee kwenye maombi yakumpigania hubby wako bwana henry kilewo...rip mzee kiria
 
RIP Baba mkwe. Umetangulia mbele ya haki ukituacha tukiipambania haki. Hakika tutashinda
 
Pole sana dada Joyce, mungu aiweke mahali pema roho ya baba Mzee Kiria.
Be Strong babe!!
 
Pole Sana Joyce, God will see you through all these trials. Keep the Faith
 
kila kitu hulipwa hapahapa duniani,hayo ni malipo ya tindikali yaliyomuhusisha mumeo,tegemea mabaya zaidi
 
Dah! pole sana Joyce. mtu wako wa karibu sana yuko remand, Mwenyezi Mungu pekee ndiye wa kukutia nguvu.
 
daa ..pole sana.
Mungu akujalie wepesi katika magumu haya unayopitia.
 
Pole sana da Joyce, Mungu mwenye kufariji ninayemtumikia awafariji, awafute machozi na kuwatia nguvu nyote ktk kipindi chote cha msiba wa baba yetu mpendwa..... THE LORD GAVE AND THE LORD HAS TAKEN AWAY, MAY HIS NAME BE BLESSED...... JOB 1:21b
 
JUL102013





BABA MZAZI WA JOYCE KIRIA .. Michael Francis Iwambo Kiria wa kibosho dakau nganyeni amefariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi. Kesho ni safari ya kuelekea moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Pole sana mtangazaji wangu mahiri kwa hizi double misfortune! Mungu akupe nguvu ya uvumilivu!
 
JUL102013



BABA MZAZI WA JOYCE KIRIA .. Michael Francis Iwambo Kiria wa kibosho dakau nganyeni amefariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi. Kesho ni safari ya kuelekea moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.

What a difficult time it is for Joyce!! Pole sana Joyce, makamanda tunafahamu huu ni wakati mgumu sana kwako tukizingatia kwamba kwa sasa pia na Mumeo anakabiliana na ukandamizaji wa dola, take heart my sister kwamba hizo ndio changamoto za maisha; wala sio wewetu! kaza moyo dada, usikate tamaa; muombe Mungu bila kuchoka, nina hakika utavuka; Mwenyezi Mungu atakufuta machozi na haya yote yatakuwa historia.
Tuko pamoja sana; Pumzika kwa amani Mzee wetu Kiria

 
...
Kwa Jina la Baba,
na la Mwana,
na la Roho Mtakatifu.
... Amina
 
Pole sana Joyce, Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu ulichonacho
RIP mzee Kiria
 
Maisha yana misukosuko mingi na mingine haisubiriani bali inaweza kuja kwa pamoja. Only ukiwa mvumilivu na subira na huku ukimtegemea Mungu ndiyo tu silaha ya kukuwezesha kuvuka na ku make difference. Jipe Moyo mkuu utavuka dada Joyce.
 
Back
Top Bottom