BABA MZAZI WA JOYCE KIRIA .. Michael Francis Iwambo Kiria wa kibosho dakau nganyeni amefariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi. Kesho ni safari ya kuelekea moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.
pole sn joyce kwa kufiwa na baba yako! hiyo ni kazi ya Mungu. umo ktk mtihani mkubwa kufiwa na mzazi huku mumeo akiwa rumande. kaza moyo! ni mitihani ambayo huwakuta binadamu, wewe ukiwa mmoja wao
Ni majaribu ya duniani, Kaza moyo dada yetu na Mungu awape nguvu katika wakati huu Mungu.
Roho ya Marehemu ipate rehema kwa Mungu na Apumzike kwa Amani. Amina
MUNGU ampe nguvu dada yetu mpiganaji aweze kuhimili mikiki mikiki hii inayomkumba pia Mungu ampe pumziko la milele Baba yetu mzee Kiria,Amen. Unapokaribia kupambazuka majaribu huongezeka na ukishinda hapo kumekucha; be strong mafisadi wasije wakapenyeza rupia zao wapuuzi sana waalaaniwe
pole sana dada ila tambua mungu hajakuacha ukiona machungu yanazidi jua neema imekaribia na dhahabu hupitishwa kwenye moto ili ingae zaidi
ucjal haya yote yatapita na utaucmulia ukuu wa Mungu
Nilipata kusikia Waswahili wakisema Hakuna Msiba Usiokuwa na Mwenzie! Sijahakikisha kuwa hili ndilo linalompata dada yetu Joyce, lakini linaendana.
Kaza roho Joyce na jiandae kwa lolote! Nawakumbuka wanao siku ile wakisema "baba yetu yuko? inasikitisha"
Pumzika kwa amani mzee Kiria.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.