KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,766
- 3,018
Allah uwahifadhi waja wake.Bila shaka atakuwa mahali salama.King...
Nimeona baada ya Sesten kuweka ushahidi ule wa yanayofanyika na watendaji wa serikali dhidi ya Waislam ukumbi umekuwa kimya sana.
Nimerusha ule ushahidi wake na umesomwa kwa kupasiana na umewafikia watu wengi.
Hili sikutegemea.
Nimehamasika na nimeingia Maktaba kutafuta yale ambayo yanafanana na aliyotueleza Sesten.
Hebu someni kisa kingine hicho hapo chini:
View attachment 2105736
Mwalimu Athmani Khalfan Mrindoko Mwalimu wa Shule ya Msingi
Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko Mwalimu wa Shule ya Msingi Lwande Handeni Kosa Lake Kusomesha Wanafunzi Qur'an na Kukataa Kuchakachua Mitihani
Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Lwande moja ya vijiji ambavyo mwaka wa 2013 vilivyoshambuliwa kwa tuhuma za ugaidi.
Mwalimu Athmani alikuwa mwalimu mwajiriwa na serikali kusomesha masomo ya kisekula lakini kwa mapenzi yake katika Uislam kwa kuwa walimu wa somo la dini ya Kiislam Shule za Msingi hakuna yeye alijitolea kuwasomesha wanafunzi hawa dini ya Kiislam na kuwatungia mitihani.
Kisa chake ni kisa cha kusikititisha na kuhuzunisha.
Siku za nyuma Mwalimu Athmani alifatwa na walimu wenzake akaelezwa kuwa imetoka amri juu kuwa walimu washirikiane kuwafaulisha watoto darasa la saba kwa kuwakokotolea wanafunzi majibu ya mtihani wa mwisho wa darasa la saba ili kunyanyua ufaulu wa shule na hatimaye wilaya.
Mwalimu Athmani akakataa hili kwa misingi ya Uislam kuwa hicho kitendo ni ghushi yaani udanganyifu.
Akawaeleza kuwa imani ya dini yake inakataza mambo kama hayo.
Udanganyifu huu ukakwama na sababu ikawa ni yeye Mwalimu Athmani.
Hapa ndipo zilipoanza chuki dhidi yake.
Sasa lilipotokea sakata la Lwande askari waliovamia kijiji kwa madai ya kupambana na Al Shabab Mwalimu Athmani akakamatwa, kupigwa na kufunguliwa kesi ya kujeruhi Mahakama ya Handeni.
Mwalimu Athmani sasa hivi ni masikini.
Alipoachiwa gerezani kwa dhamana alikuta nyumba yake imevunjwa na vitu vyake vyote vimeibiwa.
Huyu ndiye ''gaidi'' anaesemekana alikuwa akishirikiana na Al Shabab.
Hapakuwa na ushahidi wa ugaidi hivyo akaachiwa na kazi akaachishwa.
Mwalimu muadilifu anaesomesha watoto kitabu cha Allah na kuwafunza maadili mema kwa mfano, Mwalimu Athmani Khalfan Mrindoko akazuliwa kuwa ni ''Al Shabab,'' bila ya ushahidi.
Haya ni machache.
Yapo mengi katika dhulma hii ya kumfanya mtu akabubujikwa na machozi.
Sasa imepita karibu miaka 9 sijapata taarifa za Mwalimu Mrindoko.