Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Waziri...
Sijakuelewa.

Mimi ni nani hapa niko nimejitambulisha kwa jina langu halisi na picha na videos zangu naweka.

Watu wanakifahamu kwa majina, sura na sauti.

Niko JF kwa zaidi ya miaka 10 na nimefikia hadi kupewa tuzo kwa michango yangu.

Wewe nani mwenzangu?[/ hadhira inataka kujua kipi kinachokusukuma kuandika hizi mada zako?na pia ni kwanini maandiko yako yote yanamnasaba wa upande mmoja wa Imani je wewe ni mwanaharakati wa haki na usawa katika kutaka kuvumbua ukweli uliofichwa ili kuleta usawa katika haki tenganifu au wewe ni mzalendo ambaye unahitaji uwepo uthamini wa historia na kuenzi sanjali na kutambulika kwa juhudi za kweli za wapigania uhuru au wewe ni mdini ambaye upo kwaajili ya kutetea maslah ya dini yako ambayo unahisi yanakandamizwa .
 
Hahahahaha mzee unamajibu ya kifyosi tunasema watu wa pangani,but hadhira inataka kujua kipi kinachokusukuma kuandika hizi mada zako?na pia ni kwanini maandiko yako yote yanamnasaba wa upande mmoja wa Imani je wewe ni mwanaharakati wa haki na usawa katika kutaka kuvumbua ukweli uliofichwa ili kuleta usawa katika haki tenganifu au wewe ni mzalendo ambaye unahitaji uwepo uthamini wa historia na kuenzi sanjali na kutambulika kwa juhudi za kweli za wapigania uhuru au wewe ni mdini ambaye upo kwaajili ya kutetea maslah ya dini yako ambayo unahisi yanakandamizwa .
Waziri...
Hapa sitaingia katika mjadala na wewe hadi kwanza tukubaliane kuwa tunajadili kwa adabu na heshima.

Kwa ajili hii basi nakuomba uondoe hiyo kejeli katika kicheko chako na urejee kwa heshima.

Ukishafanya hivyo In Shaa Allah nitatoa mchango wangu.

Nimeweka hapo juu ujuzi wangu mdogo ili tufahamiane lakini bahati mbaya hukuweza kutambua au umekupita.

Tafadhali fanya rejea.
 
Waziri...
Hapa sitaingia katika mjadala na wewe hadi kwanza tukubaliane kuwa tunajadili kwa adabu na heshima.

Kwa ajili hii basi nakuomba uondoe hiyo kejeli katika kicheko chako na urejee kwa heshima.

Ukishafanya hivyo In Shaa Allah nitatoa mchango wangu.

Nimeweka hapo juu ujuzi wangu mdogo ili tufahamiane lakini bahati mbaya hukuweza kutambua au umekupita.

Tafadhali fanya rejea.
Sawa mzee wangu
 


Ukishasikiliza mazungumzo ya Mwalimu Nyerere katika hiyo video hapo juu sasa soma Hotuba yake aliyotoa Bungeni tarehe 10 Desemba, wakati Tanganyika inakua jamuhuri mwaka wa 1962.

Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislam na Wakristo.

Kwa nini ilikuwa lazima Mwalimu awataje Waislam katika hotuba ile?

Sababu ni jinsi Waislam walivyokuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukoloni na namna walivyounda TANU wakamchagua kama kiongozi na kuumuunga mkono toka siku alipochukua uongozi wa TAA katika uchaguzi wa tarehe 17 April, 1953 Ukumbi wa Arnautoglo alipogombea nafasi ya urais dhidi ya Abdul Sykes aliyekuwa Act. President na Secretary wa TAA.

Kwa bahati mbaya sana hii ni historia ambayo ilifunikwa na hakuna yeyote aliyekuwa anaijua hadi nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes na kuchapwa mwaka wa 1998.

Mwalimu anasema katika hotuba yake ya Jamhuri ndani ya Bunge la Tanganyika:

''Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa.''

Hii ilikuwa kauli ya serikali ya kudhihirisha nia yake njema ya kupigania haki na usawa kwa raia wote wa Tanganyika.

Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini na kuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwa serikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebisha hali hiyo.

Tarehe 5 Novemba, 1985 wakati Mwalimu anastaafu urais, Mwalimu aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam.

Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo.

Katika hotuba hii Nyerere kwa mar ya kwanza hadharani alimtaja Abdul Sykes.

Mwalimu alimtaja na mdogo wake Abdul, Abbas Sykes na Dossa Aziz.

Wazee hawa aliokuwa anawahutubia wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono wakati wa kudai uhuru.

Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru.

Nyerere alisema neno zito sana kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:

''Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo.

Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho.

Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo.

Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.''

Swali linalokuja hapa ni kuwa ikiwa Mwalimu alisharekebisha upogo huu baina ya Waislam na Wakristo haya malalamiko ya leo kutoka kwa Waislam kuwa wanabaguliwa tunauelezaje?

Waislam hawasemi kweli?

Mgawano wa madaraka ndani ya serikali ya Tanzania baina ya Waislam na Wakristo ni 20:80.

Tumefikaje katika hali hii?

Ni muhimu sana mtu anapotaka kujadili tatizo hili la udini muhimu akaangalia historia hii kwanza kama nilivyoieleza hapo juu kwa kusikiliza mazungumza ya Mwalimu kuhusu udini na kusoma Hotuba yake ya Jamhuri ndani ya Bunge la Tanganyika mwaka wa 1962.

Tatizo hili la udini nimelijadili kwa kirefu sana katika kitabu cha Abdul Sykes.

Tatizo hili si tatizo la kupuuzwa na wala si la leo.

Tatizo hili lilianza mwaka wa 1958 na likasababisha ugomvi mkubwa baina ya Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir akafukuzwa TANU.

View attachment 2096477
View attachment 2096478
Kauli za mwalimu zilikuwa ktk maneno na ukija ktk vitendo unakuta tofauti, so alikuwa mfasaha na mlaghai sana, ukichunguza vitendo utakuta ni tofauti na alichoongea ndo maana aliasisi taifa lenye utamaduni wa kifisadi.
 
Tatizo letu kama watanzania tuna adui mmoja na ndo ametengeneza maadui wenzake anatuchapa tusistawi.Adui mkubwa ni CCM.Huyu ametengeneza ubaguzi,amestawisha ujinga ,umaskini na chuki za kikabila na kidini.Wanaoitwa Sukuma gang,ni kikundi cha watanzania wenzetu,Wana dini kama zetu lakini siyo wenzetu.Tunapotofautiana kwa vyovyote adui yeye hufurahi.Mzee Ndugayi alikuwa mtu na nguvu nyingi lakini adui alipomchoka akamtupa pembeni.Tuunganishe nguvu tunaweza kushinda adui.
Wazanzibar hutuona wabara kuwa chanzo cha matatizo yao lakini kumbe wao wanapata hayo matatizo kutoka watu wale wale wanaowatesa wabara.Adui yetu kama watanzania nimemtaja hapo juu.
 
Unaweza kumlaumu Mwalimu kwa mengi na mengine yote ila sio kwa Udini na Ukabila. Eneo hilo alifaulu kwa asilimia 100.
 
Yoda,
Kuna mambo mimi huona haya kuandika hivi sasa.
Sifa ya kutokuwa na udini na ukabila Tanzania sio tu inazungunzwa huku ndani, bali hata majirani zetu wa karibu na walio mbali na sisi wanafahamu hivyo.
 
Yoda,
Kuna mambo mimi huona haya kuandika hivi sasa.

Sifa ya kutokuwa na udini na ukabila Tanzania sio tu inazungunzwa huku ndani, bali hata majirani zetu wa karibu na walio mbali na sisi wanafahamu hivyo.
Yoda,
Kama nilivyosema kuna mambo mimi nashindwa leo kuyajadili.

Hata hivyo katika kitabu cha Abdul Sykes sehemu ya mwisho (Part Three) inaitwa ''Conspiracy Against Islam.''

Kipate kitabu hiko usome.
Muhimu sana.

Usikimbilie kurejea kwangu kwa mjadala wa swali hili hadi umesoma.
Soma utaongeza maarifa kuhusu ukweli wa tatizo hilo katika nchi yetu.
 
Tangawizi,
Soma kwa utulivu utaelewa kuwa ninachozungumza ni kuwa kuna tatizo serikali wanalikwepa toka enzi ya Mwalimu.

Hakuna popote nilipozungumza kuhusu, "special status," kwa Waislam.

Unadhani hii 20:80 ni sawa?

Ukishakuwa na hali hii tayari serikali yenyewe ishawagawa raia wake katika matabaka makubwa mawili.
Naona mambo ni MOTO. Kimya kimya
 

Attachments

  • IMG_20230227_171330.jpg
    IMG_20230227_171330.jpg
    106 KB · Views: 14
Tangawizi,
Soma kwa utulivu utaelewa kuwa ninachozungumza ni kuwa kuna tatizo serikali wanalikwepa toka enzi ya Mwalimu.

Hakuna popote nilipozungumza kuhusu, "special status," kwa Waislam.

Unadhani hii 20:80 ni sawa?

Ukishakuwa na hali hii tayari serikali yenyewe ishawagawa raia wake katika matabaka makubwa mawili.
Nenda kawafaulishe waislamu kwa bao la mkono huko Necta
 
Pep,
Mwalimu angeacha misingi mizuri leo tusingejikuta kwanza tunaandika upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Pili tusingekuwa na mjadala huu uliotukutanisha hapa.
Ulitakiwa kuwa vipi huo msingi katika hoja hii?
 
Wakristu wao wanapambania haki ya Kabila, matambiko, Uchief, utemi wenzao Waislamu wanapigania Uislamu.
Mmeshapoteza hii game, soon or later mtajua, kwa maana hata wealth hamna pia, wealthy people Tanzania mnawajua !
2024 je bado unaamini comment yako ina afya kwa Taifa?

Ungependa iwe vipi, dola ya kiislamu,ya kikristo au tubaki kama secular(taifa lisiwe na dini)?
Na je wa dini tofauti waishi vipi?.

Hii comment yako ya 2022 imekaa kama unaamini katika machafuko na probably upande wako utashinda.

My friend, ni huzuni kuwa na fikra za aina hii,tukifika huko taifa halitatulia,watu watalia na kuzikana kila siku.

Mwisho watanzania wengi sio wajinga, ndio maana hata viongozi wenye dini zao waliposhika hatamu hawajajaribu suala kama hilo kabisa, hata Kikwete alikwepa issue ya mahakama ya kadhi.

Bora mambo yaende taratibu tu na sio kulazimisha,mfano kuongezeka population,kujenga misikiti na kufundisha watu dini yako unayotaka iwe dini ya taifa.
 
Pep,
Unayosema huenda ni kweli kabisa kuwa hujabaguliwa na wewe hujabagua mtu.

Muulize Mmarekani Mweupe kama yeye keshabaguliwa atakwambia bado sijabaguliwa na pengine atakuambia yeye hajabagua mtu.

Sasa nakuuliza je wewe uko katika kundi la wanaobaguliwa na hukubaguliwa?
Mbona unakwenda mbali sana Nigeria kutafuta mifano ya ubaguzi?

Vipi hali ya hapa ulikoishi kwa miaka 30?
Hali ikoje?

Nakusihi kwa ajili ya heshima yake tumwache Mwalimu tusimwingize katika huu mjadala wa mimi na wewe.

Huenda ikawa wewe hujui uhusiano wa wazee wangu na Mwalimu na historia yao wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wazee wangu ndiyo waliompokea Mwalimu Dar es Salaam 1952 na kuunda TANU 1954 kutoka African Association waliyoasisi 1929.

Historia hii nimeaindika, iko na inasomwa.

Naijua historia ya Mwalimu vizuri sana kiasi mimi ni mmoja wa watu waliohojiwa wakati inaandikwa historia ya Julius Nyerere na jopo la waandishi wa historia hii waliisifia Maktaba yangu kuwa moja ya maktaba kubwa tatu zilizo na taarifa za Mwalimu; maktaba ya Salim Ahmed Salim, Brigadier General Hashim Mbita na ya Mohamed Said.
View attachment 2096659


View attachment 2096546
Kulia ni Prof. Issa Shivji, Prof. Said Yahya Othman na Dr.
Ng'waza Kamata walipokuja kunihoji kuhusu Mwalimu.
Ugomvi wako na Mwl Nyerere ni dhidi ya wazee wako tu sio watanganyika au Watanzania!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom