Baba niko busy, nikipata nafasi nitakuja

Baba niko busy, nikipata nafasi nitakuja

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,353
Shost alikuwa na mapenzi kwa boy friend wake, alikuwa anakwenda for a week, wakati huo ni mwanafunzi. Majibu yalipotoka amepiga chini, basi aliamua kuhamia kwa jamaa mazima. Walianza kuishi kama mume na mke na kufanikiwa kupata watoto wawili.

Jamaa ni mchacharikaji hasa, anapigana mpaka nchi jirani kwenye biashara. Amejenga nyumba ya kawaida, kuna usafiri wa kupeleka watoto shule, mama ana ka usafiri kake. Shost yangu hafanyi kazi, ni mama wa nyumbani.

Sasa hivi hawana maelewano kabisa na mwanaume huyu. Yaani yule mwanaume anakuja pale nyumbani kuangalia watoto wake tu, anaishi na shost kama yuko na shemeji yake. Zaidi ya salamu hakuna hata kiss, hii hali imekua inamfustruate shost yangu tangu January mwaka huu. Kumbuka hajaolewa wala kutolewa mahari. Sasa nilimpa ushauri aende kwao kidogo ampe jamaa nafasi ya kumiss.

Kilichotokea, shost alikwenda kwao, jamaa wala hajapiga hata simu, sasa kinachomuuma aliacha watoto akitegemea baada tu ya siku mbili atapigiwa simu arudi, kimya. Baba yake ameamua kumpigia simu baba watoto, anamuuliza unafahamu kuwa mwenzio yuko hapa, akasema anafahamu ndio maana hakumtafuta. Baba akauliza tena hujiulizi kwanini amekuja bila kukuaga? Alijibu, baba niko busy nikipata nafasi tutaongea vizuri.
 
1465626355347.jpg
 
Safi. Kwani mwanaume ana liability yoyote kwa huyo dada?? Kamuoa, hapana!! Ana mpango wa kumuoa, hapana. Atulie
Hapo mwanaume pengine kapata mwanamke wa kuoa.

Kibaya zaidi shost ananilaumu kwa aidea yangu ya kuondoka, ananiambia ni aibu sasa akirudi itaonyesha kabisa yeye ndie mwenye shida ni kheri asingeondoka.
 
wewe uliye mshauri, ulimshauri by experience yako au? klm wewe ulifantwa mama ilikuwa bahati ila wengi hatufanyagi ujinga uo, kumbuka kuna vituo kibao vinalea watoto wa wnaume walio hachana na wake zao, huyo jmaa ameleta watoto wake wawili hapa kituoni kwetu na sisi tunalea kila siku anaacha matumizi 20000, ila tumeingia mkataba na kituo wa miezi miwli maana amesema anafunga ndoa mwezi ujao kama rafiki yako atakuwa hajarejea ajue imekula kwake.
 
Mwanaume msimamo bhana, mwenzako anapigana na maisha mpate kusomesha na kula mwanamke unaanzisha libeneke, ahya sasa kaa hukohuko kwenu wala usirudi
 
Mimi ningerudi tu nilee wanangu kama kuondoka aondoke yeye, haya mambo yakusikiliza au kuomba ushauri kwa marafiki yanajutishaga sana, maamuzi mazuri ni ya wewe na ubongo wako tu mara 100 umuombe ushauri Mama yako.
 
Mwambie arudi tu hapo alee wanae . mambo ya ndoa kama yapo yatakuja tu polepole aiskazimishe... Wanaume wenyewe ukiwaonyesha unashida ya ndoa watakunyanyasa mpaka ukome .. Muhimu muonyeshe unashida na pesa zake basi ajiongeze si kujpa stress za ndoa.. Halafu kuzalishwa haina maana lazima uolewe jamani .. Hawa viumbe hawa waonage wakiwa wamevaa nguo tu basi
 
Hakuna tatizo hapo.na huyo shost alikubali vp kutundikwa watoto wawili bila ndoa

Alijua watoto wakishapatikana ndio mwanzo wa familia kinachofuatia wazee wanatafutwa, mahari inalipwa, ndoa inabarikiwa kanisani. Ilikuwa Technic know how.
 
Mimi ningerudi tu nilee wanangu kama kuondoka aondoke yeye, haya mambo yakusikiliza au kuomba ushauri kwa marafiki yanajutishaga sana, maamuzi mazuri ni ya wewe na ubongo wako tu mara 100 umuombe ushauri Mama yako.
Kweli kabisa sababu rafiki hamjui mwenzio vilivyo wewe muhusika ndiyo unamjua vizuri .
 
Mwambie arudi tu hapo alee wanae . mambo ya ndoa kama yapo yatakuja tu polepole aiskazimishe... Wanaume wenyewe ukiwaonyesha unashida ya ndoa watakunyanyasa mpaka ukome .. Muhimu muonyeshe unashida na pesa zake basi ajiongeze si kujpa stress za ndoa.. Halafu kuzalishwa haina maana lazima uolewe jamani .. Hawa viumbe hawa waonage wakiwa wamevaa nguo tu basi

Kitu kingine kinamuuma ni aibu aliyomwingiza baba yake, yani jamaa ameonyesha dharau kwa baba. Nimeongea nae anasema baba pia hamshauri kurudi kwa mwanaume mwenye dharau hizo.
 
Mimi ningerudi tu nilee wanangu kama kuondoka aondoke yeye, haya mambo yakusikiliza au kuomba ushauri kwa marafiki yanajutishaga sana, maamuzi mazuri ni ya wewe na ubongo wako tu mara 100 umuombe ushauri Mama yako.
Sababu iliyonifanya kutoa ushauri huu ni kwakua shost anataka kuwa mke halali, niliona yeye kwenda nyumbani itasaidia kuleta communication kati ya jamaa na wazazi.
 
Wabeijing wengine wapo wapi? Naona pamependeza hapa
 
Mnaishi na mwenzako, msome vizuri huyo mtu wako yukoje. Kama unataka kuondoka ondoka kweli, lakini kutishia unaondoka teh sio kwa hawa wanaume wa mwendokasi. Utarudi mwenyewe bila kuitwa, tena kwa aibu kijuso kidogooo, afu unamkuta mwenzio hana hata habari

Mwambie shoga ako arudi alee watoto wake, ndo ashalikoroga hivyo. Kingine kama ataamua kurudi shule au kutafuta kazi/biashara itakuwa kheri zaidi. Achakarike tu na maisha yake na wanawe, me sioni dalili ya ndoa hapo kwa sasa hivi honestly.
 
Kama hawajagombana yeye kilimkimbiza nini sasa, yaani uache watoto eti unalazimisha ndoa, yaani Sie wanawake kuna muda akili zinahama jamani. Hilo ni suala la yeye na mzazi mwenzie kuelewana tu, kama ndoa ipo tu hata uwe na watoto sita na anaweza kuwa na hiyo ndoa wala asiifurahie wangapi wapo kwenye ndoa na wanaishi kama maadui bwana aaaaah, tena amshukuru Mungu analishwa, watoto wanasoma na usafiri wa kwenda sokoni anao. Mwambie arudi haraka akawalee watoto ni upepo tu umepita hapo mumewe mtarajiwa atarudi kwenye hali yake ya kawaida.
 
Akili za kuambiwa lazima uchanganye na zako..Kama jamaa alikuwa anatafuta sababu ya kumpiga chini hapo anafurahia mno tena na hiyo simu kutoka kwa Baba mkwe ni uthibitisho tosha kuwa mwanamke kashafika kwao..Hakuna cha kumfuata wala nini nikupambana na watoto tu kama hilo ndilo lilikuwa lengo la huyo jamaa...Sumu haijaribiwi kwa kuonja..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom