Ni siku niliyokutana na mtu maarufu sana katika jukwaa hili pendwa la MMU Jamiiforums. Sikufahamu umuhimu wa siku hiyo kwani nilienda pale kwa mualiko wa dada yangu gfsonwin. Nakumbuka sana kina cacico, Asprin, Madame B, amu, Jiwe Linaloishi, Nicas Mtei, Paloma, Kaizer walikuwepo.
Watu walikuwa na nyuso za furaha na kuchangamka. Baadaye nilikuja kugundua sio wao bali ni effect ya Contessa gin, strawberry lips na govinder kumar.
Mdau huyu naye kwa kutumia kisingizio hicho akaaga kwa mkewe kuwa atakuwa na marafiki zake kwa muda tu then atarudi nyumbani kujumuika na familia yake. Yaliyotokea ni mengi kuyaelezea. Mama Ngina karibu aue mtu baada ya mumewe kurudi nyumbani na shati lililochafuka lipstick.
It was a perfect excuse it was his BIRTHDAY! (Ingawa inasemekana ukweli wa mambo anaufahamu Paloma)
Na leo ni mwaka mmoja umepita tangu siku ile...nikutakie tena heri na fanaka katika mwaka huu mwingine uliiongezewa kuishi.
Nionesheni kwanza ndyofu zangu kabla sijasema lolote.. BTW Happy birthday mkuu... Keep on using that rubber sheath (Ha ha haaa, hapa usinipige ngumi) Be blessed with a long life .. Pamoja