Baba na mwana ...! Kweli wakati si milele

!
20210821_192136.jpg
 
Ilitokea baba akampenda sana mtoto wake wa kwanza ila akang'amua mtoto huyo mpendwa alikuwa na mbinu za kumchukua baba yake msukule. Alimfukuza nyumbani na kama watoto wanatolewa zawadi anatafuta mtu wa kumchukuwa ahame kabisa nyumbani kwake.
 
Ilitokea baba akampenda sana mtoto wake wa kwanza ila akang'amua mtoto huyo mpendwa alikuwa na mbinu za kumchukua baba yake msukule. Alimfukuza nyumbani na kama watoto wanatolewa zawadi anatafuta mtu wa kumchukuwa ahame kabisa nyumbani kwake.
Duh, mara nyingi watoto/vijana wanaopendwa sana na wazazi wao zaidi baba; huwa wanaharibu mambo. Hata sijajuaga ni kwa nini wajameni!
 
Kuna jambo limenitafakarisha sana...mahusiano ya baba na mtoto...Kwenye Biblia takatifu kuna simulizi nyingi zinazowahusu baba na mwana...hata Mungu mwenye enzi yote yote anamtaja Yesu Kristo kama mwanae mpendwa
Baba kama mzazi ana nafasi kubwa kiroho kwa mtoto kutokana na kizalia DNA ....baba ana uwezo wa kutoa laana na ikashika na pia ana uwezo wa kubariki na mtoto akabarikiwa

Kwenye dhana nzima ya baba na mwana kuna
Baba halisi
Baba halali
Baba wa kufikia
Baba wa hiari
Baba wa kurithi
Ni katika aina zote hizo za ma baba ....inaweza ikatokea tu kiasili kabisa baba akajikuta anampenda sana mmojawapo wa watoto wake wengi alionao...na sometimes sio lazima awe wa kumzaa yeye....yani mtoto wa kufikia anaweza kupendwa zaidi kuliko mtoto halisi

Mtoto mpendwa kwa baba anapogundua kuwa yeye ndio kipenzi cha dingi kuliko wengine...kwa akili za kitoto huanza kuringa na kufanya mambo ya kijinga mengi akiamini kuwa baba hawezi kumfanya kitu ....kuna wakati anaweza hata kuzusha jambo ama kumsingizia mtu kitu kwa baba, na baba bila kutafakari marambili akamchukulia hatua mtu huyo bila kuangalia uhalisia wa tuhuma zenyewe
Mtoto akiona hivyo huota mapembe na kuvimba kichwa...lakini waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...na ngoma ikivuma sana hupasuka.....!!!.ni katika kilele cha upendo wa baba kwa mtoto ndio jambo baya sana hutokea na baba akili kuanza kumrudi taratibu
Ewe mtoto ukishaona baba hatoki tena kwenda na wewe popote iwe bar, kwenye harusi ama mialiko yoyote...ukiona baba hakuiti tena chumbani kwake muongee...ukiona baba hakuiti tena akutume hata dukani...tambua tu kuwa sasa baba upendo umepungua na hakupendi tena kama zamani...utajipendekeza na kujifanya umejutia makosa yako lakini wewe sio wake tena....na akimpata mgeni wa kumpa zawadi anaweza kukugawa bure
Ila ukiona baba unampenda sana mtoto mmoja kuliko wengine bhac ujue hao wengine sio damu yako. DNA haiongopi abadan!
 
Back
Top Bottom