Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,610
ippmedia.com
WANANCHI wa kitongoji cha Mikoroshoni katika kata ya Jonad wilayani Kyela mkoani Mbeya, wamekumbwa na taharuki baada ya kumkuta, Girbati Sanga mkazi wa eneo hilo, akimbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kyela
Sanga anayejulikana kwa jina maarufu la Majungu, ni mfanyabiashara maarufu wa kuuza nyama choma na ndizi katika kitongoji cha Mikoroshoni.
Tonny Kojaki mkazi wa Mikoroshoni, alisema tukio hilo limewashangaza wengi kwa kuwa baada ya kusikia kilio cha mama mzazi wa mtoto huyo, walisogea eneo la tukio na kukuta baba wa mtoto huyo akitoka chumbani akiwa na taulo na baada ya kuingia ndani walimkuta mtoto tayari ameharibiwa.
Alisema siku ya tukio baba mzazi alimvizia mwanaye akitoka bafuni na kuamua kumbaka na kwamba walipomuuliza mtoto huyo alisema, alipotoka kuoga mtuhumiwa alimshika na kumziba mdomo kisha kumwingilia kinguvu.
Alisema licha ya mama yake kuingia chumbani humo na kupiga kelele, lakini alichelewa na kwamba alimkuta mtuhumiwa kishamaliza kufanya unyama huo.
''Mimi ni mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Ndandalo, huwa nakula nyama katika ofisi ya huyu mtuhumiwa, kuna maneno mengi yanasemwa kuwa anatembea na watoto wake kwa ajili ya ushirikina ili apate mali, najiuliza licha ya kuuza nyama nyingi za kuchoma na ndizi kila siku, lakini mbona haendelei,'' alisema.
Rameck Mbembela mkazi wa Ndandalo, alisema Majungu amewatia aibu kwa kutembea na mtoto wake, kwa kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kwa mtu huyo kutembea na watoto wake na kwamba kitendo cha kumbaka mtoto mdogo kimewasononesha na wanaomba serikali ichukue hatua kali dhidi yake.
Justin Silas ambaye ni Ofisa Ustawi wa Jamii, alikiri kutokea tukio hilo na kwamba alifuatilia vipimo hospitalini ambavyo vilionyesha mtoto huyo kuingiliwa kimwili.
Alisema baada ya kubainika hivyo, mtoto huyo alipewa dawa za kuzuia maambukizi ya magonjwa.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei, alikiri kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa alikamatwa na anatarajia kufikishwa mahakamani.
Sent using Jamii Forums mobile app