Baba mtoto kanitelekeza

Nimecheka kweli kweli. Bado hujafikia huko?

Kwakweli nyuzi zote zinazoandikwa za kulalamika kuhusu mapenzi me hua najua walengwa ni ambao wako in their 20's.. Nimeshangaa kuona mtu mzima naye anasumbuka nayo
Watu wazima wanaohangaika na hizi ishu ni wengi mno ila wanaona aibu na sometimes wanaamua kujiua na kuua watoto sababu wakijitokeza kwenye Jamii badala ya kupata msaada watu wanaishia kuwakebehi. Ila wakisikia wamefanya madhara Kwa familia, watasema "Si angeongea!"
 
Habarini?

Ninaomba nieleweke kwamba mimi si mgeni, nimekua nikisoma mijadala mbalimbali lakini leo nami nimewiwa nilete kisa changu ambacho ninaamini kwa namna moja au nyingine kitawasaidia watu kadhaa.

Mimi mwanamke wa miaka 32, nimeajiriwa mahala Fulani. Kiukweli, nilikua kwenye mahusiano Kwa muda mrefu sana tangu nikiwa chuo hadi hivi majuzi. Hali ya mahusiano yetu yalikua ya kusuasua mno. Leo mko poa, kesho majanga hali ambavyo ilinikatisha tamaa sana. Ingawa jamaa alinitamkia ndoa wakati Fulani lakini binafsi kwa tabia za jamaa, sikuona hata kivuli endapo tungefunga ndoa.

Mwenzangu kwanza ni mnywaji sana wa pombe kiasi kwamba mara kadhaa ilimletea shida kwenye ajira yake na alisimamishwa mara nyingi sana. Mbali na hiyo, ni mtu ambaye bado hajui anataka nini. Leo mtapanga hiki, kesho mtagombana muanze upya so mnakua mara kadhaa hakuna mtakachokamilisha.

Mara nyingine anadai anataka kuoa mtu wa kabila lake, mara anaweza kuanzisha mahusiano na vitoto vya chuo ingawa yeye ana 36 years.

Kwa mahusiano yetu ya miaka Zaidi ya nane, hatukuwai kujaliwa mtoto ingawa jamaa alinitamkia mara moja akisema ananiacha sababu simpi mtoto then baadaye akaomba msamaha na maisha yakaendelea.

Mungu si Athuman! Mwezi wa tano nilijigundua ni mjamzito. Nikamshirikisha mwenzangu ambaye hakuwa na furaha nayo kabisa. Akanishauri sana tutoe tukizingatia bado tunajitafuta and blablabla.

Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.

Kweli, jamaa alihangaika sana kunishawishi kutoa ili tuendeleze mahusiano (ambayo hayana dura) nikaamua kuweka msimamo wangu kwamba akijisikia kuondoka, aondoke ila mtoto kama lolote likitokea basi liwe limepangwa na Mungu ila sipo yeye. Aliamua kuondoka na wala sikujushughulisha naye kabisa.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia safari yangu ya ujauzito hadi sasa, hakuna kilichonisumbua. Kiukweli, nina furaha na amani zote, sielewi ni kwa nini. Nimejikuta natamani kuwaambia wanawake wenzangu, wasikubali kuendeshwa na wanaume wa namna hii ili kuendeleza mahusiano.

Focus na unachokichagua kwani hata ningetoa, sio kweli kwamba mahusiano yangeboreka, tena yangekua mabaya zaidi. Ninamshukuru sana na niwatakie jioni njema.
Pole. Mwanamke ukishaona mwanaume aliyekupa ujauzito anakuambia utoe basi hiyo ni green light kimbia kufa kupona.

Hakuna mwanaume anayeweza kumpa mwanamke anayempenda ujauzito kisha akamuambia autoe.

NEVER!
 
Amekwambia toa mimba muda bado. Ukakataa. Sasa kakutelekeza kivipi wakati umeapa kwake liwalo na nalo liwe?!
Acha kulazimisha majukumu kwa mwanaume. Umejitakia mwenyewe kuwa single maza. Pambana na Hali yako...
Kwa hiyo ni sawa kumwaga damu sababu ya kulea? Na Hakuna sehemu niliyosema ninamtegemea. Sijui ni kwanini wengi mnaongelea abortion kama kuchinja kuku. Huwezi kukionea kiumbe kisicho na hatia huruma? Utembee na dhambi ya kumwaga damu hadi siku ya kifo? Ili iweje, aendelee kubaki na mimi then nikiwa naye napata faida gani kubwa? Kwa uzazi ulivyo changamoto hivi? Mbona kuna wababa wana huruma mno, wanabeba majukumu huku wanaamua kuwa Ni mtoto aliyetelekezwa. Na uzuri mtoto akiwa Hana mzazi, anasimamiwa na Mungu.
 
Watu wazima wanaohangaika na hizi ishu ni wengi mno ila wanaona aibu na sometimes wanaamua kujiua na kuua watoto sababu wakijitokeza kwenye Jamii badala ya kupata msaada watu wanaishia kuwakebehi. Ila wakisikia wamefanya madhara Kwa familia, watasema "Si angeongea!"
Kwakweli Bora umeongea, hiyo ya kujidhuru ndo mbaya zaidi
 
Imagine watu wameoana, wanawatoto Zaidi ya watatu, baba kaamua kuoa mtu mwingine kimyakimya na kutelekeza familia 😢 hiyo utafananisha na kukimbiwa na baba mtoto ambaye hamkuwa kwenye maagano? Wababa wengi wanateseka ila watasemea wapi!
Unaweza kukuta hata wazazi wetu wanateseka Ila ndo hivyo Tena hawana namna inabidi watunze heshima ya familia 😌😌
 
Back
Top Bottom