Baba mtoto kanitelekeza

Habarini?

Ninaomba nieleweke kwamba mimi si mgeni, nimekua nikisoma mijadala mbalimbali lakini leo nami nimewiwa nilete kisa changu ambacho ninaamini kwa namna moja au nyingine kitawasaidia watu kadhaa.

Mimi mwanamke wa miaka 32, nimeajiriwa mahala Fulani. Kiukweli, nilikua kwenye mahusiano Kwa muda mrefu sana tangu nikiwa chuo hadi hivi majuzi. Hali ya mahusiano yetu yalikua ya kusuasua mno. Leo mko poa, kesho majanga hali ambavyo ilinikatisha tamaa sana. Ingawa jamaa alinitamkia ndoa wakati Fulani lakini binafsi kwa tabia za jamaa, sikuona hata kivuli endapo tungefunga ndoa.

Mwenzangu kwanza ni mnywaji sana wa pombe kiasi kwamba mara kadhaa ilimletea shida kwenye ajira yake na alisimamishwa mara nyingi sana. Mbali na hiyo, ni mtu ambaye bado hajui anataka nini. Leo mtapanga hiki, kesho mtagombana muanze upya so mnakua mara kadhaa hakuna mtakachokamilisha.

Mara nyingine anadai anataka kuoa mtu wa kabila lake, mara anaweza kuanzisha mahusiano na vitoto vya chuo ingawa yeye ana 36 years.

Kwa mahusiano yetu ya miaka Zaidi ya nane, hatukuwai kujaliwa mtoto ingawa jamaa alinitamkia mara moja akisema ananiacha sababu simpi mtoto then baadaye akaomba msamaha na maisha yakaendelea.

Mungu si Athuman! Mwezi wa tano nilijigundua ni mjamzito. Nikamshirikisha mwenzangu ambaye hakuwa na furaha nayo kabisa. Akanishauri sana tutoe tukizingatia bado tunajitafuta and blablabla.

Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.

Kweli, jamaa alihangaika sana kunishawishi kutoa ili tuendeleze mahusiano (ambayo hayana dura) nikaamua kuweka msimamo wangu kwamba akijisikia kuondoka, aondoke ila mtoto kama lolote likitokea basi liwe limepangwa na Mungu ila sipo yeye. Aliamua kuondoka na wala sikujushughulisha naye kabisa.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia safari yangu ya ujauzito hadi sasa, hakuna kilichonisumbua. Kiukweli, nina furaha na amani zote, sielewi ni kwa nini. Nimejikuta natamani kuwaambia wanawake wenzangu, wasikubali kuendeshwa na wanaume wa namna hii ili kuendeleza mahusiano.

Focus na unachokichagua kwani hata ningetoa, sio kweli kwamba mahusiano yangeboreka, tena yangekua mabaya zaidi. Ninamshukuru sana na niwatakie jioni njema.
Mtoto Hana Baba
 
Ana uhakika ila ni muoga sana wa maisha. Ni kawaida yake kuwapa wanawake zake dawa za kuua watoto Kwa kisingizio kuwa hana maisha. Aliwahi kuwa na mtoto mmoja ambaye hajui ada wala chakula. Kiufupi ni mtu asiyependa majukumu. Yeye anachojua ni pombe.
Muache aende akaikologee zege.

CC Yombo msukuma
 
Umetumia akili sana kwenye hii comment
Single mothers mara nyingi wao ndo wazinguaji,hawawezi kutulia, inawezekana huo ulevi unatokana pia na wewe kumpa stress huyo jamaa.

Maisha ni uvumilivu hamna aliyekamilika, heri hata shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua.

By the way maamuzi ni yako mwanaume hawezi kubadilika tu na kufukuzia wanawake wengine bila kuwa kuna mapungufu aliona kwako au ameona we siyo mtu sahihi hata wa kuzaa naye ndo maana hatua ya mwanzo alikuambia itoe.
 
Pole sana miaka 8 si kitoto ni mingi sana. Sema dada zetu hawa nao kuna muda akili zao hazina akili, anaweza tokea mtu wa maana anataka kujenga nae future na amuoe, dada mwenyewe sasa kakomaa na limtu lisilo na dira kabisa, mipombe, kubeti, visuruali vya kubana. Hovyo sana wadada
Duuuh! mkuu,mwanaume akiwa aabet responsibly,hafai kumuoa mdada anayejielewa?
Mbona naona walimu,manesi,madaktari,wafanyabiashara n.k wanabeti?
Aisee.
 
Habarini?

Ninaomba nieleweke kwamba mimi si mgeni, nimekua nikisoma mijadala mbalimbali lakini leo nami nimewiwa nilete kisa changu ambacho ninaamini kwa namna moja au nyingine kitawasaidia watu kadhaa.

Mimi mwanamke wa miaka 32, nimeajiriwa mahala Fulani. Kiukweli, nilikua kwenye mahusiano Kwa muda mrefu sana tangu nikiwa chuo hadi hivi majuzi. Hali ya mahusiano yetu yalikua ya kusuasua mno. Leo mko poa, kesho majanga hali ambavyo ilinikatisha tamaa sana. Ingawa jamaa alinitamkia ndoa wakati Fulani lakini binafsi kwa tabia za jamaa, sikuona hata kivuli endapo tungefunga ndoa.

Mwenzangu kwanza ni mnywaji sana wa pombe kiasi kwamba mara kadhaa ilimletea shida kwenye ajira yake na alisimamishwa mara nyingi sana. Mbali na hiyo, ni mtu ambaye bado hajui anataka nini. Leo mtapanga hiki, kesho mtagombana muanze upya so mnakua mara kadhaa hakuna mtakachokamilisha.

Mara nyingine anadai anataka kuoa mtu wa kabila lake, mara anaweza kuanzisha mahusiano na vitoto vya chuo ingawa yeye ana 36 years.

Kwa mahusiano yetu ya miaka Zaidi ya nane, hatukuwai kujaliwa mtoto ingawa jamaa alinitamkia mara moja akisema ananiacha sababu simpi mtoto then baadaye akaomba msamaha na maisha yakaendelea.

Mungu si Athuman! Mwezi wa tano nilijigundua ni mjamzito. Nikamshirikisha mwenzangu ambaye hakuwa na furaha nayo kabisa. Akanishauri sana tutoe tukizingatia bado tunajitafuta and blablabla.

Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.

Kweli, jamaa alihangaika sana kunishawishi kutoa ili tuendeleze mahusiano (ambayo hayana dura) nikaamua kuweka msimamo wangu kwamba akijisikia kuondoka, aondoke ila mtoto kama lolote likitokea basi liwe limepangwa na Mungu ila sipo yeye. Aliamua kuondoka na wala sikujushughulisha naye kabisa.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia safari yangu ya ujauzito hadi sasa, hakuna kilichonisumbua. Kiukweli, nina furaha na amani zote, sielewi ni kwa nini. Nimejikuta natamani kuwaambia wanawake wenzangu, wasikubali kuendeshwa na wanaume wa namna hii ili kuendeleza mahusiano.

Focus na unachokichagua kwani hata ningetoa, sio kweli kwamba mahusiano yangeboreka, tena yangekua mabaya zaidi. Ninamshukuru sana na niwatakie jioni njema.
Hahahaha ana date na wanachuo halafu yupo 36, yaani mwanaume huwa hatoki kama wewe hujamsababisha, yaani problem yako unamchukulia huyo jamaa kama mdori and not husband to be. Hakuna mwanaume anayependa kuchukuliwa kama msukule wa kwenye TV series. Wanawake wengi wajinga wakiona waume zao wanapata matatizo badala ya kuwaombea eti unaungana na dunia kumlaani. Wewe ni moja ya hao. Muombe Mungu akupe neema ya kutambua.
 
.......Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.
Single mother by your own conset.

Bear the consquences as results of your decision to have kid before marriage.
 
Hahahaha ana date na wanachuo halafu yupo 36, yaani mwanaume huwa hatoki kama wewe hujamsababisha, yaani problem yako unamchukulia huyo jamaa kama mdori and not husband to be. Hakuna mwanaume anayependa kuchukuliwa kama msukule wa kwenye TV series. Wanawake wengi wajinga wakiona waume zao wanapata matatizo badala ya kuwaombea eti unaungana na dunia kumlaani. Wewe ni moja ya hao. Muombe Mungu akupe neema ya kutambua.
Naona umekwepa kutumia neno kuwa aachr ujinga.

Nimesoma btn lines nimeona mtoa hoja ana tayizo ambalo hatoweza kutulia na mwanaume
 
Back
Top Bottom