begi la pesa
JF-Expert Member
- Apr 11, 2019
- 682
- 1,220
pole sana dada na hongera kwa msimamo huo, ila jamaa kama hajiamini hivi kama ndo amekupa katoto? au ni mawazo yangu tu? .baadae jiandae kwani atakusumbua kuhusu kudai mtoto.
Nimecheka kweli kweli. Bado hujafikia huko?
Watu wazima wanaohangaika na hizi ishu ni wengi mno ila wanaona aibu na sometimes wanaamua kujiua na kuua watoto sababu wakijitokeza kwenye Jamii badala ya kupata msaada watu wanaishia kuwakebehi. Ila wakisikia wamefanya madhara Kwa familia, watasema "Si angeongea!"Kwakweli nyuzi zote zinazoandikwa za kulalamika kuhusu mapenzi me hua najua walengwa ni ambao wako in their 20's.. Nimeshangaa kuona mtu mzima naye anasumbuka nayo
Kila mtu ana historia yake. Usijifananishe na mtu au mapito ya mtu. Kila Jambo Mungu analiruhusu Kwa sababu Fulani.Kumbe kuna watu wana miaka 36 na bado wanajitafuta duh kumbe mi mdogo sana asee!!
Pole. Mwanamke ukishaona mwanaume aliyekupa ujauzito anakuambia utoe basi hiyo ni green light kimbia kufa kupona.Habarini?
Ninaomba nieleweke kwamba mimi si mgeni, nimekua nikisoma mijadala mbalimbali lakini leo nami nimewiwa nilete kisa changu ambacho ninaamini kwa namna moja au nyingine kitawasaidia watu kadhaa.
Mimi mwanamke wa miaka 32, nimeajiriwa mahala Fulani. Kiukweli, nilikua kwenye mahusiano Kwa muda mrefu sana tangu nikiwa chuo hadi hivi majuzi. Hali ya mahusiano yetu yalikua ya kusuasua mno. Leo mko poa, kesho majanga hali ambavyo ilinikatisha tamaa sana. Ingawa jamaa alinitamkia ndoa wakati Fulani lakini binafsi kwa tabia za jamaa, sikuona hata kivuli endapo tungefunga ndoa.
Mwenzangu kwanza ni mnywaji sana wa pombe kiasi kwamba mara kadhaa ilimletea shida kwenye ajira yake na alisimamishwa mara nyingi sana. Mbali na hiyo, ni mtu ambaye bado hajui anataka nini. Leo mtapanga hiki, kesho mtagombana muanze upya so mnakua mara kadhaa hakuna mtakachokamilisha.
Mara nyingine anadai anataka kuoa mtu wa kabila lake, mara anaweza kuanzisha mahusiano na vitoto vya chuo ingawa yeye ana 36 years.
Kwa mahusiano yetu ya miaka Zaidi ya nane, hatukuwai kujaliwa mtoto ingawa jamaa alinitamkia mara moja akisema ananiacha sababu simpi mtoto then baadaye akaomba msamaha na maisha yakaendelea.
Mungu si Athuman! Mwezi wa tano nilijigundua ni mjamzito. Nikamshirikisha mwenzangu ambaye hakuwa na furaha nayo kabisa. Akanishauri sana tutoe tukizingatia bado tunajitafuta and blablabla.
Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.
Kweli, jamaa alihangaika sana kunishawishi kutoa ili tuendeleze mahusiano (ambayo hayana dura) nikaamua kuweka msimamo wangu kwamba akijisikia kuondoka, aondoke ila mtoto kama lolote likitokea basi liwe limepangwa na Mungu ila sipo yeye. Aliamua kuondoka na wala sikujushughulisha naye kabisa.
Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia safari yangu ya ujauzito hadi sasa, hakuna kilichonisumbua. Kiukweli, nina furaha na amani zote, sielewi ni kwa nini. Nimejikuta natamani kuwaambia wanawake wenzangu, wasikubali kuendeshwa na wanaume wa namna hii ili kuendeleza mahusiano.
Focus na unachokichagua kwani hata ningetoa, sio kweli kwamba mahusiano yangeboreka, tena yangekua mabaya zaidi. Ninamshukuru sana na niwatakie jioni njema.
Ni kweli lakini mnachoshangaza, ukiona huyu akufai, unamganda ili iweje? Why wasting ur time? Ama unakua na watatu, wote pia Wana shida?Hayo ni malalamiko ya upande wako ukijipamba, we tabia zako zipoje , wanaume wengi wakiona mwanamke mzinguaji wanakupuuza tu na kukupotezea
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole. Mwanamke ukishaona mwanaume aliyekupa ujauzito anakuambia utoe basi hiyo ni green light kimbia kufa kupona.
Hakuna mwanaume anayeweza kumpa mwanamke anayempenda ujauzito kisha akamuambia autoe.
NEVER!
8 good years!Miaka 8😄
Kwa hiyo ni sawa kumwaga damu sababu ya kulea? Na Hakuna sehemu niliyosema ninamtegemea. Sijui ni kwanini wengi mnaongelea abortion kama kuchinja kuku. Huwezi kukionea kiumbe kisicho na hatia huruma? Utembee na dhambi ya kumwaga damu hadi siku ya kifo? Ili iweje, aendelee kubaki na mimi then nikiwa naye napata faida gani kubwa? Kwa uzazi ulivyo changamoto hivi? Mbona kuna wababa wana huruma mno, wanabeba majukumu huku wanaamua kuwa Ni mtoto aliyetelekezwa. Na uzuri mtoto akiwa Hana mzazi, anasimamiwa na Mungu.Amekwambia toa mimba muda bado. Ukakataa. Sasa kakutelekeza kivipi wakati umeapa kwake liwalo na nalo liwe?!
Acha kulazimisha majukumu kwa mwanaume. Umejitakia mwenyewe kuwa single maza. Pambana na Hali yako...
Mwamba alikua anaisomesha mileage akampa na zawadi ya mtoto8 good years!
Kwakweli Bora umeongea, hiyo ya kujidhuru ndo mbaya zaidiWatu wazima wanaohangaika na hizi ishu ni wengi mno ila wanaona aibu na sometimes wanaamua kujiua na kuua watoto sababu wakijitokeza kwenye Jamii badala ya kupata msaada watu wanaishia kuwakebehi. Ila wakisikia wamefanya madhara Kwa familia, watasema "Si angeongea!"
Mbona mnatutisha sasa, miaka 32 bado mnasumbuka na mapenzi 🤔🤔
Nimeanza kuamini kweli mapenzi hayana umriTunateseka mdogo wangu
Imagine watu wameoana, wanawatoto Zaidi ya watatu, baba kaamua kuoa mtu mwingine kimyakimya na kutelekeza familia 😢 hiyo utafananisha na kukimbiwa na baba mtoto ambaye hamkuwa kwenye maagano? Wababa wengi wanateseka ila watasemea wapi!Nimeanza kuamini kweli mapenzi hayana umri
Kumbe wewe bado katoto?! Itabidi niache kuchangia thread za mtoto.Kwakweli nyuzi zote zinazoandikwa za kulalamika kuhusu mapenzi me hua najua walengwa ni ambao wako in their 20's.. Nimeshangaa kuona mtu mzima naye anasumbuka nayo
Unaweza kukuta hata wazazi wetu wanateseka Ila ndo hivyo Tena hawana namna inabidi watunze heshima ya familia 😌😌Imagine watu wameoana, wanawatoto Zaidi ya watatu, baba kaamua kuoa mtu mwingine kimyakimya na kutelekeza familia 😢 hiyo utafananisha na kukimbiwa na baba mtoto ambaye hamkuwa kwenye maagano? Wababa wengi wanateseka ila watasemea wapi!