Baba Mkwe wangu ananitishia NISHAURINI

...Duh! Mkuu Paka Jimmy, hayo Masharti unayodhani Jamaa kamuwekea Mkewe...!!! Ngoja kwanza niendelee Kuvunjika Mbavu..!!!😛ound:😛ound:
 
Tafuta jamaa yoyote kutoka mkoa wa Mara akuonyeshe jinsi ya kuishi na mkeo.Mkeo hana tatizo ila wewe mwenyewe tu, kiburi, ubabe na jeuri aliyonayo unailea wewe mwenyewe.Mpe kichapo cha nguvu pamoja na orgasm la nguvu mbona atakuwa mtiifu.Yaani na kushangaa kumrudisha mke nyumbani kwa kakosa kama hako.Kosa kubwa kwa mwanamke ni uzinzi na ushirikina tu mwengine kama mwanaume unatakiwa kuyasolve bila hata kuwashirikisha watu.
 
Vp kwa upande wa mke yeye anareact vp je anatoa maelezo yoyote ya kukuplease au yuko kmya tu?

Kwa sababu anataka aonekane hana kosa haswa mbele ya wazazi wake anajitahidi kuonyesha kuwa reaction ya wazazi ni yao binafsi asihusishwe jambo ambalo ni la kisanii sana na haiwezi kuwa kweli
 
 

Nilishawaeleza twice mara ya kwanza walielewa na kumwonya na mara ya pili pia
 
...Duh! Mkuu Paka Jimmy, hayo Masharti unayodhani Jamaa kamuwekea Mkewe...!!! Ngoja kwanza niendelee Kuvunjika Mbavu..!!!😛ound:😛ound:

Mkuu kuna watu wamekulia kwenye maisha ya kanuni kutoka kwa wazazi wao,wengine wamepata kanuni wakiwa kwenye mafunzo mathalan shule na wengine labda kwenye military training na wengine makazini!

Kosa wanalolifanya ama niseme tunalolifanya wanaume wengi kwa makusudi ama kutojua ni kufikiri baada ya kulipa mahari ndiyo umemnunua binti wa watu kwa ujumla na kwamba akifika kwako ni lazima afuate prinsiple ulizojiwekea...ni kosa kubwa sana kwa kuwa victim atakuwa wewe mwenyewe so far mkeo atakuwa anaishi nje ya kanuni zako!

Sio jambo rahisi kwa watu wawili mliozaliwa na wazazi tofauti,mkakukia kwenye mazingira tofauti,tena kwa malezi totauti kukosa kasoro mbili tatu. Muhimu si kufukuza bali kujua nini cha kuacha wewe ama kujiongeza ili walau muendane kwa maana ukianza kukosoa sana mwishowe nawe utajikuta unajikosoa!
 
Kabla ya kumrudisha kwao ulishazungumza na wakwe zako? Kumrudisha mke wako kwao ni dalili mbaya kama bado una nia ya kufanya mazungumzo na isitoshe mda wote huo wazazi wako ndio walokuwa waamuzi! Ni vipi kama wakifikiri mlikuwa mkifanya maamuzi ya upande mmoja?
 
Ni wiki imepita tangu nimrejeshe kwao wife kwa mara ya kwanza tangu tuoane miaka 10 iliyopita kutokana na kutozingatia makubaliano tunayowekeana kama couple na jeuri
NISAIDIENI BUSARA ZA KU REACT!!!!

Kwani mmewekeana masharti gani?
 
 


ni kweli huyu mkosa mada kwanza kaeleza ksi upande mmoja tu halafu anataka tumhukumu mke wake na wazazi wake bila kuwasikia au kueleza matatizo yao kwa kina..

nakubaliana na wewe kwa 100% kuwa huyu jamaa ndiye mwenye matatizo na sio mke wake, na huyo mwanamke anonysha ni mzuri na anaelewana hata na wakwe zake vizuri(wazazi wa mume) na dio mana kwa maelezo ya jamaa huyu mke huwa anakimbilia nyumbani kwa wakwe( wazazi wa mume). Na pia wazazi wa mume wasingemtetea kama kweli huyu binti angekuwa mkorofi kama mleta mada anavyotaka kutuaminisha.

Na ili kuthibitisha kuwa huyu binti ni msafi na huyu jamaa ndio mkorofi ndio maana wazazi wake yeye binti pamoja na wazazi wake yeye kijana wanamtetea. kwa vyovyote vile huyo kijana ndio mwenye matatizo na sio huyo binti. Kumbuka kuwa wazazi wako wwe na wazazi wake yeye wote ni watu wazima wenye busara zao. Haiwezekani wote kwa pamoja kwa nyakati tofauti wamtetee mke wako, ni lazima ww una matatizo.

Na pia kwa nini umlazimishe aende kwao wakati yeye huwa anakwenda kwenu? kwani wazazi si wale wale tu kama mtu ameamua kwenda kwenu kwa nini umzuie na umlazimishe aende kwao. Wewe ndio huna busara kabisa, yaani binti anajaribu kuficha aibu ya magomvi yenu kwa wazazi wake halafu ww unamlazimisha akawasimulie? Hivi ulifikiri wazazi wake wanamchukia binti yao kama wewe? We umepata mke mzuri ambaye anakufichia upuuzi wako kwa kutowaambia ndugu zake ili ndugu zake wasikuchukie. huyu mke anakupenda sana na hataki uonekane mbaya nyumbani kwao, halafu ww unalazimisha uonekane mbaya kwa wakwe? kichwa yako ina matatizo si bure

Na mwisho mambo ya kurudishana nyumbani yamepitwa na wakati, eti nirudi nyumbani nikafanye nini? kha tutabanana hapohapo..hapo sasa badala ya kusove ishu umeitapakaza na kuwa stori ya mtaa.....
 



Sikiliza mafundisho ya ndoa na familia Kiisa Siku jumatatu saa 3 kamili usiku Radio 5, au alhamis saa 3 kamili usiku radio upendo. MUNGU ATAIOKOA NDOA YAKO NDUGU YANGU.
 
muhadisiaji akiwa mmoja habari huwa haikamiliki,embu mlete hewani shem nae atuambie,enasema miaka 9 matatizo yote wazazi wako ndo washurulishi mwaka wa 10 ndo wakweze wakusaidie,inaonyesha hiyo ndo inamigogoro kweli kila mwaka mnagombana kiasi mpaaka muamuliwe?hapa ni zaidi ya uyasemayo mlete shemu nae amalizie upande wa pili, ama sivyo unanifanya niamini tunajadiri kitu tusichokielewa vyema.
 
Kwanza pole sana Mwanakwetu, hata kabla ya kuuliza swali naanza kama mtabiri. Huyu wifi lazima ni binti wa kwanza katika watoto wa mzee huyo, kwa sababu inaonyesha tangu utoto amekuwa akideka sana kwa wazazi wake. Ingekuwa kuna binti ambaye ni dada yake angeangalia maisha ya dada yake katika ndoa na angejirekebisha. Hapo hana sehemu anaweza kuiga maisha ya mtangulizi wake.

Nikisoma mada hii najifunza kitu toka kwa Baba yake kwamba anamchango mkubwa sana kuharibu mwenendo wa mwanae. Uthibitisho wa hili ni pale anapomwambia kuwa atamrudisha kwa nguvu na kwamba hata akishindwa kufungua mlango atauvunja, hii inampa kichwa cha mbuzi binti mwenyewe kwamba safari hii amepata mtetezi wa uhakika. Kitendo cha Baba mkwe kutamka hivyo inaashiria wewe kaka umekuwa tegemeo kubwa kwa familia hii bila wewe kujua. Nasema bila wewe kujua kwasababu huyu wifi inaelekea amekufanya ni kitega uchumi chake.

Mfano:- Ukiona amejaa kiburi ujue amekusanya kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwako na hivyo zinampa jeuri. Kujifanya amejirekebisha kwa kipindi cha mwaka mmoja ni pale anapopanda DECI yake na baada ya muda anavuna na kujaa nundu ya kiburi tena.

Watu wa namna hii hujifanya wako busy kuwatembelea ndugu zao, kumbe hapana anatumia muda mwingi kuwatembelea marafiki zake kuwaonyesha uwezo alionao kifedha. Ukali na kiburi chake ni silaha ya kuhakikisha anaendelea kuwa katika hali ya kifedha ili isiwe rahisi kwa marafiki zake kugundua mapungufu yake kifedha. Kwa asilimia kubwa huyu wifi anapotoshwa na marafiki zake, yawezekana kindoa ni mwaminifu japo ni dhaifu wakati mwingine.

Ushauri wangu:-

1. Siku akirejea hapo nyumbani baada ya kufikia suluhu usimpe kiasi kikubwa cha fedha kwani hata katika maandiko kuna maandiko yanasema "Kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote.

2. Kuna wale ambao Baba anafanya biashara tofauti na mkewe, la msingi hapo ni kuwa na akaunti moja kuleta discipline ya fedha.

3. Itisha kikao upande wako na upande wake wifi mkae pamoja mkishirikisha wazee wenye busara sana wampe maadili binti huyu kizungu mkuti mdandia treni kwa mbele.
 
imenisikitisha sana ishu hii. Pole sana ndg yangu, hiyo ni mitihani katika maisha na mitihani hiyo tumeumbiwa sisi wanadamu. Kaka cha kufanya hapo ni kuwashirikisha ndugu zako wewe wajue vitisho unavyopata kutoka kwa wazazi wa mkeo, (nimekushauri uwashirikishe ndugu zako pia kwa kuwa kwa sasa matatizo yenu sio siri za ndani tena, familia zenu zinayafahamu). Hii itasaidia kwa wao pia kuingilia kati na kukaa pamoja pande zote mbili na kufikia muafaka wa suala hili.
 
Hivi mwanamke hawezi fanya maisha yake bila kuwa kwenye ndoa? Kitendo cha wazazi kutoa vitisho ni kuonyesha jinsi walivyo wadhaifu kwa kutaka kumrudisha haraka kwa mmewe. Wanaona shida gani ya kumuita mkwe wao na kujua nini hasa tatizo linalowakabili.
 

Vitisho nimesha vi ripoti polisi dada asante. Kwani siwezi kuwa submissive zaidi ya hapo kiasi cha kudharauliwa na baba mkwe kiasi hicho?
 

Kwenye RED nafikiri ingekuwa solution na hata mimi nilitaka ikiwa vipi niwe free ili wife awe huru ku exercise tabia zake hizo kwa uhuru bila kuingiliwa. Iweje wang'ang'anize kurudi kama vile nao hawamhitaji?
 
mimi mwanaume hawezi nirudisha nyumbani kamwe,kwanza im idependent woman anaanzaje kunirudisha kwetu?kanikuta nilishatoka mikononi mwa wazazi eti anirudishe big no,hata alete winch,kurudi kwenye maada kwa nini wewe Mwana Kwetu hujasema mkeo kafanya nini mpaka umrudishe kwao?Inawezekana wewe ndo una makosa,kuwa muwazi
 
Last edited by a moderator:
maisha ya ndoa haya mwalimu wala doctor, maisha ya ndoa mwalimu wake na doctor wake ni mke na mume, wakati namuoa mke wangu nilimwambia matatizo ya ndani yatatatuliwa na sisi wenyewe, yakifika kwa wazazi wangu au wazazi wake au mtu yeyote awe ndugu au asiye ndugu kwa kusudio la kuyatatua basi ndo mwisho wa ndoa yetu,
 
Mwana Kwetu mbona unakuwa mgumu kusoma alama? Ina maana hata wao pa kumuweka hawapaoni, tena ilikuwa nafuu kuwa at least yuko mahali, halafu wewe unamrudisha? Lazima tuvunje mlango kukurudishia bwana....


Pole yangu bado unapata, coz inaonekana ushauri utapatikana kwa wazazi wako sio wake...
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…