Muuza simu used
JF-Expert Member
- Aug 23, 2017
- 4,393
- 7,107
Pole sana MkuuLeo week ya pili nimeshindwa kabisa kupokea simu ya Baba mkwe na Mshenga wangu.
Iko hivi katika misoto yangu na kukulu kakala za maisha atimae nikajikuta nimedondokea kwa mtoto wa kichaga Kama ilivyo janga kwa wanaume wengi wa mjini.
Mipango ikapangwa na siku ya kufika ukweni kupeleka posa ikafika. Kidume nikajikoki na Mshenga wangu na wadada 3 wa kukodi tukazuka ukweni.
Mambo yalikua shwari hadi pale mjomba mtu akapewa fursa ya kutupangia package ya mahari ili mpango mzima ukamilike.... list ya makorokoro kibao, Mara mkaja wa mama, Bibi, mablanket ya Mama na mashangazi, mbege mapipa matatu, mbuzi 3 wa maziwa na....mwishoni akataja cash money 3 Mil.
Mimi kipindi anataja yale mazaga hata nilikua sifuatilia ,akili yote ilikua inasubiri point ya msingi Cash money.
Badae ikatolewa option ya ku convert the overall cost ika amount Kama 5 Mil. na ushee!
Jitihada za mshenga kupangua bei hazikuzaa matunda. Mbaya zaidi ile tumemaliza events shangazi anatuzuia hakuna kuondoka mpaka tumelipia gharama za maandalizi walioyotufanyia.
Kwa shingo upande nikausukuma mzigo wa M pesa tsh 280, 000 coz walidai laki 3.
Niliporudi lodge usiku mzima sikulala , series nzima ikawa inaji frash back repetitively.
Nika najiuliza kwani wananiuzia mke kisa ni afisa ustawi wa jamii?
Ana kipi Cha ziada ambacho wake wa ndg zangu wameolewa na jumla ya mahari tulizotoa na makokoro yote hata milioni haikufika?
Kwani ana kismat Cha mafanikio? Mbona tangu tuingie kwenye relationship mambo mengi tunakimbizana kwa had-hoc za kufa mtu?
Na mengine mengi ambayo si busara kuyaanika humu.
Alifajiri nikaamua kufanya maamuzi magumu ..."Katu sitorudi tena ukweni." Kwa maana kuwa sitoi tena mahari, mtoto wao nimeshamtia mimba ,wakimtaka waje wamchukue.
Ni hayo tu.....sirudi ukweni tena
Mashemeji zangu wachaga povu ruksa. Ila katu sirudi tena ukweni.
umefanya good decision achana na huyo punguwani.....huwez lipa mahari yote hiyo mkuu...ila mkuu ulienda kuoa Machame niniLiwalo naliwe...I have made my decision
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119] Jamani nimecheka asubuhi yote hiiiiSolution hii hapa mkuuView attachment 1220901
Ya nini kujisumbua na madeni wakati iko mikoa unapata mke hata kwa aya moja tu kwenye quranHuyu kijana Mang'aa yeye na mshenga wake wameshindwa kuelewa mila za kichaga. Mimi mchaga pure nilioa mchaga mwenzangu nikalipa mahari laki 8.
Hayo makorokoro mengine yanayofika milioni kadhaa utaratibu unalipa mdogo mdogo mpaka uzeeni.
Mzee wangu mpaka sasa hajamaliza mahari huwa tunaamini mahari ni jambo endelevu.
Hiyo laki 8 ni vile vitu muhimu vya kununua kimila.
Naona shemeji ako mmoja huyu hapa kaanza kukutisha.Itakuja kukukosti.
Sure hapa hawajamtendea haki mwana.Wamezingua kwa kifupi.Mm nisingerudisha maana akil yangu naijua mwenyewe jinsi ilivyo faster kufanya michanganuo na kuchukua maamuzi.Dah poa braza tunaheshimu maamuzi yako, usirudi tu ukweni, sio sababu ya mahari kubwa ila kuombwa kurudisha gharama ya tafrija ile sio sawa kabisa maana we hukuwaambia waandae tafrija ila ni wao kama wao
Nimecheka kwa sauti kwenye daladala [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Solution hii hapa mkuuView attachment 1220901
Jamaa unaroho ngumu kinoma yaani unawasusia na ushamjaza mimba??
Kabisaa hiyo 280k na mm imeniuma kama nimechangia kuitafutaBado kidogo nikushauri uongee na huyo mama watoto kuhusu hilo mil 5 ili awashawishi wazazi wakupunguzie..
ila kila nikiikumbuka laki mbili na themanini ya chakula uliyolipishwa naskia uchungu Chief..
tupa kule hio familia takataka.