Baba mkwe kakataa mahari... kuku! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba mkwe kakataa mahari... kuku!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 4, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Kabla hujaamua kupeleka mahali kwa watu hasa kwa wale wasio wa kabila lako husisha watu kwanza...

  Kijana mmoja chakaramu alimpenda binti kutoka mojawapo ya makabila yanayofuga ng'ombe sana maeneo ya kanda ya ziwa. Bila kumuuliza mpenzi wake jamaa akaamua kufunga safari kwenda kijijini kwa wazazi wa binti kujitambulisha. Alipofika huko akajitambulisha na kuleta zawadi za kuku kama kianzio cha mahari...mambo yalikuwa hivi:

  Mzee: Karibu kijana habari za wapi?
  Kijana: Miye natoka mjini mzee na nimekuja kuleta ujumbe wangu wa kujitambulisha
  Mzee: Ah kujitambulisha nini?
  Kijana: Mzee mimi na binti yako tunaishi pamoja na nimekuja kuomba baraka zako ili nimuoe
  Mzee: Umekuja kunini!!? kwa tahamaki mzee aliuliza.
  Kijana: Kuomba baraka zako.

  Mzee alikaa kimya kwa sekunde kidogo.

  Mzee: Na hilo tenga la kuku?
  Kijana: Mzee ni kifunga uchumba!
  Mzee: Baba una wazazi wewe?
  Kijana: Hapana mzee wazazi wangu walishafariki
  Mzee: Una wazee huko kwenu?
  Kijana: Wazee wa nini tena baba?
  Mzee: Kijana umenitusi na kunitukana kwa namna za ajabu kabisa. Naomba uondoke hapa.


  To cut the long story short...


  Miaka 25 baadaye kijana (sasa mzee) anaishi na binti wa wote; wamezaa watoto na hawajafunga ndoa na hajaonana na baba mkwe tangu siku ile.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Asante kwa hadithi hadithi!.

  Ila haijatulia kwa sababu its too good to be true!.

  Muoaji toka kabila la wafugaji kwenda na kifungauchumba cha kuku?!.

  Binti unaishi nae asikueleze mahitaji ya kwao?!.

  Baada ya ba mkwe kususa life ikaendelea miaka 25!. Msuso wa wazazi hata mwaka tuu ni karne, ndio itakuwa miaka 25!.

  All and all hadithi ni hadithi,

  Thanks.

  Pasco
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280

  well ni kweli kwa kila details ukiondoa "pakacha"; walikuwa kuku lakini.
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo ya washenga, huendi peleka uchumba bila kuwa na mshenga. Huyo jamaa alikosea kwa hilo!


  Chengine sidhani kama kwenye sehemu za kufunga ndoa wanauliza kama baba na mama wameridhika au mmpata baraka zao. Wangapi wameoana bila ya kupata muafaka wa wazee wao, kama wameamua kuishi pamoja bila baraka za wazee sioni tatizo la kutofunga ndoa, it doesn't make different to me.
   
 5. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Hay MM naona umeamua utembelee jukwaa hili kwa staili ya kishigongo shigongo,karibu mwanafyale
   
Loading...