Baba mkwe anaponiambia nijiongeze ana maana gani au anataka kumuozesha binti yake kwa mwanaume mwingine?

Ndugu habari za saiz kwanza mtaniwia radhi kwa rafudhi yangu, mimi nina mke tunamiaka 3 ndani ya ndoa yetu mwaka tulio ingia kutimiza miaka 3 nilimuomba mke wangu nikatafute maisha Dar es salaam miezi minne baadae na yeye nikamleta Dar es salaam.

Akakaa mwaka mzima tukapanga tujikite kwenye kilimo akakubali pia akarudi nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya kilimo baada ya kilimo kufika mwishoni mke wangu ameenda kwao na baba mkwe amempokea pia hakunijulisha chochote nilijaribu kumpingia aliniambia nijiongeza kama redio ya mbao mke kumuuliza kilicho mpeleka anasema amechoka kukaa peke yake.

Sasa najiuliza maagano yetu yamekuwa bure? na kama amechoka kukaa peke yake kule nyumbani amepata wakukaa nae mpyaa? pia ananiambie niende nyumbani kama siwezi kwenda hawezi kurudi analazmisha na mimi hapa Dar es salaam sio kibarua nimeajiliwa kuacha kwa kukurupuka siwezi nitakuwa nimevunja mkataba sasa najiuliza baba mkwe ana maaana gani kusema nijiongeze?

Anataka kumuozesha bintie semu nyingine? naombeni ushauri wakuu nifanyi kipi cha kuokoa ndoa hiii nimeweka mezani ,,asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana bro.
Hata mimi nakushauri ujiongeze Aisee..

Samahani kama bado hujaelewa bado...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom