fimboyaasali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 8,606
- 8,269
hiyo para ya meisho umeandika nini?Baada ya kuweka mizizi mizuri ukweni na kuwa na mahusiano mazuri na ukweni kwangu, niliamua nikatoe mahari baada ya miezi kadhaa kutoa posa, mshenga alimuuliza baba mkwe wajipanga vipi siku wakitaka kurudi hatua inayofuata.
Baba mkwe alisema nataka kuona hao wawili wana mahusiano mazuri.
Basi baada ya miezi kadhaa kupita ilibidi nitoe taarifa kwa mshenga kwamba nataka tukatoe mahari.
Taarifa ilimfkia baba mkwe na tulipanga siku ya kutoa mahari.
Ikiwa imesalia wiki moja kufika siku ya tukio, bibie alitangulia kwao ili kupokea wageni wake.
Ajabu baba mkwe aliomba kuongea na mimi, akanimbia anataka mimi niende kwanza kabla ya tukio.
Basi nilipohitikia wito wa baba mkwe, aliniuliza maswala mengi na tuliongea kama masaa 3 hivi na mchanganyiko wa story za huku na kule.
Baada ya maongezi, baba mkwe akasema sioni sababu za wewe kutoa mahari kikubwa ni kuzingatia hayo tuliongea na kumtanguliza Mungu.
Asema baba mkwe, naona kabisa ni jinsi gani mwenzio umemtunza na naona kabisa mabadiliko ya maisha kwa mwanangu, sikuwah kujua kama mwanangu ni mtu mwenye furaha hivi, siku hzi naona kabisa amechangamka tofauti na zamani.
Baada ya kurudi home,simu yangu moja kwa moja kwa mshenga kwamba ukweni hawataki mahari ila tutaenda kufamiana na maongezi zaidi lakini tusipeleke cent yeyote.
Mwenzenu nimeoa ndoa ya kanisani, licha bado tunaishi tofauti. hapa nafatilia maswala ya huakika cheti cha ndoa.
Mimi nimesema nilicho kisema hayo mengine ni ya kwako kijana
Ewaaaah 😂😂😂😂Huyo baba mkwe ni kama mimi, nimeshapanga sitakuja kupokea mahari kwa mabinti zangu
Huyu nishawahi mimi mkuuMkuu naomba tufahamiane, mapema...
Mzee anamjuua mwanae,unaweza Kuta hatulii na mwanaume! Koo mzee hatakii aibu. Take care
Soma kwa makini sana hiyo comment itakusaidia...Mimi niliandaa mahari na niliomba tuambie mahari, hapo kweli tunapenda vitonga?
Naona msambaa umemkomalia kijana wa watuMahari ni ya mwanamke sio ya baba, bibi wala mjomba.... Mpe mkeo mahari yake acha janja janja
Msambaa [emoji848] usiniweke kwenye makabila yasiyoelewekaNaona msambaa umemkomalia kijana wa watu
Mtibeli kashadandia uzi na hakuna kitu mleta uzi unaweza kumfanya🤣🤣😇.. Nakubali sana pigo za Mtibeli by the way.💪💪💪Huyo Mzee ni Mtibeli.
Watibeli ndio tupo hivyo. Hatuwezi uza Binti zetu kama watumwa.
Ni Binti zetu, Binti wa Tibeli ni Binti huru.
hakika wako wengine. Ni tatizo kubwa mpka unajuta.Piga kifua sema umempata baba mkwe mwana sana .
Yapo mengine hapo yangetaka uyape mpaka hela za kuzeekea na kuzikwa nazo ila hilo libaba mkwe lako lina miakili sana
Afu ulipaswa ujiongeze,nunua blangeti la bibi na baba na mama na,Kanga na vitenge vya mashabgazi muulize mwenzio atakupa idadi ya wanaostahili kupata hivyo na mazaga mengine mwambie mkwe umeleta zawadi.Mama mkwe wako na shangazi watajua anagawaje hivyo kwa watu wana.
Usisahau shangazi ni baba,Shangazi apewe kitenge kizuri na shati la mumewe.
Ukimaliza kuja kunishukuru.
Umetisha sana mkue