MKATA KIU
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 3,481
- 8,582
Habari wadau.
NIna baba yangu mdogo alikuwa bosi kwenye wizara moja serikalini. Alikuwa na cheo cha kamishna kwenye taasisi moja inayosimamiwa na wizara yake.
Mwaka 2021 Bahati mbaya baba mdogo alipata matatizo kazini. Matatizo hayo yalimfanya apoteze ajira yake na kupata kesi mahakamani.
Ilichukua miaka miwili mahakama kutoa hukumu ya kesi hiyo. Ambapo ilimuamuru aende jela miaka 8 ama alipe faini milioni 40.
Ikabid familia ikae vikao. Ila milioni 40 hiyo haikupatikana ndani ya muda wa kulipwa uliopangwa . Baba mdogo akahukumiwa kwenda jela.
Kilichoniumiza hiyo hela ni ndogo kuliko uwekezaji alioufanya baba mdogo kwa watoto wake kielimu.
Baba mdogo ana mtoto wa kiume above 30 yrs wakati anahukumiwa. Mtoto huyo alisomeshwa chuo uingereza na shule alisomeshwa shule maarufu za mama lwakatare. Ila alishindwa msaidia baba yake sababu hana ajira ya kueleweka.
PIa baba mdogo ana mabinti wawili wote walikuwa above 27 wakati baba mdogo anahukumiwa. Na hao mabinti chuo mmoja alisomeshwa india na mwingine malaysia.. ila na wao walishindwa kupata hela ya kumchangia baba yao.
Baba mdogo alikuwa mtoaji mzuri kwenye kanisa lake alilokuwa anasali. Ambalo ni kanisa la dhehebu maarufu kwa sheria kali kwa waumini wake. Kanisa lake pia lilishindwa kufanikisha kupatikana hiyo hela ya faini.
Baba mdogo ana nyumba nzuri ya kuishi ya ghorofa moja ambayo yeye na familia yake walikuwa wanaishi. Nyumba bado ipo familia yake inaishi, hakuiuuza ili alipe faini maana familia haina nyumba nyingine ya kuishi.
Binafsi najiuliza hivi ni sahihi mzee wa miaka 60 kukubali kwenda jela sababu familia yako itakosa nyumba nzuri ya kuishi ?
Pia najiuliza nini faida ya kusomesha watoto shule za gharama ama nje ya nchi kama ajira yao hujawaandalia unategemea waje kuajiriwa na watu wengine? Hela za ada alizotumia baba mdogo angejengea nyumba nyingi, nahisi zingemsaidia kukwepa kwenda jela.
Pia najiuliza, je wanaume ni magreda kazi yetu kuchonga barabara tu. Tumekuja duniani kujali mke na watoto na sio kujijali wenyewe ?