Baba, mama, binti nani mwenye makosa??


charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,153
Likes
1,594
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,153 1,594 280
Mu hali gani wana MMU???

Kuna Bi shost mmoja alipata nafasi ya kuchukua degree katika chuo kimoja Jijini Dar Es Salaam, basi bana Degree ikapata attachment ya ujauzito baadaye akajifungua mtoto wa kiume kabla ya ndoa. Mamake akafanya manuva ya kufa mtu mpaka binti akafunga ndoa ila ndoa imekuwa ndoanoooo!!!!!

Kabla ya kumaliza chuo binti alipata ujauzito.... Taarifa zote alipewa mama mtu, mama mtu kila mara anafunga safari kutoka Kigoma mpaka DSM kufuatilia hali ya mwanaye mjamzito bila baba mtu kushtukia issue nzima. Kila mara baba mtu alipouliza mbona binti yetu haji likizo, mama ake binti alikuwa akimtetea mara ooh yuko field, mara ooh kapata kazi temporary kwenye Kampuni flan atakuja tu.......

Mwisho wa siku binti akajifungua, baba huko Kigoma hana habari. Na vile aliishia vidatoni ndo kabisaaa hawezi kufatilia ratiba za chuo. Mama kafunga kibwebwe ataka aoneshwe mkaza mwanaye, binti huyooo kamuonesha mamaye kijana alompa mimba. Mama akamwambia bintiye kijana mwenyewe naona hana hata mpango wa kukuoa. Miezi yote tisa mpaka mtoto anakaribia kuanza kukaa mwanaume hana hata dalili ya kuoa.

Hapo mama na bintiye wanaumiza kichwa wapi wataficha aibu yao kwa Mzee, Mzee mwenyewe ni mnene wa Chama fulani hapo Kigoma. Basi akili mukichwa, mama akamshawishi bintiye waende kwa Mtaalamu wa kamati ya ufundi " Sangoma".... Salaaale!!!! Mtaalamu akafanya mambo mpaka kijana akalainika, mwisho wa siku akatangaza ndoa bana......

Kijana akafuata utaratibu kama kawa, ila siri ya mtoto ibaki kwa mama na binti. Bahati nzuri kijana naye alikuwa anatokea Kigoma, basi taratibu zote zikafanyika bila binti kwenda kwao ili issue ya mtoto isijulikane kwa Mzee.... Mahari ikapangwa na ikalipwa, vikao vya harusi na send off vikaanza pande zote mbili.

Na vile Mzee alikuwa mnene wa Chama Mjini hapo, alikusanya michango ya kufa mtu. JAMANI HAKUNA SIRI YA WATU WAWILI DUNIANI AISEEE...... Sijui kilitokea wapi kidudumtu kisichopenda mafanikio ya wenzao.... "Hayo ni malalamiko ya binti baada ya mkasa mzima" Si kikaenda kumtonya mnene..... Bintiyo alishabeba mimba na kujifungua mtoto wa kiume na hata kuishi tayari anaishi na huyo mumewe mtarajiwa!!!

Mnene alifyum yaan ilikuwa balaa nusura ya mkosi, ugomvi ukamuendea mama mtu. Mzee kuunganisha dots ndo akagundua chanzo cha safari za mara kwa mara za mkewe kwenda Dar Es Salaam. Ndani hakukaliki, mama keshatukanwa kila aina ya matusi. Ila MMAZA BANDIDU kweli alikana kujua ujauzito wa mwanaye ila mwisho wa siku mnene alipokaribia kumuUFOO SARO mama alikiri kila kitu....

Mzee akamwambia kama unataka nikusamehe naomba urudishe michango ya kila mtu aliyechanga katika maandalizi ya send off. Dah...... Bonge la aibu!!!!!!!! ili kunusuru maisha yake ilibidi afiate maelekezo aisee. Kila shilingi ilirudi kwa mwenyewe kama ilivyochangwa na sherehe ya send off ikaishia hewani....

Dah... Usingizi unanilemea kesho.nitamalizia upande wa binti na upande wa kijana!!

Stay tuned......
 
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Messages
5,609
Likes
1,062
Points
280
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2011
5,609 1,062 280
Safi sana. Ujinga muufanye huko aibu nïibebe mimi kwamba nimeharibu pesa za watu!
 
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,005
Likes
6,446
Points
280
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,005 6,446 280
umeanza lini huu mchezo??
 
Ablessed

Ablessed

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2013
Messages
4,621
Likes
118
Points
145
Ablessed

Ablessed

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2013
4,621 118 145
Ni hadithi nzuri ngoja niisubiri ingawa nang'atwa na mbu jamani tamthilia zingine hizi zina mambo.
 
Slave

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Messages
5,317
Likes
741
Points
280
Slave

Slave

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2010
5,317 741 280
Ndoa ndoana.inawezekana mdingi ndiye mmegaji kwa binti hata huyo chalii atakuwa wake
 
C

chibahu

New Member
Joined
Nov 22, 2013
Messages
3
Likes
0
Points
0
C

chibahu

New Member
Joined Nov 22, 2013
3 0 0
Mmh huyo mzee simuelewi, kama bint kesha zaa, sasa huyo mzee anatakaje?
 
tinna cute

tinna cute

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2013
Messages
4,649
Likes
82
Points
0
tinna cute

tinna cute

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2013
4,649 82 0
Mzee noma,,, tunasubili hili pich usichelewe sana..
 
Mapi

Mapi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
6,864
Likes
180
Points
160
Mapi

Mapi

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
6,864 180 160
sangoma ndio alikitia kitumbua mchanga.....ila besti kitu kama shigongo. Hahaha
 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,153
Likes
1,594
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,153 1,594 280
Jamani ndo kwanza naamka ngoja nikapata burekifasiti kisha nije hapa..... Karibuni!!!

 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,153
Likes
1,594
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,153 1,594 280
Ilipoishia............

Mzee akamwambia kama unataka nikusamehe naomba urudishe michango ya kila mtu aliyechanga katika maandalizi ya send off. Dah...... Bonge la aibu!!!!!!!! ili kunusuru maisha yake ilibidi afiate maelekezo aisee. Kila shilingi ilirudi kwa mwenyewe kama ilivyochangwa na sherehe ya send off ikaishia hewani....

Endeleaa.........

Mama mtu akarudisha michango kwa kila mtu aliyechanga kwa aibu, ila hakuwa na OPTION!!!!! Pamoja na michango ya Send off kurudishwa haikuathiri vikao vya upande wa Mume mtarajiwa. Ilifika siku ya harusi binti akafunga ndoa bila uwepo wa Baba na wala baraka za baba! Baada ya harusi binti huyooo kaondoka na mumewe kurudi Dar Es Salaam. Mama na baba binti wakabaki na msala, mwisho wa siku wakasuluhishwa na wazee yakaisha.

Maisha yakasonga, JAMANI ACHENI NDOA ZINAZOSHIKILIWA NA KAMATI YA UFUNDI!!!!!!!!! Mkumbuke kuwa chanzo cha ndoa ni kamati ya ufundi, mama na binti hawakuacha kupalilia ndoa kupitia kamati ya ufundi, Kila mara mama na binti wanawasiliana. Enheee mnaendeleaje, sio sms sio calls maadamu mambo yaende sawia. Si makali ya ndoa yaakaanza kupungua, ikabidi mama mtu amtext bintiye kitu cha kufanya, ooh fanya hivi chukua hiki na hiki nedna kule na kule fanya haya yafuatayo.

Mungu si Abdallah wala Yassin, mume machale ya naniliu yakamcheza. Siku ya siku akaanza kupekua simu ya mkewe, alichokikuta hatakisahau maishani, mume alimtisha kumuUFOO SARO binti akasema yote, chanzo kikiwa ni Bi. Mkubwa. Mume akafoward zile sms zote kwenye simu yake kisha akamwambia binti tunakwenda kwenu mguu kwa mguu. Binti na mume huyooooo mpaka kwao. Akaita wazee na wazazi pia, akawaonesha ushahidi wote, ooooooohhhhhhh baba mtu kusikia hivyo kidogo apasuke, alitamani ardhi ipasuke aingie kuficha aibu. Mama ndo kabisa "presha za kupanda na kushuka moyo" kidogo afariki dunia.

Mama akakiri na kuomba msamaha yeye pamoja na binti yake, ila mume awaambia binti abaki kwanza kwao mpaka hapo atakapomuita! Mpaka leo bado ndoa hiyo haijasuluhishwa kutokana na ushirikina na mama na binti.

HIVI NANI HAPO ALIKUWA NA MAKOSA ZAIDI????? Binti kumficha baba yake kuwa kapata ujauzito, mama kumshawishi binti kwenda kwa Sangoma, baba kurudisha michango ya Send Off??????
 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,153
Likes
1,594
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,153 1,594 280
sangoma ndio alikitia kitumbua mchanga.....ila besti kitu kama shigongo. Hahaha
Hapana mkuu... MIe huwa sina story za Shigongo hii kitu ni live, natamani watu flan humu watoe ushahidi...
 
badiebey

badiebey

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Messages
5,888
Likes
485
Points
180
badiebey

badiebey

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2013
5,888 485 180
Baba hajielewii,sasa angetulia ankam'sendoff mwanae angepungukiwa nini?
mama nae mshirikina kwel
binti bora hakuitoa hyo mimba alee mwanae
 
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
45,860
Likes
16,300
Points
280
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
45,860 16,300 280
Wazazi wengi wakika wana michango mikubwa kwa kuharibu maisha ya watoto wao wa kike.
 

Forum statistics

Threads 1,250,699
Members 481,460
Posts 29,742,298