Baba kanumba ajibu mapigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba kanumba ajibu mapigo

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Dr. Chapa Kiuno, Feb 20, 2012.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  TAKRIBAN wiki moja tangu mwigizaji mstari wa mbele katika sinema za Bongo, Steven Charles Kanumba kuyafungukia maisha aliyoishi kwa baba yake mzazi, Charles Kusekwa Kanumba, mzee huyo amejibu mapigo, Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza kunasa sauti yake.
  KUMBUKUMBU ZA KUSIKITISHA
  Akizungumza kwa dakika 30 kwa njia ya simu kutokea Ngokolo, Shinyanga anakoishi, mzee huyo alizirarua moja kwa moja kauli za mwanaye alizozitoa kuhusu yeye alipohojiwa na Kipindi cha Take One kinachorushwa mawinguni na Runinga ya Clouds kwa msaada wa Mtangazaji Zamaradi Mketema.
  AANZA KUFUNGUKA
  Baada ya kujitambulisha na Ijumaa Wikienda kuweka sawa kinasa sauti chake, mzee huyo alisema: “Yote yaliyozungumzwa na Steven (Kanumba) si ya kweli na yametokana na mama yake mzazi.
  “Mama yake alinikimbia nyumbani na Steven akiwa mdogo kabisa, akaenda naye Bukoba na kumficha huko hadi alipougua, akashindwa kumtibu na kumrudisha hapa Ngokolo akiwa na miaka mitatu, akanibwagia.
  “Hapa nyumbani nilikuwa nimeshapata mke mwingine (anaitwa Rehema), tulimpeleka kutibiwa mpaka akapona na kupata afya, akawa kama wengine.
  “Huyu mke wangu anayesema alikuwa akimtesa, ndiye aliyemlea mpaka alipofikisha umri wa kuanza darasa la kwanza.
  Akiendelea kusimulia mkasa mzima, mzee huyo alisema: “Alianza shule hapahapa, akasoma hadi alipomaliza darasa la saba na kujiandaa kwenda sekondari.
  “Mama yake akaja tena kumchukua, akaenda kuishi naye kwake eneo la Kambarage. Sasa anaposema sikumpa malezi mazuri, ni yapi hayo?
  “Pia Steven katika kauli zake, amesema eti mimi na mama yake (wa kambo) tulikuwa tunamchungisha mbuzi na kuosha sana vyombo, wewe mwandishi hujakaa kijijini? Kuchunga mbuzi au ng’ombe mbona ni kawaida sana?
  “Kusema ukweli amenidhalilisha sana. Baada ya maneno yake yale nilimpa siku tatu aniombe radhi lakini alikataa, machozi yangu kwake yapo moyoni mwangu.”
  Ijumaa Wikienda: “Unamaanisha nini kusema akuombe radhi?”
  Baba Kanumba: “Kwa hizo kauli zake alizofundishwa na mama yake.”
  Ijumaa Wikienda: “Kwa nini unasema alifundishwa na mama yake? Kwani Kanumba alikuwa haoni anachofanyiwa kipindi yupo kwako?”
  Baba Kanumba: “Kuosha vyombo, kuchunga mbuzi, kupika ni kumnyanyasa mtoto? Si alikuwa akifundishwa jinsi ya kuishi kwa kujitegemea?”
  Ijumaa Wikienda: “Kwani hakukuwa na watoto wengine wa kumsaidia kufanya hizo kazi hadi akawa anafanya yeye?”
  Baba Kanumba: “Yeye ni mtoto wa mwisho, ilimpasa afanye kazi hizo. Tena nashangaa, amekuwa akija huku mara kwa mara na mama yake mdogo (Rehema) wanapatana sana.”
  “Mara nyingi amekuwa akija huku nyumbani, nyota yake ikishuka anakuja. Mwaka jana mwezi wa 9 alikuja, nyota yake ilikuwa imefifia, nikamtafutia kizizi ikarudi tena, si unaona amekuwa maarufu zaidi.”
  Ijumaa Wikienda: “Unataka kuniambia wewe ni mganga wa kienyeji?
  Baba Kanumba: “Hapana, lakini najua dawa za kumfanya mwanangu azidi kuwa maarufu.”
  KANUMBA MIKONONI MWA IJUMAA WIKIENDA
  Baada ya kuzungumza na mzee huyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kanumba na kumpasulia jipu kuhusu alichokisema baba yake.
  Kwanza alikiri namba iliyozungumza na Ijumaa Wikienda ni ya baba yake, kisha kwa huzuni kubwa, msanii huyo alianza kwa kusema: “Nimesikitishwa sana na uongo ambao amezungumza baba yangu.
  “Naamini kama angeangalia kipindi asingenijibu hivi. Mimi sikwenda kwenye kipindi kumsemea. Ila nilikuwa najibu maswali niliyoulizwa. Niliulizwa historia ya maisha yangu ikoje? Ndiyo nikaweka wazi.
  “Anachonilaumu yeye ni kipi? Kusema ukweli? Kama anaona nimemdhalilisha, anisamehe sana, lengo langu halikuwa kumdhalilisha. Lakini ukweli utabaki palepale.
  “Ikitokea siku nikaitwa kwenye runinga nyingine na kuulizwa, nitasema yaleyale kwa sababu ndiyo ukweli wangu, mimi sipendi kusema uongo.
  “Anaposema mama alinibwaga kwake nikiwa na miaka 3, ni uongo, mimi nilikwenda kwa baba nikiwa darasa la 4, mkubwa kabisa.

  YALIYOSITIRIKA YASEMWA
  “Mbona mama alimpeleka Ustawi wa Jamii akanikana, hajawaambia? Au anadhani sijui?
  “Kingine kinachoniuma ambacho sijakisema, (baba) ana tabia ya kuniomba fedha akidai anataka kufanyia kazi fulani au anakwenda kwenye matibabu, lakini kumbe sivyo.
  “Halafu mbaya zaidi nikimtumia fedha anawaambia watu pale mtaani acheni nizile fedha za mjinga. Inaniuma sana.
  “Pia, mimi sijawahi kwenda kwake kutaka dawa ya kukuza jina langu, kwanza wala hajui ilikuwaje nikaingia kwenye hii sanaa. Yeye alishtukia tu naonekana kwenye runinga.
  “Siwezi kutumia ushirikina ili niwe maarufu, mama kanilea kwa misingi ya dini na ugomvi wetu mkubwa alikuwa akitaka kila ninaposafiri nibebe Biblia kwenye begi.”

  Kuhusu kupewa siku tatu kuomba radhi?
  Kanumba: “Si kweli, tangu nilipohojiwa kwenye kile kipindi hajawahi kuniambia hivyo.”

  KUTOKA KWA MHARIRI
  Ni vema sana kwa familia ya Mzee Kanumba kukaa na kuondoa haraka hii tofauti. Baba Kanumba, kama ana udhaifu atakuwa anaujua, Kanumba vilevile atakuwa anajua wapi amemkwaza baba yake, wazungumze yaishe ili neno la Mungu lisemalo “tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna atakayemuona Mungu asipokuwa nao” lipate kutimia.

  BABA KANUMBA AJIBU MAPIGO - Global Publishers
   
 2. Nyundo Kavu

  Nyundo Kavu Senior Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Baba Kanumba: "Yeye ni mtoto wa mwisho, ilimpasa afanye kazi hizo. Tena nashangaa, amekuwa akija huku mara kwa mara na mama yake mdogo (Rehema) wanapatana sana."
  "Mara nyingi amekuwa akija huku nyumbani, nyota yake ikishuka anakuja. Mwaka jana mwezi wa 9 alikuja, nyota yake ilikuwa imefifia, nikamtafutia kizizi ikarudi tena, si unaona amekuwa maarufu zaidi."
   
 3. s

  shosti JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Zee jongo limejikamatisha hapo mwisho...
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Duu hatari kweli mbona sijui nimuamini nani mdingi au kanumba?
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mtoto wa Nyoka ni Nyoka..aliyofanya baba yake kama ni kweli anaonekana ni Nyoka na anayoyajibu Kanumba dhidi ya Baba yake anaonekana nae ni Nyoka...
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Haaaaa Tuliozoea jiji tunasema ngoma droo!
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  dah! Kumbe mtoto wa mwisho anatakiwa aoshe masufusia, achunge mbuzi, aoshe vyombo,afue,adeki,apike huku wenzie wamerilax?
   
 8. Nyundo Kavu

  Nyundo Kavu Senior Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  ndiyo tumepewa hiyo na Baba Kanumba,,,,,,, kazi ipo
   
 9. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  sipendi baba na mtoto kudhalilishana hadharani
   
 10. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kanumba mambo ya familia yako leo umeweka hadharani inakusaidia nini?mshukuru mungu unaishi na wazazi wako wanaishi na kama walikutenda vibaya si busara kuwadhalilisha wazazi,mimi kama mzazi sijapenda ulichofanya,mwombe mzee msamaha na wala usishindane naye
   
 11. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Nimekutana na wa2 wa karib na kanumba!Ukwel aloelezea kanumba tangu mwanzo inasemekana ni kwel!Na mkitaka mjue ukwel fuatlien kazi zke za filamu mtagundua uhalsia wa bakground yke!Bt kiujumla ni MFUMO WA MAISHA tu, thnx 2 God!Wte wasameheane!
   
 12. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  mzee kasema kweli kwa maisha ya mwanza hasa kijijini. Mimi pia nimechunga sana ng'ombe, mbuzi, kuvua samaki, kutengeneza matofali na kuuza kuni pamoja na mambo mengine magumu nikiwa nalelewa kwa baba mdogo. sijui na mimi nimlipue. but hata baba zetu walipokuwa wanaenda kurudia darasa la saba vijiji vya jirani hali ilikuwa hiyo hiyo, si kunyanyaswa ndo life style ya kijijini hasa ukiwa mdogo katika iyo familia
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nikweli kabisa ila tatizo nikwanini yeye 2 wakati anandugu zake? Any way yaliyopita yamepita asamehe na kusahau
   
 14. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  unapokuwa unamtendea mtoto utotoni bila kujua ya mbeleni halafu leo hii hataki ukweli ni mdhaifu na wapo wazazi wengi kama baba kanumba mwacheni kanumba aseme ukweli iwe fundisho kwa wengine
   
 15. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani kwa uelewa wangu, huyu mzee baba Kanumba'' anaonekana ni muongo, Kanumba yamalize na mzee wako sio vizuri kuanza kurushiana maneno kwenye vyombo vya habari...
   
 16. m

  mbweta JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mtoto wa mwisho lazima ufundishwe kazi ilo ni kweli mana yake angezaliwa mwingne angempokea kanumba hzo kazi kama ye alivopokea kwa nduguze.
   
 17. T

  TUMY JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeyapenda maneno aliyomaliza nayo mwandishi, ila yangu mimi ni machache tu wao wenyewe ndio wanaoweza kumaliza huo mzozo, mizozo kwenye familia hutokea na watu hukaa chini na kusameheana.Ni matumaini yangu yatakwisha mapema.
   
 18. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Iwe kweli au uwongo ila umaarufu!pesa!elimu au mionekano yetu isifanye tuwadharau wazazi wetu!!!baba na mama ni zawadi!
   
 19. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Vyovyote itakavyokua Kanumba sio wakuongea pumba kama hizo kwa baba yake, kama anataka tusikie tusiyo yajua yake
  aendelee kumchokonoa huyo babake,yatatoka mengi ajute kuzaliwa na huyo mzee.....
   
 20. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mmmh hii inaonyesha vipi familia za kiTZ bado zinaamini ushirikina. Nimesikitika!
   
Loading...