Baba kamuacha Mama, kaangaika na kupata maambukizi, kaugua mama kamuudumia kapata nguvu na kutaka kuendeleza mahusiano na Mama, Mama kagoma.

TOFU

JF-Expert Member
Aug 26, 2012
573
196
Wakuu nawasalimu kwa heshma na taadhima ...

Nianze kwakusema Baba alimuacha Mama na kuamua kuwa kijana wa Mambo mengi

Katika maangaiko yake kwa bahati mbaya akapata maambukizi ya VvU na kupelekea kuugua sana

Alipoenda kucheki afya aligundua tayari ni muadhirika wa UKIMWI

Ilhali Mama hakuwa na Maambukizi yoyote

Kipindi cha kwanza aliugua sana

Mama hakumuacha ila alimuuguza Mume wake mpaka alipopata nguvu

Kwa kumbukumbu zangu Baba alilala kitandani kama miaka saba (7) akiwa mgonjwa na kipindi chote hichi aliugizwa na Mke wake ambae ndio Mama mzazi

Balaa lilianza pale Baba alipopata nguvu na kutaka kuendelea na Mama ilhali alimuacha Mama kipindi akiwa mzima

Mama akagoma katu katu

Kila mmoja akawa na chumba chake japo wakawa wanaishi nyumba moja

Wachungaji wakajaribu kutatua mgogoro bila mafanikio

Ndugu nao wakajaribu bila mafanikio

Kwakuwa kulikuwa na ugomvi wa kila siku basi sisi watoto tuliamua Mama aishi nyumba tofauti japo kwenye boma moja

Baba akaamua kuleta Mwanamke mwingine

Mbaya zaidi yule Mama aliyeletwa kawa adui wa Mama pamoja na sisi watoto wake

Mpaka yale maeneo ambayo mzee alitugaia kama sehemu tutakazojenga makazi yetu nayo akabatilisha na kusema watoto tumeungana na Mama ili kumuangamiza yeye

Baba anataka Mama aondoke kabisa kwenye lile Boma au nyumba anayoishi kwa ushawishi wa Mama mpya aliyemleta!

Kiujumla sisi watoto wote ni watu wazima kila mmoja anajitegemea na hakuna tunachoitaji kutoka kwa Baba mzazi ila hatupo tayari kuungana na Mama wa kambo ili tumfurahishe Baba

Maana watoto tunaonekana wabaya kwasababu tu tunaonekana tupe upande wa Mama

Wakuu wangu,nahitaji ushauri wenu kwani naamini wengi humu mmenizidi kwa vingi ..

Jeh! niungane na Baba kwenye maamuzi yake ili anipe Mali au niendelee kuketi upande wa Mama kwasababu bado naona Mama hakutendewa haki

Najua fika mimi ni Mwanaume na sinui nitadondokea wapi ila naheshimu utu kuliko kitu ...!!

Kwa heshima zote ndugu zangu naomba kuwasilisha japo uwandishi wangu sio wakuridhisha ila natumai nimeeleweka ...
 
Hata mimi ningekuwa mama yenu nisingekubali mahusiano na mtu aliyeenda kubeba maradhi huko. Ningemsamehe ila maradhi yake abaki nayo. Tena huyo mama yenu ana roho nzuri sana kumhudumia miaka yote hiyo kwa kweli.
Mtoeni mama yenu hapo apate amani, anasimangwa na mali pamoja na wema wake aliofanya, huyo baba mwachieni mali zake yatamkuta tu siku moja atawatafuta mwenyewe. Haki ya mtu haipotei hata siku moja.
 
Hakika ...
Asante kwa Ushauri ...
 
Kuna wanawake wana laana kweli ya kutaka vya bure.. huyo mwanamke yake yatampata tu nae anayoyataka hataishi kuyafurahia.. hapo lazima anahesabu siku Baba yenu aitwe na Mola afaidi na ndio maana anataka msihusike tena. Ila na hao wachungaji na ndugu wengine wana majanga jamani.. duh!!!
Msali sana na Mola hatawatupa..

Mama yenu amwambie anataka ampe pa kuishi kabla hajatoka hapo.. kumbuka wamefika hapo huyo aliyeingia kavikuta hakusaidia kuvichuma.. achukue vyake.. msikubali ma alipo anaishi pake hapo hapo.

Umesema mko vizuri.. sasa unafikiria ya mali tena!!! Shikamana na Mama yenu aishi kwa furaha zaidi akijua mpo upande wake na mnasimama haki yake.. muache kumwendekeza huyo Baba yenu mkazieni haswaaa mkumbusheni alipotoka pia.. akigoma atajihu ila Mama yenu haki msimamie aipate.

Ila wanaume wengine mna roho za ajabu sana aiseee..
 
Waswahili husema "Tenda wema uende zako" japokuwa sio sahihi muda mwingine......

Mama amefanya sahihi kumuuguza baba lakini kitendo cha kumnyima unyumba amefanya makosa, japokuwa wewe kama mtoto usingeweza kushauri wazazi wako kama waendelee kupeana unyumba au laa.

Kwenye thread yako umeeleza kuwa "Wachungaji wakajaribu kutatua mgogoro bila mafanikio" Je walishajaribu kwenda kwa wataalamu wa Afya kupata ushauri????

Kabla hali haijawa hapo ilipofikia sasa (baba kuleta mke mwingine) haya ni baadhi ya mambo ambayo wazazi wako wangeweza fanya na kuishi ilihali baba ni positive na mama ni negative

1. WANGEWEZA PEANA UNYUMBA KWA KUTUMIA CONDOM

2. MZEE ANGEWEZA MEZA DAWA KWA USAHIHI MPAKA HALI YAKE IFIKIE STAGE INAYOITWA "UNDETECTED" YANI ANAISHI NA MAAMBUKIZI LAKINI HAWEZI MUAMBUKIZA MAMA HATA KAMA WASIPOTIMIA KINGA NA KWA HICHO KIPINDI CHA MIAKA SABA ALICHOUGUZWA KAMA ALITUMIA DAWA KWA USAHIHI NATUMAINI KWAMBA LAZIMA ATAKUWA YUPO UNDETECTED

3. MAMA ANGEWEZA TUMIA NJIA INAYOITWA PRE-EXPOSURE PROPHYLAXIS (PrEP) YANI ANGEWEZA NA YEYE KUTUMIA ARV KWAAJILI YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA HIV (STUDIES ZINASEMA NJIA HII HUWEZA KUMKINGA MTU HADI KWA ASILIMIA 99) NA PIA GUIDELINE MPYA INASEMA MTU ANAWEZA MEZA ARV KABLA YA KUFANYA TENDO TU NA BADO AKAWA SALAMA BILA KUPATA MAAMBUKIZI

NINI UNACHOWEZA KUFANYA WEWE KAMA MTOTO.

KAMA WAZAZI WAKO WAMEFUNGA NDOA NA NA INAONEKANA NI NDOA YA KIKRISTO AMBAYO NI YA MKE MMOJA TUU BASI BADO MAMA NDIO MKE HALALI WA MZEE BASI UNAWEZA MPA MAMA HUO USHAURI NILIOKUPA HAPO JUU, JINSI YA KUISHI NA MTU MWENYE MAAMBUKIZI BILA KUPATA MAAMBUKIZI.

KAMA MAMA AKIKUBALI KUMPA MZEE UNYUMBA NA MZEE AKAKUBALI KUPIGA CHINI NYUMBA NDOGO BASI MAISHA YANAWEZA RUDI KAMA ZAMANI

KAMA NILIVYOSEMA NI NGUMU KWA MTOTO WA KIAFRICA KUWAPA WAZAZI USHAURI JUU YA KUPEANA UNYUMBA BASI UNAWEZA TUMIA WATAALAMU WA AFYA WAKAMPA MAMA SHULE.

SISI WAZUNGU TUNAAMBIANA TUU NA WAZAZI WETU KUHUSU HAYO MAMBO UTASKIA "YOU GUYS CAN STILL HAVE SEX WITHOUT KUAMBUKIZANA"
 
Mama yenu ni mwanamke hasa mi kiukweli nikifinywa tu sisamehi kirahisi ijekuwa jitu limenitelekeza likaukwaa halafu nimuuguze miaka 7!!!! Kuwa mkweli siwezi

Simameni na mama yenu ikiwezekana muhamisheni hapo bomani kwenu
 
Dah wanaume nyie ni wabinafsi sana yaani bado unadiriki kusema huyo mama amekosea kumnyima unyumba mumewe!!!

Back
Top Bottom